Kuna Tofauti Gani iliyopo kati ya Blog na Tovuti?

Kuna Tofauti Gani iliyopo kati ya Blog na Tovuti?

Watu wengi wamekuwa wakijiuliza na kushindwa kupambanua tofauti iliyopo kati ya blog na tovuti. Inawezekana hata wewe ni miongoni mwao. Katika makala ya leo nitakushirikisha tofauti iliyopo kati ya blog na tovuti na kipi uchague kama unataka kuanzisha biashara mtandaoni na kutengeneza kipato.

Blog ni nini?
Blog ni tovuti inayowekewa makala mara kwa mara kwa lengo la kuvuta wasomaji na hivyo kuweza kufikia malengo yaliyokusudiwa.Katika kila makala kunakuwa na sehemu ambapo msomaji anaweza kuandika maoni yake kuhusiana na makala hiyo au kuuliza swali.

Umekuwa ukisoma blog nyingi bila wewe kujua na hata sasa uko kwenye blog yangu. Inawezekana umewahi kusikia maneno blog na tovuti. Je unajua tofauti yake?
Katika Makala hii tutaangalia maana ya blog, tofauti iliyopo kati ya blog na tovuti na kipi unapaswa kuchagua kati ya blog na tovuti.

Kimsingi blog zote ni tovuti , lakini sio tovuti zote ni blog.

Tofauti iliyopo kati ya Blog na Tovuti.
Kabla hatujaangalia tofauti iliyopo kati ya blog na tovuti, hebu tuangalie kwanza historia fupi ya blog jinsi ilivyoanza mpaka sasa.

Historia fupi ya Blog
Blog zimekuwepo toka miaka ya 1993 na kwa sasa zina miongo miwili na nusu. Japokuwa kumekuwa na mjadala kuwa ni nani hasa mwandishi wa kwanza wa blog, kuna mtu mmoja anaweza kuwa ndiye mwandishi wa kwanza wa blog.

Mwaka 1993 Rob Palmer alianza kufanya kazi kwenye kampuni moja mjini London ambapo alikuwa akiandika makala za robo mwaka za kampuni na kuziweka kwenye tovuti ya kampuni.

Wakati Palmer alipokuwa akiandika makala kwa ajili ya kampuni yake, karibia mwaka mmoja baadaye blog nyingine ilianzishwa na Justin Hall. Blog yake ilikuwa na links na hivyo, watu wengine pamoja na makampuni wakagundua umuhimu wa kuwa na aina hiyo ya tovuti kwa ajili ya kubadilishana taarifa.

Wakati wa kipindi hicho blog zilijulikana kama “online journal” na “online diaries”. Mwaka 1997 mwandishi wa blog Mmarekani Jorn Barger aliziita blog kama “weblog,” ambapo kwa haraka sana zilibadilika jina kutoka “online diaries na online journals “ na kuwa “blog” kama tunavyolitumia leo.

Watengenezaji wa mifumo ya internet (Web developers ) kwa haraka waligundua kuwa watu walipendelea zaidi blog kuliko kitu kingine mtandaoni na hivyo wakaamua kutafuta suluhisho la kuboresha blog.

Mwaka 1998, Open Diary ilianzishwa. Hili lilikuwa ni jukwaa (platform) la watu kuandika makala zao na kubadilishana uzoefu wakati huohuo likiwa na sehemu ya watu kutoa maoni (comments). Platform zingine za blog zilianzishwa zikiwemo LiveJournal, Blogger, Tumblr na Xanga.

Ilipofika mwaka 2003, shughuli za blog zilibadilika kabisa pale ambapo wanachuo wawili walipotengeneza WordPress, mfumo bora kabisa (content management system (CMS)) ambao unachukua karibia mbili ya tatu ya tovuti zote zilizopo kwenye mtandao wa internet duniani leo.

Mwaka 2007, mifumo mingine ya blog (micro-blogging) ilianzishwa. Miongoni mwa mifumo iliyoanzishwa ilikuwa ni Twitter kwa lengo la watu kuandika makala fupifupi zenye maneno kati ya 300-400.

Mwaka 2016, WordPress ilianzisha mfumo kwa ajili ya blog ( .blog domain extension), hali ambayo ilizifanya blog kuendelea kuongeza umaarufu. Kwa sasa kunakadiriwa kuwa na  makala mpya millioni 70 zinazoandikwa na kuwekwa kwenye blog za WordPress kila mwezi.

Kuna tofauti gani kati ya Blog na Tovuti?

Kuna Tofauti Gani iliyopo kati ya Blog na Tovuti?

Tofauti kubwa iliyopo kati ya blog na tovuti ni kuwa, blog inawekewa makala mpya(dynamic) mara kwa mara wakati tovuti haiwekewi makala mpya mara kwa mara (static).

Na kama tulivyoona kabla, blog zote ni tovuti lakini si tovuti zote ni blog.
Tofauti nyingine kubwa ni kuwa tovuti huwa inakuwa na kurasa za msingi kama vile:

Mwanzo au Nyumbani (home),

Huduma zetu (service page) na

Wasiliana Nasi (Contact page).

Pia tovuti inaweza kuwa hata yenye ukurasa mmoja.

Kwa upande mwingine, blog ina kurasa kama zile zilizopo kwenye tovuti pamoja na sehemu ya kuweka makala mbalimbali ambayo kila mara makala mpya huwa zinawekwa.Kila makala huwa na sehemu ambayo wasomaji wanaweza kuuliza maswali au kutoa maoni yao.

Kila unapoweka makala mpya , makala mpya huoneana juu ya makala zingine za zamani. Hivyo wasomaji wako watakuwa wakiona makala mpya kwanza.

Kipi bora, kuwa na Tovuti au Blog?

Kumbuka nilisema hapo awali kuwa tovuti imeundwa na kurasa za msingi tu kwa mfano:

Masaa yako ya kazi,anuani au Menu.

Bidhaa unazouza.

Huduma unazotoa.

Hivyo hata ukurasa mmoja unaweza kutosha kuunda tovuti.

Lakini Blog huwa ina hizo kurasa zote ambazo tovuti inazo pamoja na ukurasa wa kuweka makala mpya (Post page).
Hivyo kama unahitaji kuwa unaweka makala mbalimbali ili kuwasiliana na wateja wako, nakushauri uwe na blog badala ya tovuti.

Blog ni njia nzuri sio tu ya kuwasiliana na wateja wako bali pia kuvutia wateja wapya kuja kwenye biashara au huduma unayotoa.

Kuna tofauti gani kati ya kurasa za msingi na kurasa za Makala (Post pages)?

Kurasa za Makala(Post pages):
1. Huwa zinawekewa makala mara kwa mara.
2. Kila makala huwa na kichwa cha habari na wakati mwingine vichwa vidogo vya habari.
3. Makala huwa zimepangiliwa kulingana na mwezi na mwaka zilipowekwa.
4. Makala huwa zimepangiliwa kulingana na makundi (categories).
5. Kila makala ina sehemu ya kuweka maoni (comments)
6. Kila makala ina jina la mwandishi na tarehe iliyowekwa.
7. Unaweza kuwa na makala zisizokuwa na idadi.

Kurasa za Msingi (pages):
1. Huwa na taarifa za msingi ambazo hazibadiliki mara kwa mara.
2. Taarifa hizi hazionyeshi kuwa ziliwekwa lini.
3. Kurasa hizi zimeandikwa si kwa lengo la kushare taarifa zake kwenye mitandao ya kijamii.
4. Hazina sehemu ya kuweka maoni (comments).
5. Hazina taarifa za mwandishi wala tarehe ya kuandikwa.
Idadi ya kurasa za msingi huwa ni ndogo.

Kurasa za msingi ambazo kila blog na tovuti zinapaswa kuwa nazo.
Hata kama blog yako ni kwa ajili tu ya kuandika makala mbalimbali, kurasa hizi zifuatazo unapaswa kuwa nazo.

1.Sisi Ni Nani (About page)
Ukurasa wa Sisi Ni Nani (The About Us Page) hutumika kuelezea kuwa Blog yako au Tovuti yako inahusika na nini.
Ukurasa huu unasaidia kuwaelezea watembeleaji wa blog au tovuti yako huduma unayotoa na hivyo kuwawezesha kufanya maamuzi kama huduma unayoitoa wanaihitaji au la. Katika ukurasa huu unaweza pia kuelezea kampuni yako, malengo na njozi za kampuni yako kuhusiana na huduma unayotoa.
Kama wewe ni mwandishi wa blog, unaweza kutumia ukurasa huu kuweka link za mitandao yako ya kijamii, kuwaomba wasomaji wako waungane na wewe (follow) kwenye mitandao ya kijamii, kuwasimulia wasifu wako kwa ufupi na kuwaelekeza makala muhumu kwao kuzisoma.

2. Wasiliana Nasi (Contact page)
Huu ni ukurasa ambao unaweza kuweka form ambayo watu wataweza kuwasiliana na wewe na kupata huduma unayoitoa.Pia unaweza kutumia ukurasa huu kuuza bidhaa au huduma unayotoa. Hii ni sehemu ambapo utaweka anuani yako ya barua pepe (email), Anuani yako na namba ya simu. Uwe ni mwandishi wa blog au mfanyabiashara ,unatakiwa kuweka mawasiliano yako wazi kupitia ukurasa huu ili watu waweze kukupata kwa urahisi.

3. Privacy policy page
Unapaswa kuwaambia watembeleaji wa blog yako kuwa unakusanya taarifa zao kwa mfano, email au hata kupitia kifaa cha Google Analytics ambacho huwa kinatoa takwimu za watembeleaji wa blog yako.

4. Vigezo na masharti (Terms of Service)
Ukurasa huu ni wa muhimu kama unauza bidhaa kwenye blog yako au unatangaza bidhaa za makampuni mengine kwa kulipwa gawio (commission). Ukurasa huu unaelezea jinsi ambavyo mteja pamoja na wewe mtoa huduma haki zenu zinalindwa kwenye biashara hiyo.

Hizi ndio kurasa nne ambazo kila tovuti inapaswa kuwa nazo.
Pamoja na kuwa na kurasa hizi, ninasisitiza tena kwa nguvu zote kuwa na blog kwenye tovuti yako.

Kwanini kila Tovuti inapaswa kuwa na Blog?

Kuna Tofauti Gani iliyopo kati ya Blog na Tovuti?


