Jinsi Ya Kuanzisha Biashara Mtandaoni: 1. Utangulizi.

Jinsi ya kuanzisha biashara mtandaoni

Karibu mpendwa msomaji wangu katika mfululizo wa masomo haya ya Jinsi ya kuanzisha biashara mtandaoni. Katika masomo haya ambayo yanaanza leo, nitaelezea hatua kwa hatua jinsi ambavyo unaweza kuanzisha biashara yako mtandaoni na ukatengeneza kipato.

Katika masomo haya nitaelezea mambo mengi yakiwemo: Jinsi ya kuchagua wazo la biashara yako. Hii itakuwa ni sehemu ya kwanza kabisa. Na kisha nitaelezea jinsi ya kupima soko la biashara yako na hivyo kuwa na uwezekano wa kuuza. Kuangalia soko kwa ujumla itakusaidia kupata uelewa wa jinsi utakavyoingia katika soko la mtandaoni ukiwa na kitu cha kipekee na hivyo kukufanya ujulikane na kuliteka soko.

Katika masomo haya tarajia kufanya mazoezi machache ili kufahamu wazo bora la biashara yako, hii ni kwa sababu, mara nyingi tunaweza kuwa na mawazo mengi ya biashara yanayopita kwenye vichwa vyetu. Hivyo nitaelezea jinsi ya kuchagua wazo moja sahihi la biashara yako.

Pia inawezekana ukawa hauna wazo la biashara hata moja, nitakueleza jinsi ambavyo unaweza kupata wazo bora la biashara yako ya mtandaoni. Hivyo katika hatua hii nitahakikisha umepata wazo la biashara yako kabla ya kuendelea na masomo yanayofuata.

Unapokuwa umepata wazo sahihi la biashara itakusaidia kuhakikisha kuwa unaokoa muda na pesa nyingi iwezekanavyo ambazo ungeweza kuzipoteza kwa kuwa na wazo lisilo sahihi la biashara. Kinachofurahisha sana katika mfululizo wa masomo haya ya Jinsi ya kuanzisha biashara mtandaoni ni kwamba, nitakuwa nikifanya mazoezi haya na wewe, kwa hiyo tutaweza kupata wazo bora na sahihi kwa ajili ya biashara yako.

Katika mfululizo wa masomo haya, tutajifunza masomo yafuatayo:

2. Biashara inayolipa mtandaoni ni ipi?

3. Jinsi ya kutafuta wazo bora la biashara yako ya mtandaoni.

4. Jinsi ya kugundua biashara unayopaswa kufanya (Discovering your niche).

5. Jinsi ya kufanya utafiti wa wateja wako (Researching your customers)

6. Jinsi ya kuchagua aina ya biashara yako (Positioning Your Business Idea)

7. Jinsi ya kushirikisha watu wa karibu wazo lako la biashara.

8. Jinsi ya kutathimini wazo la biashara yako.

9. Jinsi ya kuweka malengo ya biashara yako.

10. Jinsi ya kuweka mikakati na mwelekeo wa biashara yako ( Mind map)

11. Jinsi ya kuboresha mikakati ya biashara yako.

12. Jinsi ya kuweka mfumo wa biashara yako (business model).

13. Jinsi ya kupokea mrejesho wa wateja wako (Connecting for feedback).

14. Jinsi ya kufanya marekebisho kutoka kwenye mrejesho wa wateja wako.

15. Jinsi ya kuweka mwelekeo wa biashara yako.

16. Jinsi ya kuanza kuuza bidhaa yako kabla ya kuitengeneza.

17. Jinsi ya kuboresha biashara yako ya mtandaoni.

18. Jinsi ya kuuza na kulipwa mtandaoni.

19. Jinsi ya kufuatilia wateja ili waweze kununua bidhaa yako mtandaoni.

20. Jinsi ya kukuza biashara yako.

Bonus.

21. Jinsi ya kutengeneza brand na kuwa na tovuti yako ya biashara.

Nimatumaini yangu tutasafiri pamoja kwenye mfululizo wa masomo haya. Kama una maoni au swali lolote usisite kuandika hapa chini. Pia unaweza kuwasiliana nami kupitia simu namba 0752 081669. Asante na karibu kwenye somo linalofuata.

Kingi Kigongo
Ungana nae
Latest posts by Kingi Kigongo (see all)

4 Replies to “Jinsi Ya Kuanzisha Biashara Mtandaoni: 1. Utangulizi.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error

Enjoy this blog? Please spread the word :)

Follow by Email
WhatsApp