
Karibu mpendwa katika makala hii. Katika makala hii nitazungumzia hatua 6 za kufuata ili uweze kuanzisha na kumiliki blog itakayokuletea pesa mtandaoni.Hivi unajua kuwa kwa kuanzisha blog unaweza kutumia elimu au ujuzi ulionao kujiingizia kipato mtandaoni bila kuathiri shughuli zako zingine?
Katika makala zilizopita nilielezea maana ya blog na sababu za msingi za wewe kuwa na blog yako mwenyewe. Kama hujapitia makala hiyo unaweza kuipitia halafu ndio uendelee na makala hii. Katika makala hii nitakuelezea hatua sita muhimu za kufuata ili uweze kuanzisha na kumiliki blog itakayokuletea kipato mtandaoni.
1. Chagua Mada (niche) utakayokuwa ukiandikia makala zako.
Hatua ya kwanza kabisa unapotaka kuanzisha blog ni kuchagua mada (niche). Blog nyingi huwa zinaelezea Mada moja. Kwa mfano, kuna blog zinazoandika michezo, habari, afya, elimu na mada zingine nyingi. Hivyo kama wewe una ujuzi wowote, chagua mada ya kuandika kwenye blog yako. Usichanganye mada nyingi kwenye blog yako.
2. Chagua Sauti yako ya kiuandishi (choosing your own voice)
Kitu kizuri sana ninachokipenda kwenye blog ni kuwa, kila mwandishi ana mfumo wake. Hivyo unaweza kuchagua mfumo wowote wa kiuandishi katika blog yako. Kwa mfano : unaweza kuwa unaandika makala katika mfumo wa kitaalamu au unaweza ukawa unaandika makala za kawaida.
3. Chagua vitu vya kuandika kwenye blog yako.
Baada ya kuchagua Mada ya kuandika kwenye blog yako, hatua inayofuata ya kuanzisha blog ni kuchagua mambo ambayo utaandika na yale ambayo hutaandika.
4. Andika makala nzuri na zenye mvuto.
Ili uweze kuwa na wasomaji endelevu kwenye blog yako, unapaswa kuandika makala zenye mvuto na zinazotatua matatizo ya jamii.
5. Tambua aina za makala utakazoandika.
Hatua nyingine ya kuanzisha blog ni kuchagua mtindo wa makala zako. Kuna aina nyingi za mitindo ya uandishi wa makala baadhi yake ni hii ifuatayo :
Mtindo wa kuorodhesha (List) .
Kwa mfano :Mambo sita ya kufanya ili uweze kufanikiwa katika maisha.
Mtindo wa kuandika dondoo (Tips)
Kwa mfano :Ukitaka kufauru mtihani, zingatia mambo yafuatayo.
Mtindo wa kuelezea (review) huduma au bidhaa .
Mfano :Maelezo kuhusu simu ya IPhone 6.
Mtindo wa kupendekezea (recommendation) bidhaa au huduma.
Mfano :Ukitaka kupiga picha zenye ubora camera ya cannon itakufaa.
Mtindo wa ‘jinsi ya ‘(how to)
Mfano :Jinsi ya kuanzisha blog.
Mtindo wa mahojiano (interview)
Mfano :Kutana na Bilionea Maganga aliyeanza biashara yake kwa kuuza ubuyu.
Mtindo wa kutumia video
Mtindo wa kurekodi sauti (podcast)
Mtindo wa kualika wataalam wa mambo mbalimbali (guest post) kuandika makala kwenye blog yako.
6. Weka ratiba nzuri ya kuweka makala zako.
Weka ratiba nzuri ya kuweka makala zako. Ninakupendekezea uwe unaweka makala kila siku, kila baada ya siku mbili, mara mbili kwa juma n.k. Jambo la msingi la kuzingatia hapa ni kuwa na ratiba maalumu ya kuweka makala zako ili uweze kuwa na wasomaji wengi watakaofuatilia blog yako.
Nimatumaini yangu kuwa umejifunza kitu katika makala hii ya hatua za kuanzisha blog. Kwa maoni au swali au ushauri, usisite kuwasiliana nami kwa whatsap 0752081669. Au unaweza kuweka maoni yako hapa chini.
Karibu katika makala ijayo
- Mbinu Tatu Rahisi Za Mafanikio Zinazopuuzwa. - August 9, 2024
- Jinsi Ya Kugundua Kusudi La Maisha Yako - August 7, 2024
- Kanuni za Kujiwekea Malengo - August 5, 2024
One Reply to “Hatua 6 Za Kuanzisha Blog.”