Kama tovuti yako imetengenezwa kwa kutumia  WordPress au platform zingine, inawezekana kabisa kuweka blog kwenye tovuti yako!
Hii ni kwa sababu: Unapokuwa na blog kwenye tovuti yako unakuwa na uwezo wa kuvutia watembeleaji wengi kwenye tovuti yako. Hii ni kwa sababu, kwenye blog utaweza kuandika makala nyingi zenye kuelimisha na hivyo kujenga mahusiano na wateja wako. Pia unapoandika makala nyingi kupitia blog, tovuti yako itaonekana zaidi watu wanapoitafuta kwenye Google na hivyo utapata watembeleaji wengi.

Kwa nini Unapaswa kuanzisha blog (Badala ya Tovuti)?
Tovuti ni nzuri kwa watu ambao tayari wana biashara na hivyo wanahitaji tu kutangaza biashara zao. Lakini hata na wao pia wanaweza kuweka blog kwenye tovuti zao ili wapate mahali ambapo watakuwa wakiandika makala mbalimbali na hivyo kuzifanya tovuti zao ziweze kuonekana kwa urahisi kwenye Google search engine.
Tovuti sio nzuri kwa mtu ambaye ndio anaanza na hana bidhaa yoyote wala huduma anayotoa.

Kwa mfano, kama wewe una duka la nguo, unaweza kuanzisha tovuti badala ya blog. Unaweza kuweka kurasa ambazo utawaelezea wateja wako huduma unazotoa, muda wa kazi , mawasiliano yako n.k.

Hata hivyo, kama huna bidhaa au huduma yoyote unayotoa, unaweza kuanzisha blog ukielimisha watu kutokana na ujuzi ulionao na baadaye utakapokuwa umepata wasomaji wengi wanaofuatilia blog yako ndio unaweza kuamua kuuza bidhaa au huduma kutokana na kile unachofundisha.

Jinsi Blog ilivyo na njia nyingi za kutengeneza pesa kuliko Tovuti.
Sasa hebu tulinganishe jinsi blog ilivyo na njia nyingi za kutengeneza pesa kuliko Tovuti.
Kama una tovuti (Isiyo kuwa na blog) una njia chache tu ambazo unaweza kuzitumia kutengeneza kipato kupitia tovuti yako.
Njia moja iliyozoeleka ni ile ya kuuza bidhaa au huduma kutoka kwa wateja ambao tayari unao. Pia wateja wengine wanaweza kukupata kwa kukutafuta kwenye search engine kama vile Google, kwa wewe kulipia matangazo Google au kwenye mitandao ya kijamii kama vile Facebook, Instagram n.k.

Kwa upande wa Blog, kuna njia nyingi sana za kutengeneza kipato. Uzuri wa blog ni kuwa unakuwa unatengeneza kipato huku ukielimisha jamii na kukuza jina (Brand) ya blog yako na wewe mwenyewe. Miongoni mwa njia hizo ni hizi zifuatazo:
1. Kuuza huduma mbalimbali unazotoa
2. Kutangaza na Kuuza bidhaa za makampuni mbalimbali kwa lengo la kupata gawio (commissions)
3. Kuuza bidhaa mbalimbali (Physical and Digital products)

1.Kuuza huduma mbalimbali unazotoa.
Kupitia makala ambazo utakuwa unaziandika na kuelimisha jamii, watu watakuamini na kukuona kuwa wewe ni mtaalamu wa mada unayofundisha ambaye unaweza kutatua changamoto zao. Hivyo unaweza kutoa huduma mbalimbali kwa malipo kutokana na utaalamu ulionao.

2.Kutangaza na Kuuza bidhaa za makampuni mbalimbali kwa lengo la kupata gawio (commissions)
Njia nyingine unayoweza kuitumia kujipatia kipato kwenye blog yako ni ile ya kutangaza na kuuza bidhaa za makampuni mbalimbali kwa lengo la kupata gawio (commissions) . Njia hii inajulikana kwa kiingereza kama Affiliate marketing. Kuna makampuni mengi yanayotoa huduma hii ambayo unaweza kujiunga na wakakupa link ambayo utaiweka kwenye blog yako. Kila msomaji atakayebofya link hiyo ataelekezwa kwenye tovuti ya kampuni husika ambapo kuna bidhaa au huduma inayouzwa. Iwapo mteja atanunua bidhaa au huduma hiyo, wewe unapata gawio. Miongoni mwa makampuni yaliyo na program hii ni amazon, Aliexpress na kwa Tanzania kuna getvalue n.k

3.Kuuza bidhaa mbalimbali (Physical and Digital products)
Kuuza bidhaa pia ni njia unayoweza kuitumia kujipatia kipato kupitia blog yako. Unaweza kuuza bidhaa zinazoshikika (Physical Products) au bidhaa pepe (Digital products).
Bidhaa pepe (Digital products) ni rahisi sana kutengeneza kwani unaweza kukusanya makala ambazo umekuwa ukiandika na kuziweka kwenye vitabu na ukauza vitabu pepe (ebooks) . Pia unaweza kutumia makala ulizoandika kuandaa kozi na kuiuza kwenye blog yako.

Kwa ufupi:
Katika Makala hii tumeangalia tofauti ya blog na tovuti . Swali langu kwako ni kuwa baada ya kusoma Makala hii, utachagua kipi kati ya blog na tovuti?
Je una biashara na unataka iwafikie watu wengi zaidi au unahitaji kujiajiri kupitia mtandao wa internet kwa kutoa maarifa yako kwa jamii huku ukijipatia kipato?
Vyovyote vile kati ya mambo hayo mawili Blog itakuwezesha kuyatimiza kikamilifu.
Je una maoni yoyote? Usisite kudondosha maoni yako hapa chini.

Jinsi Ya Kutumia Ujuzi Wako Kujiajiri Mtandaoni

Jinsi ya kutumia ujuzi wako wako kujiajiri Mtandaoni

Katika maisha, kila mtu ana ujuzi wake. Ujuzi huu unatokana na kusomea chuoni, kufundishwa nyumbani au mtaani. Hata wewe inawezekana una ujuzi ambao umesomea chuoni au umejifunza mahali fulani. Changamoto kubwa ambayo inajitokeza hapa ni kwa jinsi gani unaweza kutumia ujuzi wako kujiajiri na kutengeneza kipato. Katika makala hii nitakushirikisha jinsi ya kujiajiri mtandaoni na kutengeneza kipato kwa kutumia ujuzi wako.
Katika makala yangu ya njia 10 za kutengeneza pesa mtandaoni nilielezea kwa ufupi njia ambazo unaweza kuzitumia kuweza kujiajiri mtandaoni na kutengeneza kipato. Katika makala hii nitaelezea kwa kina njia moja ya kujiajiri mtandaoni ambayo ni kuanzisha blog. Hapa nitazungumzia jinsi unavyoweza kujiajiri kwa kuanzisha blog ya kitaalamu (niche blog).
Maana ya blog ya kitaalamu (niche blog).
Niche blog au kwa Kiswahili blog ya kitaalamu ni aina ya blog ambayo imejikita katika kufundisha ujuzi wa aina moja. Hapa ina maanisha kuwa, kama wewe una maarifa au ujuzi wa kilimo, basi blog yako itajikita katika kufundisha kilimo tu bila kuchanganya mambo mengine yasiyohusu kilimo. Vivyo hivyo, kwa ujuzi wa aina nyingine kama vile Sheria, Biashara, Elimu, Afya, Mapambo, Mitindo, Ujasiriamali na kadhalika.
Hivyo, kwa kutumia ujuzi au maarifa yoyote uliyonayo, unaweza kuanzisha blog inayotatua changamoto zinazoihusu jamii yako kupitia ujuzi ulionao. Jambo la kuzingatia ni kuwa, unapokuwa umeanzisha niche blog, lenga kundi la watu wanaohitaji ujuzi wako na ujitahidi kuandika makala zinazoelimisha na kutatua matatizo ya kundi hilo. Usichanganye mada. Kama umeamua kuanzisha blog ya kufundisha mapishi au ujasiriamali, usichanganye na mada za siasa. Hii ni kwa sababu, watu watakaokuwa wasomaji wa blog yako ni wale wanaohitaji ujuzi wako na si vinginevyo.
Kwa nini unapaswa kuwa na blog ya ujuzi au utaalamu wako?
Sasa hebu tuangalie ni faida gani utazipata unapokuwa umeanzisha blog ya ujuzi au utaalamu wako.
1. Utapata wasomaji wanaopenda kufuatilia maarifa au ujuzi wako (Loyal readers)
Ukiwa na blog ya kufundisha utaalamu wako, utapata watu wenye changamoto katika jamii wanaohitaji ujuzi wako ili waweze kutatua changamoto zao. Hivyo, watu watakupenda na kukuheshimu kwa sababu unawasaidia kutatua changamoto zao.
2. Utajenga mtandao mkubwa (community) wa watu wenye ujuzi kama wa kwako na wanaopenda kujifunza ujuzi wako.
Kwa kuwa na mtandao mkubwa wa watu wenye ujuzi kama wa kwako, mtaweza kubadilishana maarifa na hivyo kukuza ujuzi wako.
3. Utatambulika katika jamii kuwa wewe ni mtaalamu.
Unapokuwa umeanzisha blog ya utaalamu wako, na ukawa unaandika makala zinazotatua matatizo katika jamii, jamii itakutambua kuwa wewe ni mtu wa kutegemewa.
4. Utakuza jina lako (Brand, Credibility and Profile)
Ukiwa unaandika makala zinazoelezea mada moja kwa muda mrefu, utaifanya blog yako iwe ni sehemu inayoaminika na kuheshimika (trusted source) kwa maarifa unayofundisha. Ukifanya hivyo kwa usahihi, utatambulika kuwa ni mtaalamu uliyebobea kwenye kada unayofundisha.
Faida za kuwa mtaalamu uliyebobea ni nyingi. Mojawapo kubwa ni pale utakapokuwa na bidhaa au huduma unayotaka kuuza. Badala ya kuanza kusaka wateja, utashangaa kuwa watu ndio watakutafuta wewe wakihitaji huduma yako kwa kuwa wanakutambua kuwa wewe ni mtaalamu uliyebobea.
5. Utaweza kuuza bidhaa zako.
Unapokuwa na blog inayoelezea mada au ujuzi wa aina moja, ni rahisi kuuza bidhaa zinazoendana na ujuzi unaofundisha na watu wakanunua. Hii ni kwa sababu, wasomaji wa blog yako watakuwa ni wale wanaopenda na kuhitaji ujuzi wako. Mfano: Ukiwa na Blog ya Ujasiriamali, ni rahisi kuuza vitabu, kozi au bidhaa zinazohusu ujasiriamali. Kadhalika kwa blog zenye ujuzi wa aina nyingine.
6. Ni rahisi kupata watu au makampuni ya kuweka matangazo kwenye blog yako.
Ukiwa na blog yenye mada au ujuzi wa aina moja, ni rahisi kupata watu au makampuni yanayotoa huduma inayofanana na ujuzi wako na wakahitaji kuweka matangazo yao ya biashara. Kwa mfano: Kama blog yako imejikita katika kuelezea mitindo mbalimbali ya nguo, ni rahisi kupata watu wanaohitaji kutangaza bidhaa zao za nguo kwenye blog yako, nao wakakulipa kwa kuweka matangazo yao.
7. Blog yako itaonekana kwa urahisi watu wanapoitafuta Google (Search engine optimization).
Google huwa inatoa kipaumbele kwa blog zinazoelezea mada ya aina moja. Hivyo blog yako itaonekana kwenye ukurasa wa kwanza. Kwa mfano: kama blog yako inahusu ufugaji wa kuku, na mtu akaandika neno ufugaji wa kuku Google, blog yako itaonekana juu kwa sababu, ina makala nyingi za ufugaji wa kuku.
8. Utaweza kuandika makala nyingi.
Unapokuwa unafundisha ujuzi unaoupenda, utakuwa na vitu vingi vya kuandika. Hivyo kila siku utakuwa unapata mawazo na maarifa mapya ya kuandika kwenye blog yako.
9. Blog yako haitapata ushindani mkubwa (Less competition)
Blog za kitaalamu huwa ni chache na huwa zinalenga kundi fulani la watu. Hivyo, unapokuwa unaandika makala zenye mada ya aina moja, utapata faida ya kutokupata ushindani mkubwa mtandaoni.
Ni matumaini yangu kuwa umepata maarifa ya jinsi ya kujiajiri mtandaoni kwa kutumia ujuzi wako. Kama utahitaji kuanzisha blog wewe mwenyewe, nimeelezea kwa kina na hatua kwa hatua jinsi ya kuanzisha blog kwenye makala yangu ya Jinsi ya kuanzisha blog na kutengeneza kipato. Pia kama utahitaji huduma ya kutengenezewa blog, unaweza kuwasiliana nami kwa simu namba. 0752 081669. Kama una maoni au swali lolote kuhusiana na mada hii, usisite kuweka maoni yako hapa chini. Asante na karibu kwenye makala zijazo.

