Jinsi Ya Kutumia Pesa Zako Vizuri Ili Ufanikiwe.

Jinsi Ya Kutumia Pesa Zako Vizuri Ili Ufanikiwe.

Katika maisha kila mtu huwa anapata kipato. Kipato hiki inawezekana kikawa kinatokana na ajira, kujiajiri au kufanya biashara. Hata wewe ninaamini huwa unapata kipato. Lakini, mafanikio katika maisha, hayatokani na kiwango cha pesa unachopata bali yanatokana na kiwango unachobakiza kwenye kila pesa inayopita mkononi mwako. Hii ndio sababu unaweza kuona mtu fulani alikuwa anapata kipato kikubwa lakini baada ya muda unashangaa kuona kuwa amezidiwa maendeleo na mtu ambaye alikuwa na kipato kidogo. Hivyo, ili uweze kufanikiwa na kuwa na uhuru wa kifedha, ni lazima ufahamu Kanuni za fedha za kuzingatia. Katika makala ya leo nitakushirikisha jinsi ya kutumia pesa zako vizuri ili uweze kufanikiwa na kuwa na uhuru wa kifedha.
Jinsi ya kutumia pesa zako vizuri ili uweze kufanikiwa.
Katika makala hii nitakushirikisha kanuni moja ya fedha iliyotungwa na Northcoste Parkinson’s. Kanuni hii inaitwa “Parkinson’s law”.
Kanuni hii inasema: Siku zote matumizi ya mtu huwa yanaongezeka kila mara kipato chake kinapoongezeka.
Hivyo, ili uweze kuwa na uhuru wa kifedha ni sharti ufanye maamuzi ya kupingana na kanuni hii ya Parkinson. Yafuatayo ni mambo ambayo unapaswa kuyafanya.

1. Hakikisha kuwa kipato chako kinaongezeka kwa kasi kuliko matumizi yako.
Hili ni jambo la kwanza kabisa na la muhimu kama unataka kuwa na uhuru wa kifedha. Maana yake ni kuwa, kama kipato chako kitaongezeka asilimia 20, basi ni sharti matumizi yako yawe chini ya asilimia 20.

2. Kuamua kujilazimisha kuendelea kuishi maisha uliyokuwa unaishi hata baada ya kipato chako kuongezeka.
Hapa inamaanisha kuwa, unaamua kuwa hautaongeza matumizi kwa kipindi fulani mpaka pale kipato chako kitakapofikia asilimia fulani. Lakini pia, hata kama utafikia asilimia ya ongezeko uliyokusudia, basi kama utaamua kuongeza matumizi basi yanatakiwa yawe chini ya asilimia ya ongezeko la kipato chako.
Lengo la kufanya hivyo ni kuhakikisha unabakiza pesa ya ziada ambayo utaitumia kwenye uwekezaji au kufanya jambo ambalo ni la kimaendeleo. Watu wengi wameshindwa kufanikiwa kwa sababu kila mara vipato vyao vilipoongezeka, waliongeza matumizi na hivyo kujikuta wanaendelea kuishi kwenye mzunguko wa kanuni ya Parkinson. Hivyo, kuanzia leo kama unahitaji kufanikiwa, hakikisha unavunja kanuni hii ili uweze kufanikiwa kwenye maisha yako.
Nimatumaini yangu umepata maarifa ambayo yatakusaidia namna ya kutumia pesa vizuri ili uweze kufanikiwa katika maisha kwa kuwa na uhuru wa kifedha. Kama una swali au maoni, basi usisite kuandika hapa chini. Pia unaweza kuwasiliana nami moja kwa moja kwa simu namba 0752 081669. Asante na karibu tena katika makala ijayo.

Kingi Kigongo
Ungana nae
Latest posts by Kingi Kigongo (see all)

One Reply to “Jinsi Ya Kutumia Pesa Zako Vizuri Ili Ufanikiwe.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error

Enjoy this blog? Please spread the word :)

Follow by Email
WhatsApp