Jinsi Ya Kuandika Makala Zenye Mvuto Mtandaoni.

Jinsi Ya Kuandika Makala Zenye Mvuto Mtandaoni.

Kujifunza  jinsi ya kuandika Makala zenye mvuto ambazo watu watapenda kuzisoma na hivyo kuwa na wasomaji wengi kwenye blog yako si jambo gumu.Ni kweli, inachukua muda mrefu,nguvu pamoja na mazoezi ya kutosha ili uwe mwandishi uliyebobea.Lakini kama unahitaji kujifunza jinsi ya kuandika Makala ambazo zitapendwa na watu na kukuongezea wasomaji kwenye blog yako unaweza kuanza baada ya kuwa umesoma mpaka mwisho Makala hii.

Katika Makala hii ya jinsi ya kuandika Makala zenye mvuto tutazungumzia kila kitu kuanzia jinsi ya kuwatambua wasomaji wako,mpaka kwenye kanuni  ya jinsi ya kupata mawazo ya Makala zitakazopendwa na wasomaji wako,Jinsi ya kuandika vichwa vya habari vitakavyovuta usikivu wa wasomaji wako na kuwafanya wahamasike kusoma Makala zako,Jinsi ya kupangilia Makala zako ili ziweze kusomeka na kueleweka kwa urahisi na mambo mengine mengi..

Jinsi ya kuandika Makala zenye  mvuto zitakazopendwa na wasomaji na kukuletea pesa mtandaoni.

Jinsi Ya Kuandika Makala Zenye Mvuto Mtandaoni.
  1. Wafahamu wasomaji wako
  2. Andika kichwa cha habari kinachovutia kwenye kila makala yako
  3. Vuta usikivu wa wasomaji wako toka mwanzo wa makala yako
  4. Fanya makala zako zisomeke na kueleweka kwa urahisi.
  5. Tumia picha na vielelezo kwenye makala zako
  6. Andika makala zinazolenga kutatua changamoto ya msomaji.
  7. Hakikisha makala zako zinaonekana vyema hata kwenye simu za mkononi.
  8. Lenga zaidi katika ubora kuliko wingi wa makala.

1. Wafahamu vyema wasomaji wako.

Kabla ya kujifunza jinsi ya kuandika Makala, unatakiwa tayari uwe umechagua mada ambayo utakuwa ukiitumia kwenye blog yako,kwa kiingereza inaitwa niche. Kwa mfano inawezekana ukawa umeanzisha blog yenye mada(niche) ya Ujasiriamali. Hivyo unatakiwa uchague mada ambayo utaitumia kwenye blog yako.Mada ndio itakayoitambulisha blog yako kuwa inaelezea kuhusiana na mambo gani. Katika mada yako,chambua ni aina gani ya maarifa au Makala ambazo ukiandika zitatatua changamoto za wasomaji wako na hivyo kuwafanya wavute usikivu katika kusoma Makala zako. Andika vitu ambavyo wasomaji wako wanahitaji kujua na sio vile ambavyo wewe unataka kuwaambia.

Chambua kwa umakini changamoto zinazowakabili wasomaji wako na hivyo uweze kuandika maarifa ambayo kwa kweli ni hitaji lao.

2. Andika kichwa cha Habari kinachovutia kwenye kila Makala yako na kinacholenga kutatua changamoto zao.

Kichwa cha habari kinapokuwa kizuri na kinachovutia na kutatua changamoto kitaifanya Makala yako ipate wasomaji wengi.Hata unapoishare Makala yako kwenye mitandao ya kijamii, watu huanza kwanza kusoma kichwa cha habari kabla ya kusoma Makala yote. Hivyo ni muhimu kutatua changamoto ya msomaji kuanzia kwenye kichwa chako cha habari ili aone umuhimu na sababu yakusoma Makala yako.

Kabla hata watu hawajaanza kusoma Makala yako, kwa kusoma tu kichwa cha habari, wanakuwa tayari wamekwishaanza kuelewa unachoenda kuzungumzia.

Utafiti unaonyesha kuwa  watu 6 kati ya  10  hushare Makala kwenye mitandao ya kijamii kama vile Facebook,Twitter na LinkedIn kwa kusoma na kuvutiwa tu na kichwa cha habari.

Sasa unawezaje kuandika kichwa cha habari ambacho kitawavutia watu na kuwafanya wasome Makala yako na kuishare?

Sasa hebu tuangalie vitu vichache ambavyo unatakiwa kuvizingatia ili uweze kuandika kichwa cha habari kinachovutia

  • Tumia namba: Watu huwa wanatafuta mtandaoni njia rahisi ya kutatua changamoto zao.Hivyo ukiandika Makala ambayo ni mwongozo unaoonesha hatua kwa hatua jinsi ya kutatua jambo Fulani, watu watahitaji kusoma Makala hiyo.