Faida 10 Usizozijua Za Kuanzisha Blog Yako.

Faida 10 za Kuanzisha blog


Kwa nini unapaswa kuanzisha blog? Kama limekuwa ni swali ambalo umekuwa ukijiuliza kwa muda mrefu, basi nikuhakikishie kuwa, makala hii ni kwa ajili yako. Katika makala hii, nitakushirikisha faida 10 usizozifahamu za kuanzisha blog yako.
Kabla ya kuendelea kwenye faida za kuanzisha blog, hebu kwanza nizungumzie maana ya blog pamoja na aina zake.
Maana ya blog.
Kwa tafsiri rahisi, blog ni aina ya tovuti. Aina hii ya tovuti inakuwa na vitu vifuatavyo:
i. Makala: Blog inakuwa na makala ambazo zinaandikwa mara kwa mara. Kila makala moja inapoandikwa inakuwa juu ya makala ya zamani. Kwa mfano, kama uliandika makala juzi na jana, makala ya juzi itakuwa chini ya makala ya jana. Mfano mzuri wa blog ni hii uliyopo kwa sasa.
ii. Sehemu ya kuweka maoni: Kila makala inapowekwa kwenye blog, kwa chini yake huwa kunakuwa na sehemu ya kuweka maoni. Hivyo, kama msomaji atakuwa amepata swali au maoni yoyote kuhusiana na makala husika, ataweza kuweka maoni yake kwenye sehemu ya kuwekea maoni.
iii. Maktaba: Hii ni sehemu ambayo makala zote za blog zilizowahi kuandikwa huhifadhiwa.
Aina za Blog.
Kuna aina nyingi sana za blog na nitakutajia aina chache tu kama ifuatavyo:
i. Blog binafsi (Personal blog)
Hizi ni blog ambazo huanzishwa na watu binafsi ili kuelezea mambo yao binafsi ya ki-maisha.
ii. Blog za biashara.
Hizi ni blog ambazo huanzishwa na watu au wafanyabiashara ili kutangaza bidhaa au huduma zao na kuweza kuwasiliana na wateja wao.
iii. Blog za kitaalamu.
Hizi ni blog ambazo huanzishwa na watu ambao ni wataalamu wa fani fulani ili kuweza kutoa elimu kutokana na utaalamu wao. Kwa mfano, kuna blog za kilimo, afya, elimu, mapambo, mapishi, mitindo na kadhalika.
iv. Blog za habari.
Hizi ni blog zinazotoa habari na matukio yanayotokea kila siku. Mfano blog ya Milladayo.
v. Blog za Burudani.
Hizi ni blog zinazoandika habari za michezo na burudani. Mfano blog ya Salehe Jembe.
Faida 10 Za kuanzisha Blog.
Kuna faida nyingi sana za wewe kuanzisha blog. Miongoni mwa faida hizo ni hizi zifuatazo:
1. Blog itakujengea ujasiri na kufahamika.
Ukiwa na blog utaweza kufahamina na watu wengi na hivyo kukuza jina lako. Kutokana na kukuza jina lako, utakuwa na followers wengi. Hivyo, ukihitaji kuuza bidhaa au huduma, tayari utakuwa na mtaji wa watu wengi wanaokufahamu.
2. Kupata watembeleaji wengi (Traffic) kwenye bidhaa au huduma unayotoa.
Kama utakuwa unauza bidhaa au unatoa huduma mtandaoni, unapokuwa na blog na ukawa unaandika makala mbalimbali za kuelimisha, utapata watembeleaji wengi kwenye blog yako na hivyo utaweza kuwauzia bidhaa au huduma unayotoa.
3. Kuongeza wigo wa marafiki (Network)
Unapokuwa na blog, utaweza kufahamiana na watu wengi kutokana na makala unazoandika na hivyo kuweza kukuza mtandao wa marafiki.
4. Kuongeza Mauzo (Sales)
Pamoja na kufahamiana na kuongeza mtandao wa marafiki, makala unazoandika zitakufanya uaminike (Trust) na kukujengea heshima (credibility) mambo ambayo ni ya msingi katika kuongeza mauzo ya bidhaa au huduma unayotoa.
5. Kujifunza zaidi.
Ili uweze kuandika makala mara kwa mara, utatakiwa kujifunza zaidi. Hivyo, kwa kuwa na blog, itakufanya uweze kujifunza kila siku mambo mapya kutokana na mada unayoandikia kwenye blog yako.
6. Kuibadilisha jamii kwa kufanya vitu vya tofauti.
Kama una maarifa ambayo ufikiria ukiyatoa kwa jamii yako yataleta mabadiliko, basi, kwa kutumia blog utaweza kuielimisha jamii yako na jamii itakupenda na kukuheshimu.
7. Utaweza kuwasaidia watu.
Kama una ujuzi wowote ambao inawezekana ni wa kujifunza au umesoma chuoni, kwa nini usiwashirikishe watu ujuzi ulionao? Kwa kutumia blog, utaweza kuwashirikisha watu ujuzi wako nao watakupenda na kukuheshimu.
8. Utaweza kutangaza biashara yako.
Kama una bidhaa au huduma yoyote, blog ni sehemu nzuri sana ya kuweza kutangaza biashara yako.
9. Jamii itakutambua kuwa wewe ni mtaalamu (Expart)
Unapokuwa na blog, utaweza kuelimisha jamii ujuzi ulionao. Hivyo, jamii itakueshimu na kukutambua kuwa wewe ni mtaalamu wa fani au ujuzi huo.
10. Utatengeneza pesa.
Unapokuwa na blog na blog yako ikawa na watembeleaji wengi, utaweza kutengeneza pesa. Katika kutengeneza pesa, kuna njia nyingi ambazo unaweza kuzitumia. Njia hizo zimegawanyika katika makundi mawili ambayo ni:
i. Njia za moja kwa moja (Direct methods)
ii. Njia zisizo za moja kwa moja (Indirect method)
i. Njia za moja kwa moja ni (Direct methods)
Njia za moja kwa moja ni njia ambazo utapata kipato moja kwa moja kutoka kwenye blog yako. Ingawa njia hizi sikupendekezei uzitumie kwenye blog yako kwani ili uweze kupata kipato kupitia njia hizi, ni lazima blog yako iwe na watembeleaji wengi. Mojawapo ya njia hizo ni:
-Kuweka matangazo ya biashara kwenye blog yako (Advertisements)
-Kupata makampuni yatakayodhamini blog yako.
Undani wa njia hizi nimeuelezea kwenye makala yangu ya njia za kutengeneza kipato kupitia blog.
ii. Njia zisizokuwa za moja kwa moja (Indirect methods)
Hizi ndio njia ambazo ninakushauri uzitumie, kwani zitakupatia kipato kikubwa hata kama blog yako itakuwa na watembeleaji wachache. Njia hizo ni pamoja na:
Kuandika na kuuza vitabu pepe (ebooks) kutokana na makala unazoandika.
Kuandaa kozi za mtandaoni kutokana na mada unazoandika na kuziuza kwa wasomaji wako.
-Kutoa huduma za kitaalamu za kulipia kwa wasomaji wako.
-Kuuza bidhaa zako zingine kwa wasomaji wa blog yako.
Njia hizi zote, nimezielezea kwa kina kwenye makala yangu ya njia za kutengeneza kipato kupitia blog.
Pia kama unahitaji kujifunza kutengeneza blog yako wewe mwenyewe, unaweza kupitia makala yangu ya jinsi ya kuanzisha blog, ambapo nimeelezea kwa kina na kwa lugha rahisi, jinsi ambavyo utaweza kuanzisha blog yako wewe mwenyewe. Lakini pia kama utahitaji huduma ya kutengenezewa blog, basi unaweza ukawasiliana nami kwa simu no. 0752 081669.
Ni matumaini yangu, kuwa umepata maarifa ya kutosha kuhusiana na faida za kuanzisha blog yako. Kama una swali au maoni, usisite kuandika hapo chini. Pia unaweza kuwasiliana nami moja kwa moja kwa kutumia na. 0752 081669. Asante na karibu tena kwenye makala zijazo.

Kutengeneza Pesa Kupitia Blog: Mambo 6 Ya Kuzingatia.

