
Kama unasoma Makala hii kwa sababu unahitaji kujua jinsi ya kutengeneza pesa(kipato) kupitia Blog, basi nikuhakikishie kuwa upo mahali sahihi.
Soma: Njia 10 za kutengeneza pesa mtandaoni bila kuathiri muda wako wa kazi
Katika Makala hii nimekuandikia njia 9 ambazo unaweza kuzitumia kujipatia kipato kupitia blog yako.
Jinsi ya kutengeneza pesa (kipato) kupitia Blog:Njia 9 unazoweza kuzitumia.
- Makala za kulipia(sponsored Blog Content)
- Kutangaza na kuuza Bidhaa za makampuni kwa lengo la kupata gawio(commisions)(Affiliate Programs)
- Kuweka matangazo ya Biashara kwenye Blog(Blog Advertisements)
- Kuuza kozi mbalimbali mtandaoni
- Kuuza bidhaa mbalimbali(Physical Products)
- Kuuza software mtandaoni
- Kuuza huduma zako mtandaoni
- Kuandika na kuuza Vitabu pepe (ebooks)
- Kuwa mshirika wa kibiashara na Makampuni mbalimbali.
Kama wewe ni mgeni kabisa kuhusiana na Blog, kabla ya kuendelea na Makala hii, unaweza kupitia Makala ya Jinsi ya kuanzisha Blog na kutengeneza pesa mtandaoni: Mwongozo rahisi wa jinsi ya kuanzisha Blog.
Kimsingi ,kuwa na blog yako mtandaoni ambayo tayari imekwishaanza kupata watembeleaji ni hatua ya kwanza kuelekea kuanza kujipatia kipato. Japokuwa ni jambo jema kufikiria njia ambazo unaweza kuzitumia kujipatia kipato kwenye blog yako hata kama ndio kwanza umeianzisha,Makala hii inawafaa zaidi wale ambao tayari wana blog zao na wameshaanza kupata watembeleaji na hivyo wanahitaji kuzipeleka blog zao katika hatua nyingine ambayo watakuwa wakijipatia kipato. Hivyo, kama bado hujaanzisha blog, unaweza kupitia Makala yangu ya Jinsi ya kuanzisha Blog na kutengeneza pesa : Mwongozo rahisi wa jinsi ya kuanzisha Blog.
Jenga msingi imara wa Blog yako kabla ya kufikiria namna ya kutengeneza kipato.
Kabla ya kwenda moja kwa moja kwenye njia za kuingiza kipato kupitia blog,hebu tujikumbushe kwa ufupi ni nini kinatakiwa ili uweze kuwa na blog yenye mafanikio.
Ili uweze kuwa na blog yenye mafanikio tuliona kuwa unapaswa kuchagua kwa uangalifu mada (niche),kuandika Makala zenye mvuto na kuitangaza blog yako ili uweze kupata wasomaji wengi. Hivyo baada ya kuwa umefanya mambo hayo yote ndio unaanza kufikiria jinsi ambavyo utajipatia kipato kupitia blog yako.
Sasa hebu tuangalie njia ambazo uanweza kuzitumia kutengeneza kipato kupitia Blog yako.
Jinsi ya kutengeneza pesa (kipato) kupitia Blog:Njia 9 unazoweza kuzitumia.
1. Makala za kulipia (Sponsored Blog Content)

Nini maana ya Makala za kulipia (sponsored content)? Hizi ni Makala ambazo Kampuni au mtu binafsi anakulipa ili uweze kuandika kwenye blog yako Makala ambayo itakuwa inaelezea Bidhaa au biashara ya kampuni yake. Kwa sababu blog yako itakuwa na wasomaji wengi, hivyo makampuni yanaweza kufanya makubaliano na wewe ili uandike Makala zinazotangaza biashara zao.
Hivyo baada ya blog yako kuwa na wasomaji wengi,unaweza kufanya makubaliano na makampuni mbalimbali au watu binafsi kuwatangazia biashara zao kupitia kuandika Makala kwa malipo.