Kwa mfano:Njia 10 za kutengeneza pesa mtandaoni

Pia unaweza kutumia mwaka kuonesha kuwa Makala yako ni ya muda huu na kuwa wasomaji wanapata maarifa ambayo hayajapitwa na wakati.

Kwa mfano:Sababu 8 za wewe kuanzisha na kuwa na Blog yako mwenyewe kwa mwaka huu wa 2021.

Angalizo: Usisubiri mpaka uwe umepata kichwa cha habari ambacho kimekamilika ndio uandike Makala,andika kichwa cha habari kadiri unavyoweza na utaendelea kuboresha kichwa chako cha habari .

Endelea kuandika Makala yako na mawazo ya vichwa mbalimbali vya habari yatakuwa yanakuja kwenye akili yako na baadaye utapata kichwa cha habari ambacho kitakufaa.

3. Vuta usikivu wa wasomaji toka mwanzo wa Makala yako.

Una sentensi moja mpaka mbili kuwafanya wasomaji wasome Makala yako au la. Hivyo kama unahitaji watu wasome Makala kwenye blog yako lazima uanze kwa sentensi ambayo itawavuta wawe na sababu ya kuendelea kusoma Makala yako.

Njia rahisi ya kuandika utangulizi mzuri ambao utawavuta wasomaji kuendelea kusoma Makala yako ni kuanza kwa kujibu Nani,Nini,wapi, lini haraka iwezekanavyo.

Katika kizazi hiki cha watu waliochoka kusoma unatakiwa kuweka pointi zako ziwe wazi badala ya kuzificha na msomaji aanze kuzitafuta.

Unapoweka pointi zako wazi mwanzoni unatoa sababu kwa msomaji kuendelea kusoma Makala yako.

4.Fanya makala zako zisomeke na kueleweka kwa urahisi.

Ni mara chache sana watu husoma neno kwa neno mtandaoni labda mpaka pale wawe wamevutiwa na Makala.

Utafiti unaonyesha kuwa ni 20% tu ya watu husoma maelezo mwanzo mwisho mtandaoni.Hivyo ili Makala zako zipate wasomaji unatakiwa kuandika katika mfumo wa kuorodhesha point(list).

Mambo mengine ya kuzingatia ni haya:

  • Aya za Makala yako ziwe fupi
  • Tumia maneno rahisi kueleweka na wasomaji.
  • Tumia mfumo wa kuorodhesha (list) kwenye makala zako.
  • Weka vichwa vidogo vya habari kwenye Makala zako
  • Unaposisitiza pointi tumia bolditalics, au saizi tofauti ya maneno.
  • Mara kwa mara tumia picha,chati na vielelezo kwenye Makala zako.

5.Tumia picha na vielelezo kwenye makala zako.

Watu wanapenda kuona picha.Hilo ni lazima ulifahamu linapokuja suala la kuandika Makala ambazo zitawavutia wasomaji wako.

Zaidi ya 50% ya ubongo wetu hupokea,kutunza na kufanyia kazi taarifa ambazo zipo katika mfumo wa picha , ukilinganisha na 8% kwa kugusa na 3% kwa kusikia.

Ili kuweza kuwa na Makala zenye mvuto kulingana na utafiti huo,ukiongeza picha kwenye Makala zako utakuwa umeongeza thamani,kuheshimika na kuaminika .

Wakati huo huo unapokuwa unaandika makala yenye makosa mengi unapoteza heshima na uaminifu ambao wasomaji wako watakuwa wameujenga kwako.

6.Hakikisha makala zako zinaonekana vyema hata kwenye simu za mkononi.

Kila mmoja anafahamu kuwa ili Makala iweze kufikia watu wengi Zaidi ni lazima iweze kusomeka kwenye vifaa mbalimbali zikiwemo simu za mkononi. Hivyo hakikisha Makala zako zinaweza kuonekana vizuri kwenye aina mbalimbali za vifaa zikiwemo simu za mkononi.

7.Lenga zaidi katika ubora kuliko wingi wa makala.

Ni kweli kuwa kuandika Makala nyingi na mara kwa mara kunaifanya blog yako ipate wasomaji wengi.Lakini kama Makala unazoandika hazilengi kutatua changamoto za watu muda sio mrefu watu wataikimbia blog yako.Hivyo wekeza katika kuandika Makala zenye ubora hata kama ni mara chache kuliko kuandika Makala nyingi zisizokuwa na ubora. Jambo la kuzingatia tu ni kuwa hata unaandika mara chache ,lazima uwe na ratiba maalumu ya kuweka Makala zako.

Asante kwa kuwa nami katika Makala hii.Je una komenti yoyote? Usisite kudondosha komenti yako hapa chini.Pia kama unahitaji ushauri, usisite kuwasiliana nami kwa simu au whatsap 0752081669.

Asante na karibu katika makala ijayo.

error

Enjoy this blog? Please spread the word :)

Follow by Email
WhatsApp