Kutengeneza Pesa Kupitia Blog: Mambo 6 Ya Kuzingatia.

Hivi unajua kuwa watu wengi wanashindwa kuanzisha na kumiliki blog kwa kudhani kuwa ni kitu kigumu na kisichowezekana? Lakini ukweli ni kuwa kuanzisha na kumiliki blog ni jambo rahisi kuliko unavyoweza kufikiria. Hivyo katika makala hii nitakuelezea mambo sita ya msingi ya kuzingatia ili uweze kuwa na blog yenye mafanikio na Kutengeneza pesa kupitia blog yako.

Katika makala iliyopita iliyokuwa na kichwa cha habari kisemacho “Sababu kumi za msingi za wewe kuwa na blog yako mwenyewe ambayo itakuingizia kipato“, nilielezea kwa kina maana halisi ya blog na pia nilifafanua sababu za msingi ambazo wewe mpendwa msomaji wangu unapaswa kuwa na blog yako mwenyewe na namna ambavyo itakunufaisha na kuwa chanzo cha kukuingizia kipato.Kama hukuisoma makala hiyo nakushauri uanze kwanza kuisoma makala hiyo halafu ndio uendelee na makala hii.

Ili uweze kuanzisha blog na kutengeneza pesa kupitia blog yako, unapaswa kuzingatia na kufanyia kazi mambo yafuatayo :

Kutengeneza pesa kupitia blog: Mambo 6 ya kuzingatia.

1.Andika makala nyingi iwezekanavyo.

Ili uweze kufanikiwa kutengeneza pesa kupitia blog yako, unapaswa kuandika makala nyingi iwezekanavyo. Jiwekee ratiba na uifuate ya kuandika makala kila siku au kila baada ya siku mbili. Jambo la msingi ni kuwa, blog yako isikae muda mrefu bila kuweka makala mpya.

2. Penda Kusoma Sana

Ili uweze kuwa na vitu vingi vya kuandika kwenye blog yako, unapaswa kusoma sana kuhusiana na mada unazoandikia blog yako.

3. Wapende na kuwathamini wasomaji wako.

Jambo jingine la kuzingatia ili uweze kutengeneza pesa kupitia blog, jitahidi kusoma na kujibu maoni na maswali ya wasomaji wako mara tu yanapotokea. Kwa kufanya hivyo wasomaji wako watakupenda na kukuheshimu.

4. Usiogope kuandika.

Ili uweze kufanikiwa kutengeneza pesa kupitia blog, unapaswa kutokuogopa kuandika maarifa uliyonayo kuhusiana Mada unazoandikia blog yako. Usiwaze watu watakufikiriaje. Kumbuka kuwa maarifa au ujuzi ulionao ni wa thamani sana kwa mtu fulani na kwamba akiupata utamsaidia na atakushukuru.

5. Penda kujifunza vitu vipya kila siku kuhusiana na ujuzi wako.

Jambo jingine la kuzingatia ili uweze kutengeneza pesa kupitia blog ni kutambua kuwa wewe huwezi kuwa unajua vitu vyote, hivyo unapaswa kujifunza vitu vipya kila siku ili uweze kuandika makala bora na zenye kugusa jamii.

6. Kuwa na subira.

Mafanikio katika blog hayapatikani kwa siku moja. Hivyo endelea kuandika makala nyingi iwezekanavyo zinazoelimisha jamii,watu watakupenda,watakuheshimu na kukuthamini na matokeo yake utayaona baadaye.

Kwa leo niishie hapo. Kama una maoni au swali lolote kuhusiana na makala hii ya jinsi ya kutengeneza pesa kupitia blog, usisite kuandika hapo chini. Au unaweza kuwasiliana nami moja kwa moja kupitia namba yangu ya whatsap 0752081669.

Asante na karibu katika makala ijayo.

Hatua 6 Za Kuanzisha Blog.

Hatua 6 Za Kuanzisha Blog.

Karibu mpendwa katika makala hii. Katika makala hii nitazungumzia hatua 6 za kufuata ili uweze kuanzisha na kumiliki blog itakayokuletea pesa mtandaoni.Hivi unajua kuwa kwa kuanzisha blog unaweza kutumia elimu au ujuzi ulionao kujiingizia kipato mtandaoni bila kuathiri shughuli zako zingine?

Katika makala zilizopita nilielezea maana ya blog na sababu za msingi za wewe kuwa na blog yako mwenyewe. Kama hujapitia makala hiyo unaweza kuipitia halafu ndio uendelee na makala hii. Katika makala hii nitakuelezea hatua sita muhimu za kufuata ili uweze kuanzisha na kumiliki blog itakayokuletea kipato mtandaoni.

1. Chagua Mada (niche) utakayokuwa ukiandikia makala zako.

Hatua ya kwanza kabisa unapotaka kuanzisha blog ni kuchagua mada (niche). Blog nyingi huwa zinaelezea Mada moja. Kwa mfano, kuna blog zinazoandika michezo, habari, afya, elimu na mada zingine nyingi. Hivyo kama wewe una ujuzi wowote, chagua mada ya kuandika kwenye blog yako. Usichanganye mada nyingi kwenye blog yako.

2. Chagua Sauti yako ya kiuandishi (choosing your own voice)

Kitu kizuri sana ninachokipenda kwenye blog ni kuwa, kila mwandishi ana mfumo wake. Hivyo unaweza kuchagua mfumo wowote wa kiuandishi katika blog yako. Kwa mfano : unaweza kuwa unaandika makala katika mfumo wa kitaalamu au unaweza ukawa unaandika makala za kawaida.

3. Chagua vitu vya kuandika kwenye blog yako.

Baada ya kuchagua Mada ya kuandika kwenye blog yako, hatua inayofuata ya kuanzisha blog ni kuchagua mambo ambayo utaandika na yale ambayo hutaandika.

4. Andika makala nzuri na zenye mvuto.

Ili uweze kuwa na wasomaji endelevu kwenye blog yako, unapaswa kuandika makala zenye mvuto na zinazotatua matatizo ya jamii.

5. Tambua aina za makala utakazoandika.

Hatua nyingine ya kuanzisha blog ni kuchagua mtindo wa makala zako. Kuna aina nyingi za mitindo ya uandishi wa makala baadhi yake ni hii ifuatayo :

Mtindo wa kuorodhesha (List) .

Kwa mfano :Mambo sita ya kufanya ili uweze kufanikiwa katika maisha.

Mtindo wa kuandika dondoo (Tips)

Kwa mfano :Ukitaka kufauru mtihani, zingatia mambo yafuatayo.

Mtindo wa kuelezea (review) huduma au bidhaa .

Mfano :Maelezo kuhusu simu ya IPhone 6.

Mtindo wa kupendekezea (recommendation) bidhaa au huduma.

Mfano :Ukitaka kupiga picha zenye ubora camera ya cannon itakufaa.

Mtindo wa ‘jinsi ya ‘(how to)

Mfano :Jinsi ya kuanzisha blog.

Mtindo wa mahojiano (interview)

Mfano :Kutana na Bilionea Maganga aliyeanza biashara yake kwa kuuza ubuyu.

Mtindo wa kutumia video

Mtindo wa kurekodi sauti (podcast)

Mtindo wa kualika wataalam wa mambo mbalimbali (guest post) kuandika makala kwenye blog yako.

6. Weka ratiba nzuri ya kuweka makala zako.

Weka ratiba nzuri ya kuweka makala zako. Ninakupendekezea uwe unaweka makala kila siku, kila baada ya siku mbili, mara mbili kwa juma n.k. Jambo la msingi la kuzingatia hapa ni kuwa na ratiba maalumu ya kuweka makala zako ili uweze kuwa na wasomaji wengi watakaofuatilia blog yako.

Nimatumaini yangu kuwa umejifunza kitu katika makala hii ya hatua za kuanzisha blog. Kwa maoni au swali au ushauri, usisite kuwasiliana nami kwa whatsap 0752081669. Au unaweza kuweka maoni yako hapa chini.

Karibu katika makala ijayo

Jinsi Ya Kuongeza Wasomaji Kwenye Blog Yako.

Jinsi Ya Kuongeza Wasomaji Kwenye Blog Yako.

Mpendwa, nikukaribishe tena katika makala hii. Katika makala ya leo nitazungumzia jinsi unavyoweza kuongeza wasomaji kwenye blog yako. Njia nitakazoeleza hapa zitakusaidia kuongeza maradufu wasomaji wa blog yako na hivyo kupata mafanikio kwenye blog yako.

Soma:Kuanzisha blog: Sababu 10 za kuanzisha Blog yako.

Jinsi ya kuongeza wasomaji kwenye blog yako.

1. Andika makala mara kwa mara kwenye blog yako.

Weka makala mpya mara kwa mara kwenye blog yako. Unaweza kuandika makala, ukaposti picha au ukaweka makala za sauti (Podcasting).

Weka ratiba maalumu kwa ajili ya kuweka makala mpya kwenye blog yako.Ratiba husaidia kuwafanya wasomaji wako wajue ni wakati gani wategemee makala mpya.

2. Wasikilize wasomaji wako na ujibu maoni au maswali yao.

Miongoni mwa vitu vizuri sana ambavyo unaweza kuvifanya kwa wasomaji wako ni kuhakikisha kuwa kila msomaji wako anafurahia kuwa kwenye blog yako. Weka kwenye blog yako ukurasa wa mawasiliano ili kama kuna swali uweze kulijibu haraka iwezekanavyo. Kama kuna maoni yoyote kwenye makala zako, jitahidi kuyajibu haraka. Kwa kufanya hivyo, utaweza kuongeza wasomaji kwenye blog yako.

3. Tembelea Blog zingine na majukwaa mbalimbali na uchangie mada zinazotolewa.

Ili uweze kuwa na wasomaji wengi kwenye blog yako, unatakiwa kushiriki kwenye blog za watu wengine kwa kuchangia maoni yako. Tafuta blog zinazoandika makala kama zako na uwe unatoa maoni yako. Unapokuwa unatoa maoni usisahau kutaja blog yako. Kwa kufanya hivyo utafanya blog yako kutambulika na hivyo kupata wasomaji wengi.

4. Alika miongoni mwa wasomaji wako kuandika makala.

Pia, ili uweze kuongeza wasomaji, unaweza kualika miongoni mwa wasomaji wako kuandika makala. Hii itasaidia kuifanya blog yako kuwa na makala zenye ladha tofauti.

