
Mpendwa, nikukaribishe tena katika makala hii. Katika makala ya leo nitazungumzia jinsi unavyoweza kuongeza wasomaji kwenye blog yako. Njia nitakazoeleza hapa zitakusaidia kuongeza maradufu wasomaji wa blog yako na hivyo kupata mafanikio kwenye blog yako.
Soma:Kuanzisha blog: Sababu 10 za kuanzisha Blog yako.
Jinsi ya kuongeza wasomaji kwenye blog yako.
1. Andika makala mara kwa mara kwenye blog yako.
Weka makala mpya mara kwa mara kwenye blog yako. Unaweza kuandika makala, ukaposti picha au ukaweka makala za sauti (Podcasting).
Weka ratiba maalumu kwa ajili ya kuweka makala mpya kwenye blog yako.Ratiba husaidia kuwafanya wasomaji wako wajue ni wakati gani wategemee makala mpya.
2. Wasikilize wasomaji wako na ujibu maoni au maswali yao.
Miongoni mwa vitu vizuri sana ambavyo unaweza kuvifanya kwa wasomaji wako ni kuhakikisha kuwa kila msomaji wako anafurahia kuwa kwenye blog yako. Weka kwenye blog yako ukurasa wa mawasiliano ili kama kuna swali uweze kulijibu haraka iwezekanavyo. Kama kuna maoni yoyote kwenye makala zako, jitahidi kuyajibu haraka. Kwa kufanya hivyo, utaweza kuongeza wasomaji kwenye blog yako.
3. Tembelea Blog zingine na majukwaa mbalimbali na uchangie mada zinazotolewa.
Ili uweze kuwa na wasomaji wengi kwenye blog yako, unatakiwa kushiriki kwenye blog za watu wengine kwa kuchangia maoni yako. Tafuta blog zinazoandika makala kama zako na uwe unatoa maoni yako. Unapokuwa unatoa maoni usisahau kutaja blog yako. Kwa kufanya hivyo utafanya blog yako kutambulika na hivyo kupata wasomaji wengi.
4. Alika miongoni mwa wasomaji wako kuandika makala.
Pia, ili uweze kuongeza wasomaji, unaweza kualika miongoni mwa wasomaji wako kuandika makala. Hii itasaidia kuifanya blog yako kuwa na makala zenye ladha tofauti.
5. Wasiliana na wasomaji wako kwa njia ya email.
Waalike wasomaji kujisajiri (subscribe) ili waweze kupata taarifa kila unapoweka makala mpya. Kuna namna nyingi ya kufanya wasomaji wajisajiri ili kupata taarifa kila unapoweka makala. Mojawapo ya njia hizo ni kuweka kifaa cha kukusanyia taarifa za wasomaji wako kama vile jina na baruapepe (email). Hivyo msomaji anapokuwa amependezwa na makala zako atajisajiri ili aweze kupata taarifa kila unapoweka makala mpya. Mfano wa kifaa hicho ni MailChimp
6. Unganisha blog yako na mitandao ya kijamii.
Miongoni mwa njia bora kabisa za kuongeza wasomaji wa blog yako ni kuiunganisha na mitandao ya kijamii kama vile facebook, twitter, Pinterest na LinkedIn .Mitandao hii ina watu mamilioni. Hivyo unapokuwa na kurasa kwenye mitandao hii na ukawa unashea makala zako, utapata wasomaji wengi.
7. Shirikisha wasomaji wako kutoa maoni yao kwa kuwauliza maswali.
Shirikisha wasomaji wako kwa kuwauliza maswali mbalimbali kuhusiana na makala unazotoa ili watoe maoni yao. Unaweza kukusanya maoni ya wasomaji kwa kuweka kifaa kinachoitwa Survey Monkey kwenye blog yako.
8. Zingatia blog yako kuonekana vizuri kwenye simujanja (smartphone).
Hakikisha kuwa blog yako inaonekana vizuri kwenye smartphone ili uweze kupata wasomaji wengi kwani kwa sasa watu wengi wanatumia simu za mkononi.
9. Andika mada tofauti tofauti kwenye blog yako.
Ili uweze kuongeza wasomaji wengi, unaweza kuchanganya mada tofauti tofauti kwenye blog yako. Lakini zingatia mada hizo ziwe zinaendana na malengo ya blog yako. Kwa mfano blog yako inahusu biashara, unaweza kuandika makala ya namna ya kuanzisha biashara, lakini pia unaweza kuchanganya makala kama vile namna ya kutangaza biashara kwenye mitandao ya kijamii n.k
Nimatumaini yangu kuwa umepata maarifa ambayo yatakusaidia kuboresha blog yako. Kwa maoni au ushauri usisite kuweka maoni yako hapa chini. Lakini pia unaweza kuwasiliana nami moja kwa moja kwa njia ya whatsap 0752081669.
Asante na karibu katika makala ijayo.
- Mbinu Tatu Rahisi Za Mafanikio Zinazopuuzwa. - August 9, 2024
- Jinsi Ya Kugundua Kusudi La Maisha Yako - August 7, 2024
- Kanuni za Kujiwekea Malengo - August 5, 2024
One Reply to “Jinsi Ya Kuongeza Wasomaji Kwenye Blog Yako.”