Unapokuwa umepata kampuni au mtu binafsi ambaye ana bidhaa na anataka uandike Makala kuelezea bidhaa yake,hakikisha kuwa unakuwa mkweli kulingana na ubora wa bidhaa hiyo kwa wasomaji wako. Hii ni kwa sababu wasomaji wako watakuwa wanakuamini na hivyo chochote unachokiandika kwenye blog yako hakikisha kuwa kina ukweli ili kuendelea kujenga Imani ya wasomaji wako. Jambo la msingi ni kuwa hakikisha bidhaa au biashara ambayo utaamua kutangaza inaendana na mada za blog yako.
2. Kutangaza na kuuza Bidhaa za makampuni kwa lengo la kupata gawio(Affiliate Programs)
Hii ni njia nyingine ya kutengeneza kipato kupitia blog yako. Katika njia hii ya affiliate Program unajiunga na makampuni yanayouza bidhaa kwa lengo la kutangaza bidhaa zao.Baada ya kujiunga utapewa matangazo yenye link ambayo utayaweka kwenye blog yako.Kila mtu anayebofya link hiyo atapelekwa kwenye tovuti ya kampuni linalouza bidhaa hiyo. Kila mtu anayenunua bidhaa kupitia link yako wewe unalipwa kamisheni kutokana na mauzo ya bidhaa hiyo.Miongoni mwa makampuni yanayotoa huduma hii ni Amazon,Aliexpress na mengine mengi yaliyoko nje ya nchi. Kwa Tanzania kuna Dudumizi n.k
3.Kuweka matangazo ya Biashara kwenye Blog(Blog Advertisements)
Kuweka matangazo kwenye blog ni njia rahisi ambayo unaweza kuitumia kujitengenezea kipato.Hata hivyo njia hii kwa kuwa ni rahisi kipato utakachoingiza ni kidogo sana kama blog yako ina watembeleaji wachache. Miongoni mwa platform ambazo unaweza kujiunga na kuweka matangazo yao ni hizi zifuatazo:PropellerAds ,Google AdSense na mengine mengi.
4. Kuuza kozi mbalimbali mtandaoni.

Je una ujuzi au maarifa yoyote ambayo unaweza kufundisha watu wengine? Je wasomaji wako wanakuona kuwa wewe ni mtaalam katika ujuzi fulani?
Tengeneza kipato kupitia ujuzi wako kwa kuandaa kozi na kuiuza mtandaoni (creating an online course ) na hapo utakuwa umetengeneza mfereji wa kukuingizia kipato kwa muda mrefu .
Kuandaa na kuuza kozi mtandaoni ni njia rahisi kwani unaweza kurekodi video fupifupi zinazofundisha ujuzi ulionao kulingana na mada unayofundisha kwenye blog yako na ukazipangilia vizuri na kutengeneza kozi ambayo utaiuza mtandaoni kupitia blog yako.Kumbuka kuwa, kama una ujuzi fulani,watu wanahitaji ujuzi wako uweze kuwasaidia katika maisha yao na hivyo wako tayari kununua ujuzi huo. Kazi kwako!
Ushauri wangu unapokuwa unahitaji kutengeneza kipato kupitia kuandaa kozi mtandaoni, ni kwa kuanza kuandaa kozi fupifupi.
Jinsi gani unaweza kuandaa kozi yako ya kwanza mtandaoni?
Jambo la kwanza kabisa,utatakiwa kujua ni ujuzi au maarifa gani unayotaka kufundisha( na itachukua muda gani kwa mtu kujifunza ujuzi huo).
Baada ya hapo,fanya utafiti upate kujua kama ujuzi au maarifa hayo unayotaka kufundisha watu wanayahitaji.
Baada ya hapo,gawanya ujuzi unaotaka kuuandalia kozi katika masomo mbalimbali. Kwa mfano, una blog inayofundisha ujasiriamali na unahitaji kuaandaa kozi ya Jinsi ya kuanzisha Biashara. Hapa utatakiwa kugawa maarifa haya katika video fupifupi zizoelezea somo mojamoja kwa mfano:
- Nini maana ya Biashara
- Jinsi ya kupata wazo la Biashara
- Jinsi ya kuandika mchanganuo wa Biashara
- Hatua za kufuata ili kuanzisha Biashara
- Jinsi ya Kusajiri Jina la Biashara BLERA n.k
Video hizi utazipangilia kwa lengo la kufikisha ujuzi uliokamilika kwa msomaji wako na hivyo kumuwezesha kutatua changamoto aliyonayo na hivyo kubadili maisha yake.
Kwa kweli fursa ni nyingi sana kutengeneza kipato kupitia kuandaa kozi kwenye blog yako.Jambo la kuzingatia ni kuwa,hakikisha kozi unazoandaa ziendane na mada(niche) unayofundisha kwenye Blog yako.
Ifanye kozi yako ya kwanza kuwa rahisi na utaendelea kuboresha zaidi unavyoendelea kupata uzoefu unapoendelea kuandaa kozi zinazofuata.
5.Kuuza bidhaa mbalimbali(Physical Products)
Pia njia nyingine ambayo unaweza kuitumia kuingiza kipato ni kuuza Bidhaa zako mwenyewe. Unaweza kufungua duka la mtandaoni kwenye ukurasa mmojawapo wa blog yako na ukauza na watu wakanunua moja kwa moja kwenye blog yako.
Unaweza kutafuta supplier kutoka kwenye soko la mtandaoni la Alibaba na ukaagiza bidhaa kwa lebo yako na ukauzia watu kwenye blog yako.
6.Kuuza software mtandaoni.
Je wewe ni mtaalamu wa computer (developer)? Au kama sio wewe je una rafiki yako ambaye ana ujuzi huo? Kama una ujuzi huo,unaweza ukaanzisha blog inayohusiana na ujuzi ulio nao na kisha ukaandaa software ambayo utaiuza kupitia blog yako kwa wasomaji wako. Hii ni njia nzuri sana ambayo itakuletea kipato kikubwa na endelevu.
7.Kuuza huduma zako mtandaoni
Kuuza ujuzi ulionao kama huduma inakaribia kufanana na kuuza kozi mtandaoni.Tofauti inakuja kuwa unapouza ujuzi wako mtandaoni unakuwa ukitoa huduma kwa mtu mmoja mmoja au vikundi vya watu kwa kuongea nao na kutoa ushauri au huduma yako.Hivyo wanakulipa kwa kutoa huduma yako.
8.Kuandika na kuuza Vitabu pepe (ebooks)

Kuandika na kuuza vitabu pepe(ebooks) ni njia nzuri sana ya kutengeneza kipato kupitia blog yako.Uzuri wa hii njia ni kuwa ukiwa tayari umemaliza kuandika kitabu chako na kukiweka mtandaoni,huhitaji gharama zingine za ziada bali kitabu chako kitaendelea kukuletea kipato kwa muda mrefu wa miezi na miaka!
9. Kipato kupitia washirika wa kibiashara(Business Partnerships)
Pale unapokuwa na blog iliyofanikiwa na kuwa na wasomaji wengi,hapo utavutia washirika wengi wa kibiashara kuungana na wewe ili waweze kutangaza biashara zao kupitia blog yako. Hii ni kwa sababu utakuwa una mtaji mkubwa wa watu.Wanaweza kutumia blog yako kuuza bidhaa au kutangaza huduma zao na wewe wakakulipa.
Kama nilivyosema hapo mwanzoni mwa Makala hii,unatakiwa kwanza kukuza blog yako ndio uweze kufikiria jinsi ya kutengeneza kipato.
Je una swali au komenti yoyote? Usisite kudondosha komenti yako hapa chini! Pia kama una hitaji ushauri wowote, usisite kuwasiliana nami kwa simu namba 0752081669. Karibu katika makala ijayo.
- Mbinu Tatu Rahisi Za Mafanikio Zinazopuuzwa. - August 9, 2024
- Jinsi Ya Kugundua Kusudi La Maisha Yako - August 7, 2024
- Kanuni za Kujiwekea Malengo - August 5, 2024
7 Replies to “Njia 9 Za Kutengeneza Kipato Kupitia Blog.”