
Mojawapo ya majuto ambayo watu wengi hupitia hasa umri wao unapokuwa umekwenda ni kuwa, hawakuishi maisha waliyokuwa wanayataka na kufanya kile kitu walichokuwa wanakipenda. Na pia hawakufikia malengo yao ya maisha kama walivyokuwa wanatamani kufikia. Katika Makala hii tutaangalia jambo kubwa ambalo limewachelewesha wengi kufanikiwa kufikia malengo yao ambalo pia linaweza kukufanya ushindwe kufanikiwa kwenye malengo yako na jinsi ya kukabiliana nalo.
Tafiti nyingi sana zinaonesha watu wengi sana hasa wanapokaribia kufa hujilaumu maisha waliyoishi. Mwanasaikolojia mmoja anayeitwa Daniel Amend aligundua kanuni nzuri sana inayoitwa 18, 40, 60. Kanuni hii ilikuwa inasema hivi:
Mtu anapokuwa na umri wa miaka 18-39 huwa anajiuliza nikifanya jambo hili, kazi hii au biashara hii watu watanionaje? Watu wa kundi hili maisha yote yanaendeshwa na maoni ya watu na sio utashi wao.
Mtu huyu akifikisha umri wa miaka 40-59 huwa anaanza kusema, kwa sasa umri wangu umekwenda hivyo sitojali. Mimi nitafanya, mwenye kunisema na aniseme lakini mimi nitafanya ili kufanikiwa.
Mtu huyu anapofikisha umri wa miaka 60 na kuendelea anakuja kugundua kuwa, watu aliokuwa anawafikiria kuwa wanamuwazia yeye hawakuwa wanamfikiria kabisa na wala hawakuwa na mpango naye. Wao pia walikuwa wanahangaikia maisha yao.
Baada ya kuona kanuni hiyo utagundua kuwa ndivyo maisha yalivyo. Watu wengi wanaishi wakiogopa kufanya kitu ambacho kingebadilisha maisha yao wakifofia kuwa watu watawaonanje au kuwafikiriaje. Kumbe wale ambao wanawahofia na wao wana mambo yao na wala hawana muda wa kuwafirikia.
Jambo kuwa ambalo unapaswa kulizingatia ili uweze kufanikiwa ni kuwa, usiwe mtu wa kuishi ili kuwaridhisha watu. Ishi maisha yako. Kama una malengo ya maisha uliyojiwekea na unahisi kuwa ukiyafanya yatabadilisha maisha yako, fanya kwa nguvu zako na akili zako zote. Usihofu kuwa watakuonaje. Kumbuka kuwa hakuna aliye na muda wa kujali au kuangalia maisha yako. Ukiwaangalia na kuwahofia watu, unajichelewesha mwenyewe.
Mfano, watu wengi wanaishi kwenye nyumba zenye gharama kubwa kupita uwezo au kipato chao, wamechukua mikopo wakanunua magari ili kuwaridhisha watu, wananunua nguo za gharama kubwa kuliko uwezo wao. Hii ni kwa sababu walitaka kuwaridhisha watu na hivyo wakajikuta wapo kwenye msongo mkubwa wa madeni katika maisha yao.
Kitu cha msingi katika maisha yako ni kuishi maisha yako na kufanya kitu unachokipenda ambacho unaona kitaleta mapinduzi kwenye maisha yako bila kuangalia watu watasemaje. Nimatumaini yangu umepata maarifa ya msingi sana ambayo yatakusaidia kufanikiwa kufikia malengo yako. Kama una maoni yoyote, usisite kuweka maoni yako hapa chini. Pia unaweza kuwasiliana name moja kwa moja kama utahitaji ushauri zaidi kwa simu na. 0752 081669. Asante na karibu katika Malala ijayo.
- Mbinu Tatu Rahisi Za Mafanikio Zinazopuuzwa. - August 9, 2024
- Jinsi Ya Kugundua Kusudi La Maisha Yako - August 7, 2024
- Kanuni za Kujiwekea Malengo - August 5, 2024