5. Wasiliana na wasomaji wako kwa njia ya email.

Waalike wasomaji kujisajiri (subscribe) ili waweze kupata taarifa kila unapoweka makala mpya. Kuna namna nyingi ya kufanya wasomaji wajisajiri ili kupata taarifa kila unapoweka makala. Mojawapo ya njia hizo ni kuweka kifaa cha kukusanyia taarifa za wasomaji wako kama vile jina na baruapepe (email). Hivyo msomaji anapokuwa amependezwa na makala zako atajisajiri ili aweze kupata taarifa kila unapoweka makala mpya. Mfano wa kifaa hicho ni MailChimp

6. Unganisha blog yako na mitandao ya kijamii.

Miongoni mwa njia bora kabisa za kuongeza wasomaji wa blog yako ni kuiunganisha na mitandao ya kijamii kama vile facebook, twitter, Pinterest na LinkedIn .Mitandao hii ina watu mamilioni. Hivyo unapokuwa na kurasa kwenye mitandao hii na ukawa unashea makala zako, utapata wasomaji wengi.

7. Shirikisha wasomaji wako kutoa maoni yao kwa kuwauliza maswali.

Shirikisha wasomaji wako kwa kuwauliza maswali mbalimbali kuhusiana na makala unazotoa ili watoe maoni yao. Unaweza kukusanya maoni ya wasomaji kwa kuweka kifaa kinachoitwa Survey Monkey kwenye blog yako.

8. Zingatia blog yako kuonekana vizuri kwenye simujanja (smartphone).

Hakikisha kuwa blog yako inaonekana vizuri kwenye smartphone ili uweze kupata wasomaji wengi kwani kwa sasa watu wengi wanatumia simu za mkononi.

9. Andika mada tofauti tofauti kwenye blog yako.

Ili uweze kuongeza wasomaji wengi, unaweza kuchanganya mada tofauti tofauti kwenye blog yako. Lakini zingatia mada hizo ziwe zinaendana na malengo ya blog yako. Kwa mfano blog yako inahusu biashara, unaweza kuandika makala ya namna ya kuanzisha biashara, lakini pia unaweza kuchanganya makala kama vile namna ya kutangaza biashara kwenye mitandao ya kijamii n.k

Nimatumaini yangu kuwa umepata maarifa ambayo yatakusaidia kuboresha blog yako. Kwa maoni au ushauri usisite kuweka maoni yako hapa chini. Lakini pia unaweza kuwasiliana nami moja kwa moja kwa njia ya whatsap 0752081669.

Asante na karibu katika makala ijayo.

Jinsi Ya Kukuza Blog Yako: Mambo 10 Ya Kuzingatia.

Jinsi Ya Kukuza Blog Yako: Mambo 10 Ya Kuzingatia.

Mpendwa, karibu sana katika makala hii. Katika makala hii nitaelezea Jinsi ya kukuza blog yako. Nitazungumzia mambo kumi ya msingi unayotakiwa kuyafanya ili uweze kuwa na blog bora ambayo itakuwa ni chanzo cha kukuletea pesa (kipato) .

Jinsi ya kukuza blog yako: Mambo kumi ya kuzingatia.

1. Tambua sauti yako.

Blog yako inakuwakilisha wewe mtandaoni. Hivyo, kila unachoandika kinawakilisha mawazo yako na hivyo kukutofautisha wewe na watu wengine. Hivyo unatakiwa kuchagua mtindo wa uandishi wa makala zako. Unapokuwa unafikiria mtindo wako wa uandishi, jiulize mwenyewe maswali yafuatayo :

unataka wasomaji wa makala zako wawe ni watu wa aina gani?

Unahitaji kuwa na blog ya kufundisha ujuzi gani?

2. Weka blog yako kuwa ni miongoni mwa majukumu yako ya kila siku.

Maisha yanabadilika. Unaweza kupata kazi mpya au kubadilishiwa majukumu, unaweza kupata watoto na hivyo majukumu yako kuongezeka. Ili uweze kukuza blog yako, hakikisha kuwa, hata kama utakuwa na majukumu mengi, weka pia blog kuwa miongoni mwa majukumu yako ya msingi. Kwa kufanya hivyo utaifanya blog yako kuwa ni sehemu ya kazi kama kazi zingine na hivyo blog yako itakuwa bora na yenye watembeleaji .

3. Uliza wasomaji wako kutoa maoni kuhusiana na makala zako.

Kila mwisho wa makala zako, wahamasishe wasomaji wako kutoa maoni kuhusiana na mada uliyoandika. Hii itakusaidia kujenga mahusiano mazuri na wasomaji wako na pia kujua mahitaji yao. Kila maoni au maswali yanapotolewa, hakikisha unayajibu kwa wakati.

 4. Tambua blog zingine zinazoandika makala zinazofanana na zako

Angalia blog zilizofanikiwa zinazoandika makala kama za kwako na ujifunze kutoka kwao, pia jiunge na majukwaa mbalimbali yanayojadili mada unazotoa. Hii itakuongezea ujuzi katika mada unazoandika.

5. Chunguza Takwimu na vyanzo vya watembeleaji wa blog yako.

Kuna faida nyingi za kujua vyanzo vya watembeleaji wa blog yako. Utajua watembeleaji wako wengi wanatoka sehemu gani, makala zipi zilizotembelewa zaidi na mambo mengine. Hii itakusaidia kujua ni mada zipi zinazopendwa zaidi na hivyo kukusaidia kujua ni mada zipi uendelee kuziandikia katika makala zako zijazo.

6. Weka malengo ya blog yako

Ili uweze kukuza blog yako, unatakiwa kuweka malengo ya blog yako yanayopimika ili uweze kujua kama blog yako inakua au la. Weka malengo mepesi kupimika kama vile

Kuongeza wasomaji: Kwa mfano : Ninahitaji kupata wasomaji wapya 50 kila mwezi kwenye blog yangu.

Ratiba ya kuweka makala kwenye blog: Kwa mfano : Nitakuwa nikiweka makala mpya moja kila siku kwenye blog yangu.

Kufungua na kutumia mitandao ya kijamii: Kwa mfano : Nitafungua kurasa kwenye facebook, twitter, na instagram. Pia nitakuwa nikishea makala mpya za blog yangu kwenye mitandao hiyo ya kijamii.

Kujipatia kipato: kujipatia kipato kwenye blog yako ni lengo la muhimu ambalo unatakiwa kuliweka. Kwa mfano : Baada ya mwaka mmoja blog yangu ianze kuniingizia kipato cha shilingi million moja kila mwezi kutokana na matangazo pamoja na kuuza bidhaa mbalimbali pamoja na huduma.

7. Weka viashiria vya mafanikio ya malengo yako.

Weka viashiria vya mafanikio ya malengo ya blog yako ili uweze kujua wapi umefikia. Kwa mfano : Uliweka malengo ya kuongeza wasomaji wapya 50 kila mwezi. Pima mafanikio kwa kuangalia takwimu za watembeleaji wa blog yako.

8.Weka malengo ya namna ambavyo blog yako itakuingizia kipato.

Kila mmiliki wa blog ni hitaji lake kuona blog yake ikimuingizia kipato cha kujikimu kimaisha. Hivyo ili uweze kukuza blog yako, unapaswa kuweka malengo ya namna gani blog yako itakuingizia kipato.Kwa mfano :

Je una malengo ya kutumia mfumo wa matangazo (ads) kukuingizia kipato? Je ni aina gani ya matangazo utaweka?

Je una mpango wa kuingia ubia na watu binafsi au makampuni kuweka matangazo yao?

Je una mpango wa kuuza bidhaa zako wewe mwenyewe kwenye blog yako kama vile vitabu au kozi mbalimbali kutokana na ujuzi wako?

Je una mpango wa kutumia blog kama jukwaa la kujitangaza kuwa wewe ni mtaalam katika jambo fulani ili watu wakutambue na kukupatia tenda za kazi mbalimbali ili uweze kuwafanyia na kujipatia kipato?

9.Anza kidogo na jipe muda kukuza blog yako.

Unaweza kuanza blog yako bila gharama yoyote kwa kutumia blogger halafu kadiri blog yako inavyozidi kukua unaweza kuihamishia kwenye mifumo mingine ya hali ya juu zaidi kama vile wordpress.

10.Kila unapopiga hatua moja, fanya tathmini.

Kwa sababu kazi ya blog ni endelevu, hivyo, ili uweze kukuza blog yako, jenga utamaduni wa kutathimini kila hatua unayopiga kufanikisha malengo uliyojiwekea kisha boresha zaidi.

Kwa leo niishie hapo. Kama una swali lolote au maoni kuhusiana na makala hii, usisite kuandika hapa chini. Pia unaweza kuwasiliana nami moja kwa moja kwa njia ya whatsap 0752081669.

Asante sana na karibu katika makala ijayo.

Sababu 10 Za Kuanzisha Blog Yako.

Sababu 10 Za Kuanzisha Blog Yako.

Kama unafikiria kuanzisha blog lakini huna uhakika kama uko sahihi na uamuzi wako, usiwe na wasiwasi kwani makala hii inakwenda kukupatia majibu yote ambayo yamekuwa yakikutatiza. Katika makala hii nitakushirikisha sababu 10 za kuanzisha blog. Basi karibu tuendelee .

Je Ninapaswa Kuanzisha Blog? Sababu 9 kwa nini unapaswa kuanzisha na kuwa na Blog yako mwenyewe. (na maswali 7 ya msingi unayopaswa kujiuliza kabla ya kuanzisha Blog)

  1. Sababu 6 za msingi za wewe kuanzisha na kuwa na blog yako mwenyewe.
  2. Sababu 3 ambazo sio za msingi za wewe kuanzisha blog (Kama una sababu hizi usianzishe blog)
  3. Maswali 7 ya muhimu unayopaswa kujiuliza kabla ya kuamua kuanzisha blog.
  4. Sasa fanya maamuzi.

Katika Makala hii tunaenda kuangalia maswali muhimu na ya msingi unayopaswa kujiuliza kabla ya kuanzisha blog. Lakini kabla hatujaendelea na maswali hayo, hebu kwanza tuangalie sababu za msingi za wewe kuwa na blog yako mwnyewe.

Tutaangalia sababu 6 za msingi za wewe kuwa na blog yako mwenyewe. Lakini pia tutaangalia sababu 4 ambazo sio za msingi.

 Sasa hebu tuendelee.

1. Sababu 6 za msingi za wewe kuanzisha na kuwa na blog yako mwenyewe.

Kama una miongoni mwa sababu hizi au nzuri zaidi ya hizi za wewe kuanzisha blog , basi ukianzisha blog utafanikiwa sana.

Sababu ya msingi #1: Unahitaji kuandika na kufundisha watu kuhusiana na mada unayoipenda.

Kama una ujuzi ,au mada unayoipenda na unahitaji kuwashirikisha watu ujuzi wako, ukiamua kuanzisha blog na kufundisha watu ujuzi wako unaoupenda, utafanikiwa sana kwenye kazi yako ya blog.

Sababu ya Msingi #2: Unahitaji kuanzisha na kujenga Biashara kupitia mtandao wa internet.

Inawezekana unahitaji kuanzisha blog ukiwa na sababu ya kuanzisha biashara yako na kuitangaza kuipitia mtandao wa internet. Au inawezekana tayari una biashara na kupitia kuanzisha blog,unahitaji kutangaza biashara yako ili iweze kuwafikia watu wengi zaidi.

Pia kupitia blog unaweza kujiajiri na kutengeneza kipato.Kwa mfano,unaweza kuuza maarifa yako mtandaoni kwa kuuza kozi mbalimbali, vitabu pepe (ebooks) au kuuza ushauri wako wa kitaalamu kwa watu.

Sababu ya msingi #3: Unahitaji kutengeneza Brand yako.

Blog ni njia nzuri sana ya kukuza jina lako na kulifanya litambulike na kuwa maarufu kwa watu. Hivyo, kama unataka watu na jamii kwa ujumla wakutambue, anzisha blog na uwasaidie watu kutatua matatizo yao kupitia kuandika makala kwenye blog yako.

Sababu ya Msingi #4: Unahitaji kutatua changamoto zinazoikabili jamii na kufanya maisha ya watu yabadilike.

Kama utaanzisha blog ili kutatua matatizo ya watu utafanikiwa sana kwani watu wana changamoto nyingi zinazowakabili na wanahitaji mtu atakayeweza kutatua changamoto zao.Hivyo kama unahitaji kuanzisha blog ili kuweza kubadilisha maisha ya watu,nakutia moyo songa mbele kwani utafanikiwa sana katika kazi yako.

Sababu ya msingi #5: Unahitaji kujiajiri na kujipatia kipato kupitia maarifa,ujuzi au hobby yako.

Pia sababu nyingine unaweza kuanzisha blog ili kujiajiri na kutumia ujuzi ulionao kufundisha watu na kujipatia kipato mtandaoni.

Soma:Njia 9 za kutengeneza kipato kupitia blog.

Sababu ya Msingi#6: Unafurahia Kujifunza Vitu Vipya Kila Siku.

Unapoanzisha blog umeanza safari ndefu ya uandishi. Hivyo utatakiwa ujifunze vitu vipya kila siku ili uweze kubobea kwenye mada unayofundisha.

2. Sababu 3 ambazo sio za msingi za wewe kuanzisha blog(Kama una sababu hizi usianzishe blog)

Pamoja na kuwa sababu nilizozielezea hapo juu ni za msingi za wewe kuanzisha na kuwa na blog yako mwenyewe, Sababu zifuatazo sio za msingi. Hivyo, kama una sababu hizi ninazoenda kuzielezea sasa au zinazofanana na hizi, usianzishe blog kwani itakuwa vigumu sana kwako kufanikiwa.

Sababu isiyokuwa ya msingi #1: Unahitaji kutengeneza Pesa Haraka.

Kama unahitaji kuwa n blog kwa lengo la kutengeneza pesa haraka ,basi unaweza kushindwa kufikia malengo yako. Hii ni kwa sababu ili uweze kutengeneza pesa kupitia blog unapaswa kujipa muda kuijenga blog yako kwa kuweka makala mara kwa mara ili ujenge mahusiano na wasomaji wako. Hivyo, kama utaweka nguvu katika kuandika makala za kuelimisha jamii, watu watakupenda na hivyo watakuwa tayari utakapoamua kuwauzia bidhaa au huduma unayotoa.

Sababu isiyokuwa ya msingi #2: Huna kitu cha kuelimisha bali unahitaji kuwa unaweka mambo maisha yako binafsi mtandaoni.

Kama unahitaji kutengeneza kipato kupitia blog kuandika maisha yako binafsi haitakusaidia kukuza blog yako. Kumbuka kuwa watu huwa wanaingia mtandaoni kujifunza maarifa ambayo yatatatua changamoto zao.Hivyo ukianzisha blog ili kuweka mambo yako binafsi hutaweza kukuza blog yako.

Hata hivyo, unaweza kuanzisha blog kutokana na hobby yako ambayo unahisi itakuwa msaada kwa watu kutatua changamoto zao.

Sababu isiyokuwa ya msingi  #3: Huwa unasoma blog nyingi na unaona ni fahari na wewe kumiliki blog.

Inawezekana ukaona kuwa kwa kuwa unapenda kusoma Makala kwenye blog mbalimbali na wewe ukafikiria kuwa na blog yako mwenyewe. Japokuwa sababu hii sio mbaya ,lakini sio sababu ya kutosha kwa wewe kuanzisha blog. Wazo hili ni sawa na la mtu anayependa kuangalia movie halafu akatamani na yeye awe muigizaji. Kuanzisha blog kunahitaji kujitoa kiasi cha kutosha kusoma na kuandika Makala mara kwa mara kama unataka kufanikiwa kwenye kazi hii. Hivyo kusema tu kuwa kwa kuwa unapenda kusoma blog mbalimbali na wewe unahitaji kuwa na blog yako mwenyewe haitoshi kukufanya na wewe uanzishe blog. Kama unataka kuanzisha blog  unapaswa kutafakari Zaidi na uwe na sababu za msingi kama nilizoziainisha hapo kabla.

Hatari nyingine ya kuanzisha blog kwa sababu tu unapenda kusoma blog zingine ni kuwa , kwa kuwa utakuwa huna maandalizi na sababu za msingi za wewe kuwa na blog utaishia kunakiri (copy and paste) blog zile unazopenda kuzisoma.

Maswali 7 ya msingi unayopaswa kujiuliza kabla ya kuanzisha Blog.

Sasa tayari umefikiria kwa kina na umeona kuwa una sababu za msingi za kuanzisha blog. Je uendelee mbele au unaenda kupoteza muda wako bure?

Hapa nimekuwekea Maswali 8 ya msingi unayopaswa kujiuliza kabla ya kuanzisha Blog.

Swali #1: Je umechagua mada unayoipenda?

Unapokuwa umechagua mada unayoipenda, hiyo ni hatua ya kwanza kuelekea mafanikio. Hii ni kwa sababu unapoanzisha blog, utaendelea kuweka Makala kwa miaka mingi ijayo. Hivyo ukiwa umechagua mada unayoipenda , utakuwa unafurahia kuandika mara kwa mara na kusoma zaidi kujiongezea ujuzi kwenye mada yako.

Swali #2: Je una ujuzi wa kutumia computer na mtandao wa internet?

Hapa sizungumzii kuwa uwe umesoma sana kuhusiana na mambo ya computer,ninachosema ni ule uelewa tu wa msingi wa jinsi ya kutumia internet.

Swali #3: Je utakuwa na muda na nguvu ya kutosha kuandika Makala?

Jambo jingine la msingi unalopaswa kujiuliza ni kuwa ,utakuwa na muda na nguvu kuendesha blog yako? Kumbuka kuwa ili uwe na blog yenye mafanikio, unapaswa uwe unaweka Makala mara kwa mara. Hivyo unapaswa ujiulize na uwe mkweli kwenye nafsi yako kama utaweza kuwa na muda wa kuandika Makala za blog yako.

Swali  #4: Jinsi gani utatengeneza kipato (pesa) kupitia blog yako?

Jambo jingine la msingi unalopaswa kulifikiria ni kuwa , ni jinsi gani utatengeneza kipato kupitia blog yako.Je utakuwa ukiuza kozi mbalimbali ulizoandaa,vitabu pepe au utakuwa ukitoa huduma ya ushauri na watu wakakulipa? Au utatumia blog yako kuuza bidhaa zako mwenyewe au kutangaza bidhaa za makampuni mengine na wewe ukapata gawio (commission)? Kimsingi kuna njia nyingi sana ambazo unaweza kuzitumia kwenye blog yako kupata kipato. Hivyo unapaswa kufikiria jinsi ambavyo blog yako itakuingizia kipato toka siku ya kwanza unapoianzisha.

Swali#5: Utakuwa ukiandaa Makala za aina gani?

Kwa kuwa Makala ndio msingi wa blog, hivyo unapaswa kufikiria Makala zako zitakuwa za aina gani. Je ni kurekodi video au kuandika Makala? Na Je utakuwa ukiandika Makala zenye urefu gani?

Hivyo, unapaswa kujiuliza jambo hili mapema kabla ya kuanzisha blog yako.

Swali #6: Utapimaje maendeleo ya blog yako?

Kuna njia nyingi za kupima maendeleo ya blog yako.

Kama lengo lako si kutengeneza pesa bali ni kuelimisha jamii, unaweza kupima maendeleo ya blog yako kwa kuangalia ongezeko la idadi ya watembeleaji kwenye blog yako na ongezeko la email za watu waliojiunga na blog yako.

Kama lengo lako ni kujiajiri na kutengeneza kipato kupitia blog utapima maendeleo ya blog yako kwa kuangalia ni kiasi gani cha pesa unatakiwa uwe umepata kupitia blog kwa kipindi ulichojiwekea. Inaweza kuwa mwezi au mwaka.

Swali #7: Utakuwa ukiweka Makala mpya kila baada ya muda gani?

Kabla ya kuanzisha blog unatakiwa pia kujua ratiba yako ambayo utaitumia kuweka Makala kwenye blog yako. Inaweza kuwa mara moja kila siku au mara moja kwa juma n.k . Hii itawafanya wasomaji wako kujua wakati maalumu ambao wakiingia kwenye blog yako watapata maarifa mapya.

Sasa ni wakati wako wa kuamua,Je unahitaji kuanzisha blog?

Katika Makala hii nimejitahidi kuelezea faida za kuanzisha blog na kumiliki blog yako mwenyewe. Pia nimezungumzia maswali ya msingi unayopaswa kujiuliza kabla hujaingia kwenye kazi hii.

Kumbuka kuwa , kama unaweza kupata masaa machache tu kwa juma na ukawa na mada unayopenda kufundisha, hakuna kitakachokuzuia wewe kuanzisha na kujipatia kipato kupitia blog. Songa mbele!

Nimatumaini yangu kuwa umepata maarifa ya kukusaidia kuanzisha blog .Kama una maoni yoyote, usisite kudondosha maoni yako hapa chini! Pia unaweza kuwasiliana nami moja kwa moja kama unahitaji ushauri, kuhusiana na jinsi ya kujiajiri na kutengeneza pesa mtandaoni kwa simu namba 0752081669.

Asante na karibu katika makala ijayo.

Njia 9 Za Kutengeneza Kipato Kupitia Blog.

Njia 9 Za Kutengeneza Kipato Kupitia Blog.

Kama unasoma Makala hii kwa sababu unahitaji kujua jinsi ya kutengeneza pesa(kipato) kupitia Blog, basi nikuhakikishie kuwa upo mahali sahihi.

Soma: Njia 10 za kutengeneza pesa mtandaoni bila kuathiri muda wako wa kazi

 Katika Makala hii nimekuandikia njia 9 ambazo unaweza kuzitumia kujipatia kipato kupitia blog yako.

Jinsi ya kutengeneza pesa (kipato) kupitia Blog:Njia 9 unazoweza kuzitumia.

  1. Makala za kulipia(sponsored Blog Content)
  2. Kutangaza na kuuza Bidhaa za makampuni kwa lengo la kupata gawio(commisions)(Affiliate Programs)
  3. Kuweka matangazo ya Biashara kwenye Blog(Blog Advertisements)
  4. Kuuza kozi mbalimbali mtandaoni
  5. Kuuza bidhaa mbalimbali(Physical Products)
  6. Kuuza software mtandaoni
  7. Kuuza huduma zako mtandaoni
  8. Kuandika na kuuza Vitabu pepe (ebooks)
  9. Kuwa mshirika wa kibiashara na Makampuni mbalimbali.

Kama wewe ni mgeni kabisa kuhusiana na Blog, kabla ya kuendelea na Makala hii, unaweza kupitia Makala ya Jinsi ya kuanzisha Blog na kutengeneza pesa mtandaoni: Mwongozo rahisi wa jinsi ya kuanzisha Blog.

Kimsingi ,kuwa na blog yako mtandaoni ambayo tayari imekwishaanza kupata watembeleaji ni hatua ya kwanza kuelekea kuanza kujipatia kipato. Japokuwa ni jambo jema kufikiria njia ambazo unaweza kuzitumia kujipatia kipato kwenye blog yako hata kama ndio kwanza umeianzisha,Makala hii inawafaa zaidi wale ambao tayari wana blog zao na wameshaanza kupata watembeleaji na hivyo wanahitaji kuzipeleka blog zao katika hatua nyingine ambayo watakuwa wakijipatia kipato. Hivyo, kama bado hujaanzisha blog, unaweza kupitia Makala yangu ya Jinsi ya kuanzisha Blog na kutengeneza pesa : Mwongozo rahisi wa jinsi ya kuanzisha Blog.

Jenga msingi imara wa Blog yako kabla ya kufikiria namna ya kutengeneza kipato.

Kabla ya kwenda moja kwa moja kwenye njia za kuingiza kipato kupitia blog,hebu tujikumbushe kwa ufupi ni nini kinatakiwa ili uweze kuwa na blog yenye mafanikio.

Ili uweze kuwa na blog yenye mafanikio tuliona kuwa unapaswa kuchagua kwa uangalifu mada (niche),kuandika Makala zenye mvuto na kuitangaza blog yako ili uweze kupata wasomaji wengi. Hivyo baada ya kuwa umefanya mambo hayo yote ndio unaanza kufikiria jinsi ambavyo utajipatia kipato kupitia blog yako.

Sasa hebu tuangalie njia ambazo uanweza kuzitumia kutengeneza kipato kupitia Blog yako.

Jinsi ya kutengeneza pesa (kipato) kupitia Blog:Njia 9 unazoweza kuzitumia.

1. Makala za kulipia (Sponsored Blog Content)

Nini maana ya Makala za kulipia (sponsored content)? Hizi ni Makala ambazo Kampuni au mtu binafsi anakulipa ili uweze kuandika kwenye blog yako Makala ambayo itakuwa inaelezea Bidhaa au biashara ya kampuni yake. Kwa sababu blog yako itakuwa na wasomaji wengi, hivyo makampuni yanaweza kufanya makubaliano na wewe ili uandike Makala zinazotangaza biashara zao.

Hivyo baada ya blog yako kuwa na wasomaji wengi,unaweza kufanya makubaliano na makampuni mbalimbali au watu binafsi kuwatangazia biashara zao kupitia kuandika Makala kwa malipo.

Unapokuwa umepata kampuni au mtu binafsi ambaye ana bidhaa na anataka uandike Makala kuelezea bidhaa yake,hakikisha kuwa unakuwa mkweli kulingana na ubora wa bidhaa hiyo kwa wasomaji wako. Hii ni kwa sababu wasomaji wako watakuwa wanakuamini na hivyo chochote unachokiandika kwenye blog yako hakikisha kuwa kina ukweli ili kuendelea kujenga Imani ya wasomaji wako. Jambo la msingi ni kuwa hakikisha bidhaa au biashara ambayo utaamua kutangaza inaendana na mada za blog yako.

2. Kutangaza na kuuza Bidhaa za makampuni kwa lengo la kupata gawio(Affiliate Programs)

Hii ni njia nyingine ya kutengeneza kipato kupitia blog yako. Katika njia hii ya affiliate Program unajiunga na makampuni yanayouza bidhaa kwa lengo la kutangaza bidhaa zao.Baada ya kujiunga utapewa matangazo yenye link ambayo utayaweka kwenye blog yako.Kila mtu anayebofya link hiyo atapelekwa kwenye tovuti ya kampuni linalouza bidhaa hiyo. Kila mtu anayenunua bidhaa kupitia link yako wewe unalipwa kamisheni kutokana na mauzo ya bidhaa hiyo.Miongoni mwa makampuni yanayotoa huduma hii ni Amazon,Aliexpress na mengine mengi yaliyoko nje ya nchi. Kwa Tanzania kuna Dudumizi n.k

3.Kuweka matangazo ya Biashara kwenye Blog(Blog Advertisements)

Kuweka matangazo kwenye blog ni njia rahisi ambayo unaweza kuitumia kujitengenezea kipato.Hata hivyo njia hii kwa kuwa ni rahisi kipato utakachoingiza ni kidogo sana kama blog yako ina watembeleaji wachache. Miongoni mwa platform ambazo unaweza kujiunga na kuweka matangazo yao ni hizi zifuatazo:PropellerAds ,Google AdSense na mengine mengi. 

4. Kuuza kozi mbalimbali mtandaoni.

Je una ujuzi au maarifa yoyote ambayo unaweza kufundisha watu wengine? Je wasomaji wako wanakuona kuwa wewe ni mtaalam katika ujuzi fulani?

Tengeneza kipato kupitia ujuzi wako kwa kuandaa kozi na kuiuza mtandaoni (creating an online course ) na hapo utakuwa umetengeneza mfereji wa kukuingizia kipato kwa muda mrefu .

Kuandaa na kuuza kozi mtandaoni ni njia rahisi kwani unaweza kurekodi video fupifupi zinazofundisha ujuzi ulionao kulingana na mada unayofundisha kwenye blog yako na ukazipangilia vizuri na kutengeneza kozi ambayo utaiuza mtandaoni kupitia blog yako.Kumbuka kuwa, kama una ujuzi fulani,watu wanahitaji ujuzi wako uweze kuwasaidia katika maisha yao na hivyo wako tayari kununua ujuzi huo. Kazi kwako!

Ushauri wangu unapokuwa unahitaji kutengeneza kipato kupitia kuandaa kozi mtandaoni, ni kwa kuanza kuandaa kozi fupifupi.

Jinsi gani unaweza kuandaa kozi yako ya kwanza mtandaoni?

Jambo la kwanza kabisa,utatakiwa kujua ni ujuzi au maarifa gani unayotaka kufundisha( na itachukua muda gani kwa mtu kujifunza ujuzi huo).

Baada ya hapo,fanya utafiti upate kujua kama ujuzi au maarifa hayo unayotaka kufundisha watu wanayahitaji.

Baada ya hapo,gawanya ujuzi unaotaka kuuandalia kozi katika masomo mbalimbali. Kwa mfano, una blog inayofundisha ujasiriamali na unahitaji kuaandaa kozi ya Jinsi ya kuanzisha Biashara. Hapa utatakiwa kugawa maarifa haya katika video fupifupi zizoelezea somo mojamoja kwa mfano:

  • Nini maana ya Biashara
  • Jinsi ya kupata wazo la Biashara
  • Jinsi ya kuandika mchanganuo wa Biashara
  • Hatua za kufuata ili kuanzisha Biashara
  •  Jinsi ya Kusajiri Jina la Biashara BLERA n.k

Video hizi utazipangilia kwa lengo la kufikisha ujuzi uliokamilika kwa msomaji wako na hivyo kumuwezesha kutatua changamoto aliyonayo na hivyo kubadili maisha yake.

Kwa kweli fursa ni nyingi sana kutengeneza kipato kupitia kuandaa kozi kwenye blog yako.Jambo la kuzingatia ni kuwa,hakikisha kozi unazoandaa ziendane na mada(niche) unayofundisha kwenye Blog yako.

Ifanye kozi yako ya kwanza kuwa rahisi na utaendelea kuboresha zaidi unavyoendelea kupata uzoefu unapoendelea kuandaa kozi zinazofuata.

5.Kuuza bidhaa mbalimbali(Physical Products)

Pia njia nyingine ambayo unaweza kuitumia kuingiza kipato ni kuuza Bidhaa zako mwenyewe. Unaweza kufungua duka la mtandaoni kwenye ukurasa mmojawapo wa blog yako na ukauza na watu wakanunua moja kwa moja kwenye blog yako.

Unaweza kutafuta supplier kutoka kwenye soko la mtandaoni la Alibaba na ukaagiza bidhaa kwa lebo yako na ukauzia watu kwenye blog yako.

6.Kuuza software mtandaoni.

Je wewe ni mtaalamu wa computer (developer)? Au kama sio wewe je una rafiki yako ambaye ana ujuzi huo? Kama una ujuzi huo,unaweza ukaanzisha blog inayohusiana na ujuzi ulio nao na kisha ukaandaa software ambayo utaiuza kupitia blog yako kwa wasomaji wako. Hii ni njia nzuri sana ambayo itakuletea kipato kikubwa na endelevu.

7.Kuuza huduma zako mtandaoni

Kuuza ujuzi ulionao kama huduma inakaribia kufanana na kuuza kozi mtandaoni.Tofauti inakuja kuwa unapouza ujuzi wako mtandaoni unakuwa ukitoa huduma kwa mtu mmoja mmoja au vikundi vya watu kwa kuongea nao na kutoa ushauri au huduma yako.Hivyo wanakulipa kwa kutoa huduma yako.

8.Kuandika na kuuza Vitabu pepe (ebooks)

 Kuandika na kuuza vitabu pepe(ebooks)  ni njia nzuri sana ya kutengeneza kipato kupitia blog yako.Uzuri wa hii njia ni kuwa ukiwa tayari umemaliza kuandika kitabu chako na kukiweka mtandaoni,huhitaji gharama zingine za ziada bali kitabu chako kitaendelea kukuletea kipato kwa muda mrefu wa miezi na miaka!

9. Kipato kupitia washirika wa kibiashara(Business Partnerships)

Pale unapokuwa na blog iliyofanikiwa na kuwa na wasomaji wengi,hapo utavutia washirika wengi wa kibiashara kuungana na wewe ili waweze kutangaza biashara zao kupitia blog yako. Hii ni kwa sababu utakuwa una mtaji mkubwa wa watu.Wanaweza kutumia blog yako kuuza bidhaa au kutangaza huduma zao na wewe wakakulipa.

Kama nilivyosema hapo mwanzoni mwa Makala hii,unatakiwa kwanza kukuza blog yako ndio uweze kufikiria jinsi ya kutengeneza kipato.

Je una swali au komenti yoyote? Usisite kudondosha komenti yako hapa chini! Pia kama una hitaji ushauri wowote, usisite kuwasiliana nami kwa simu namba 0752081669. Karibu katika makala ijayo.

Jinsi Ya Kuchagua Mada (Niche) Kwa Ajili Ya Blog Yako.

Jinsi Ya Kuchagua Mada (Niche) Kwa Ajili Ya Blog Yako.

Watu wengi wanapotaka kuanzisha blog, hupata shida waanzishe blog kuhusiana na mada ipi. Kama na wewe ni miongoni mwao,nitakupatia hatua rahisi ambazo ukizitumia utaweza kupata mada bora kwa ajili ya blog yako. Katika makala hii nitazungumzia Jinsi ya kuchagua mada (niche) kwa ajili ya blog yako. hebu tuanze kuangalia hatua hizo.

Soma: Njia 9 za kutengeneza kipato kupitia blog

Jinsi ya kuchagua mada(niche) kwa ajili ya blog yako.

1. Chukua karatasi na Orodhesha vitu vyote unavyovipenda.

Nini unapenda kufanya au kuzungumzia?

Orodhesha vitu vyote unavyovipenda kuvifanya au kuvizungumzia kwenye maongezi yako. Haijalishi ni vikubwa au ni vidogo,we viandike tu.

Inawezekana kwenye orodha yako baadhi ya vitu vikawa kwa mfano:

  • Biashara ndogondogo
  • Soka
  • mazoezi
  • Kuchati facebook na Instagram.
  • Kuogelea
  • Kusoma vitabu n.k

Sasa baada ya kuwa umeorodhesha, unapoangalia orodha yako utashangaa kuona kuwa kuna baadhi ya vitu ulivyoorodhesha vinaweza kuwa mada nzuri kwa ajili ya wewe kuanzishia blog yako. Hivyo weka alama ya nyota kwenye vitu unavyoona kwenye orodha yako vinakupendeza zaidi na vinaweza kuwa ni mada za kuanzishia blog ili uje uvirudie baadaye.

2. Fikiria juu ya Blog,magazeti na vitabu unavyopenda kusoma.

Jinsi Ya Kuchagua Mada (Niche) Kwa Ajili Ya Blog Yako.

Sasa hebu weka pia orodha ya blog,magazeti na vitabu unavyopenda kusoma. Kisha orodhesha mada ambazo huwa unapenda kusoma kwenye vitabu, magazeti au blog hizo. Utashangaa baadhi ya mada ulizoorodhesha zinaweza kuwa ni mada bora za wewe kuanzisha blog yako. Weka alama ya nyota kwenye mada ambazo unaona zinakuvutia ili baadaye uje uzirudie kuziangalia upya.

3. Orodhesha kazi zote ulizowahi kufanya na zile unazoendelea kufanya na uzoefu wako.

Njia nyingine ya kuchagua mada (niche) ni kwa kuangalia ni kazi gani ulizowahi kuzifanya au unaendelea kuzifanya? Ziorodheshe hata kama ni ndogo kiasi gani.Lakini unapendelea vitu gani (hobbies)? Viorodheshe. Inawezekana ukaanzisha blog kuhusiana na ujuzi wako wa kazini au ukachagua kipengele kimoja kati ya majukumu au ujuzi ambao unautumia kazini. Pia unaweza kuanzisha blog kutokana na hobby yako. Hivyo vyote viorodheshe. Baada ya hapo angalia kwenye orodha yako vitu ulivyovipenda zaidi na uviwekee alama ya nyota ili uje kuviangalia zaidi baadae.

4. Orodhesha vitu ulivyowahi kuvikamilisha.

Andika orodha ya vitu ulivyowahi kuvikamilisha katika maisha yako. Kwa mfano;

  • Semina ulizowahi kuhudhuria
  • Kozi ulizowahi kusoma n.k

Vyote hivi vinaweza kuwa ni vyanzo vya wewe kupata mada ambayo utaitumia kwenye blog yako. Orodhesha ujuzi ulioupata na kwenye hiyo orodha ,weka alama ya nyota kwenye ujuzi ulioupenda zaidi ili baadaye uje kuuangalia zaidi.

5. Angalia mada zenye umaarufu ambazo zitaendelea kuwa maarufu kwa miaka mingi ijayo.

Pia kama bado unapata kikwazo, orodhesha mada ambazo kwa kweli zitaendelea kuwa na uhitaji kwa miaka mingi ijayo na uangalie kipengele kitakachokufaa kwenye blog yako. Mfano wa mada hizo ni:

  • Biashara: Hii inajumuisha vipengele kama jinsi ya kuongeza kipato,jinsi ya kuanzisha biashara, jinsi ya kuwekeza,jinsi ya kupunguza matumizi,jinsi ya kuepuka madeni n.k
  • Afya:Hii inachukua eneo kubwa sana.Baadhi ya mada zake ni Jinsi ya kupunguza uzito,Afya ya akili,tiba mbadala n.k
  • Malezi: Hii inajumuisha malezi ya watoto.
  • Ujasiriamali: Hii inajumuisha jinsi ya kujiajiri n.k
  • Utengenezaji wa Tovuti: Hii inajumuisha jinsi ya kutumia WordPress n.k

Sasa mada zote ulizozipenda na kuziwekea alama ya nyota unaweza sasa kuangalia ni mada ipi itakufaa.Ili uweze kujua kama mada uliyoichagua itakufaa, unaweza kuipima kwa kutumia maswali yafuatayo:

Maswali 9 ya muhimu unayopaswa kujiuliza unapochagua mada(niche) kwa ajili ya blog yako.

Kabla ya kuchagua mada (niche) yoyote kati ya zile ulizoziwekea nyota jiulize maswali yafuatayo.

Swali #1. Je unaipenda kiasi cha kutosha mada uliyoichagua?

Unaweza kushawishika kuchagua mada kutokana na umaarufu wake.Lakini jambo la msingi kujiuliza ni kuwa ,je unaipenda kiasi cha kutosha mada uliyoichagua? Hii ni kwa sababu mada uliyoichagua utakuwa ukiitumia kwenye blog yako kwa miaka mingi ijayo. Hivyo ukichagua mada ambayo huipendi kiasi cha kutosha,kadri muda unavyokwenda utakosa hamu ya kuendelea kuandika na hivyo blog yako kufa.

Swali #2. Je una maarifa ya kutosha kutokana na mada uliyoichagua?

Kama unataka kujenga blog yenye mafanikio unatakiwa  kuandika makala ambazo zitakuwa na msaada mkubwa kwa wasomaji.Ili uweze kuwa unaandika Makala ambazo watu watazipenda na zenye kuelimisha unatakiwa kuwa na maarifa yakutosha kutokana na mada yako. Hii ni kwa sababu wasomaji watakuwa wanakutegemea wewe kuwa ni mtaalamu wa mada husika na hivyo wakati mwingine watahitaji kupata msaada wa ziada. Hivyo hakikisha una uelewa wa kutosha mada uliyoichagua.

Swali #3. Je ukiamua kuuza bidhaa au huduma kutokana na mada uliyoichagua watu watu watakuwa tayari kununua?

Kabla ya kuanzisha blog unatakiwa pia kujiuliza je kuna bidhaa au huduma yoyote ambayo utakuwa unauza kutokana mada uliyoichagua? Kwa mfano: Unahitaji kuanzisha blog kuhusiana na Biashara ndogondogo,

 Je ukiuza vitabu,kozi ,bidhaa au huduma inayohusiana na mada yako watu watakuwa tayari kununua?

Hilo pia ni swali unalopaswa kujiuliza kabla ya kuchagua mada hiyo.

Swali #5. Je mada uliyoichagua itaendelea kuhitajiwa na watu kwa miaka mingi ijayo?

Swali jingine la msingi ni kuwa, mada uliyoichagua itaendelea kuhitajiwa na watu kwa miaka mingi ijayo? Kama utachagua mada ambayo itakuwepo kwa muda mfupi halafu ikapitwa na wakati utajikuta kuwa blog yako itakuwa haihitajiki tena.

Swali #6. Je kuna ushindani kiasi kwenye mada uliyoichagua?

Unaweza ukafikiria kuwa mada nzuri ni ile ambayo haina ushindani yaani  hakuna blog nyingine zinazotoa mada hiyo. Lakini ukweli ni kuwa ukiona mada uliyoichagua haina ushindani kabisa tafsiri yake ni kuwa inawezekana mada hiyo haihitajiki sana na ndio maana hakuna blog zinazofundisha mada hiyo. Hivyo, chagua mada yenye ushindani wa wastani.

Swali #7. Je unafurahia watu wanapokutambua kuwa wewe ni mtaalam wa mada uliyoichagua?

Ili uweze kufanikiwa kwenye kazi ya blog, ni lazima kuchagua mada (Niche) unayoipenda. Ingawa hutamtangazia kila mtu kuwa wewe ni mwandishi wa blog inayoelezea mada kwa mfano ya malezi ya watoto, lakini ni jambo jema kufurahia mada uliyoichagua na pia kuona fahari watu wanapokutambua kuwa wewe ni mtaalamu wa elimu ya malezi ya watoto. