
Hivi unajua kuwa watu wengi wanashindwa kuanzisha na kumiliki blog kwa kudhani kuwa ni kitu kigumu na kisichowezekana? Lakini ukweli ni kuwa kuanzisha na kumiliki blog ni jambo rahisi kuliko unavyoweza kufikiria. Hivyo katika makala hii nitakuelezea mambo sita ya msingi ya kuzingatia ili uweze kuwa na blog yenye mafanikio na Kutengeneza pesa kupitia blog yako.
Katika makala iliyopita iliyokuwa na kichwa cha habari kisemacho “Sababu kumi za msingi za wewe kuwa na blog yako mwenyewe ambayo itakuingizia kipato“, nilielezea kwa kina maana halisi ya blog na pia nilifafanua sababu za msingi ambazo wewe mpendwa msomaji wangu unapaswa kuwa na blog yako mwenyewe na namna ambavyo itakunufaisha na kuwa chanzo cha kukuingizia kipato.Kama hukuisoma makala hiyo nakushauri uanze kwanza kuisoma makala hiyo halafu ndio uendelee na makala hii.
Ili uweze kuanzisha blog na kutengeneza pesa kupitia blog yako, unapaswa kuzingatia na kufanyia kazi mambo yafuatayo :
Kutengeneza pesa kupitia blog: Mambo 6 ya kuzingatia.
1.Andika makala nyingi iwezekanavyo.
Ili uweze kufanikiwa kutengeneza pesa kupitia blog yako, unapaswa kuandika makala nyingi iwezekanavyo. Jiwekee ratiba na uifuate ya kuandika makala kila siku au kila baada ya siku mbili. Jambo la msingi ni kuwa, blog yako isikae muda mrefu bila kuweka makala mpya.
2. Penda Kusoma Sana
Ili uweze kuwa na vitu vingi vya kuandika kwenye blog yako, unapaswa kusoma sana kuhusiana na mada unazoandikia blog yako.
3. Wapende na kuwathamini wasomaji wako.
Jambo jingine la kuzingatia ili uweze kutengeneza pesa kupitia blog, jitahidi kusoma na kujibu maoni na maswali ya wasomaji wako mara tu yanapotokea. Kwa kufanya hivyo wasomaji wako watakupenda na kukuheshimu.
4. Usiogope kuandika.
Ili uweze kufanikiwa kutengeneza pesa kupitia blog, unapaswa kutokuogopa kuandika maarifa uliyonayo kuhusiana Mada unazoandikia blog yako. Usiwaze watu watakufikiriaje. Kumbuka kuwa maarifa au ujuzi ulionao ni wa thamani sana kwa mtu fulani na kwamba akiupata utamsaidia na atakushukuru.
5. Penda kujifunza vitu vipya kila siku kuhusiana na ujuzi wako.
Jambo jingine la kuzingatia ili uweze kutengeneza pesa kupitia blog ni kutambua kuwa wewe huwezi kuwa unajua vitu vyote, hivyo unapaswa kujifunza vitu vipya kila siku ili uweze kuandika makala bora na zenye kugusa jamii.
6. Kuwa na subira.
Mafanikio katika blog hayapatikani kwa siku moja. Hivyo endelea kuandika makala nyingi iwezekanavyo zinazoelimisha jamii,watu watakupenda,watakuheshimu na kukuthamini na matokeo yake utayaona baadaye.
Kwa leo niishie hapo. Kama una maoni au swali lolote kuhusiana na makala hii ya jinsi ya kutengeneza pesa kupitia blog, usisite kuandika hapo chini. Au unaweza kuwasiliana nami moja kwa moja kupitia namba yangu ya whatsap 0752081669.
Asante na karibu katika makala ijayo.
- Mbinu Tatu Rahisi Za Mafanikio Zinazopuuzwa. - August 9, 2024
- Jinsi Ya Kugundua Kusudi La Maisha Yako - August 7, 2024
- Kanuni za Kujiwekea Malengo - August 5, 2024
2 Replies to “Kutengeneza Pesa Kupitia Blog: Mambo 6 Ya Kuzingatia.”