Vikwazo 3 Vya Kushinda Ili Utimize Malengo Yako

Jinsi ya kutimiza MALENGO yako

Katika maisha kila mtu ana malengo au ndoto Fulani anayotamanai kuikamilisha ili aweze kufikia mafanikio. Hata wewe inawezekana una ndoto katika maisha yako unayotamani kuifikia. Inawezekana unatamani kufanya mambo makubwa kabla hujaondoka duniani. Lakini si wote wanaokuwa na malengo na ndoto katika maisha yao ambao wameweza kutimiza ndoto zao. Kuna sababu ambazo zinawafanya watu wengi washindwe kutimiza ndoto walizo nazo. Katika Makala ya leo nitakushirikisha vikwazo vitatu (3) ambavyo ni lazima uvishinde ili uweze kutimiza malengo yako.
Vikwazo 3 ambavyo ni lazima uvishinde kutimiza malengo yako.
1. Kutokuamini katika uwezo ulio nao.
Watu wengi sana wameshindwa kufikia kilele cha ndoto zao kwa sababu ya kutokuaminni katika uwezo walio nao. Hii inatokana na jinsi walivyoaminishwa toka wakiwa watoto, maneno ya walimu wao, maneno ya marafiki zao, mazingira waliyokulia na kadhalika. Wamekuwa wakisikia kwenye masikio yao maneno ya kukatisha tamaa kuwa hawawezi. Inawezekana hata wewe umekatishwa tamaa na wazazi, walimu, marafiki kuwa hauwezi. Ninataka nikuhakikishie kuwa una uwezo ndani yako wa kufanya makubwa na kutimiza malengo yako. Amini katika uwezo ulio nao na uchukue hatua. Amini kuwa una uwezo wa kuwa mtu mkubwa, amini kuwa unaweza kuwa bilionea na kadhalika. Usijidharau, una uwezo mkubwa sana uliojificha ndani yako ambao unachohitajika tu kufanya ni kuchukua hatua.
2. Kuamini kuwa kuna mtu yupo mahali fulani atakusaidia.
Katika maisha, hatma ya maisha yako unaipanga wewe mwenyewe. Hakuna mtu ambaye yupo kwa ajili ya kukusaidia katika maisha yako. Hata kama yupo, tambua kuwa sio wajibu wake kufanya hivyo. Hivyo ni lazima uchukue hatua wewe mwenyewe kwa asilimia mia moja kutimiza malengo yako. Kumbuka kuwa unapokuwa umeanza kuchukua hatua watu watakuja kukushika mkono wakiona tayari umekwisha anza. Kama malengo yako ni kuwa mwandishi, anza kuandika, kama ni kufanya biashara anza kwa kiasi chochote ulicho nacho. Hata kama hauna mtaji kabisa, tumia nguvu zako kuweza kupata mtaji wa kuweza kuanzisha biashara yako. Jambo la kuzingatia hapa ni wewe kuanza, haijalishi una hali gani. Unapokuwa umeanza, fursa zingine za kukufanya usonge mbele zitafunguka.
3. Kukata tamaa.
Kikwazo kingine ambacho kinaweza kukufanya ushindwe kutimiza malengo yako ni kukata tamaa. Watu wengi wameshindwa kutimiza malengo yao kwa sababu baada ya kuanza walipopata changamoto walikata tamaa na wakaamua kuacha malengo yao. Hata wewe inawezekana tayari umeamua kuchukua hatua, jambo la msingi ni kuendelea haijalishi utapitia changamoto kubwa kiasi gani, usikate tamaa. Endelea kupambana kwani mafanikio hayaji kwa urahisi, yanahitaji kujitoa kwa nguvu zako zote na akili yako yote. Hapa unatakiwa kupuuza maneno yote uliyoambiwa na ambayo unaweza kukutana nayo kuwa hauwezi. Maneno yoyote yale ambayo yatakuvunja moyo na kukukatisha tamaa yapuuze na upige hatua na mafanikio utayaona. Kama bado haujachukua hatua ni lazima utambue kuwa unapoanza kuchukua hatua kutimiza malengo yako kuna wakati utapitia nyakati ambazo zitakufanya ukate tamaa. Usikubali endelea kuchukua hatua mpaka pale utakapokuwa umetimiza kusudi la maisha yako.
Nimatumaini yangu kuwa umepata maarifa ambayo yatakusaidia kuchukua hatua muhimu sana kwa ajili ya kutimiza malengo yako. Kama una maoni au swali lolote, usisite kuweka maoni au swali lako hapa chini. Pia kwa ushauri wowote, usisite kuwasiliana nami moja kwa moja kwa simu no. 0752 081669. Asante na karibu tena kwenye Makala zinazokuja.

Kingi Kigongo
Ungana nae
Latest posts by Kingi Kigongo (see all)

3 Replies to “Vikwazo 3 Vya Kushinda Ili Utimize Malengo Yako”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error

Enjoy this blog? Please spread the word :)

Follow by Email
WhatsApp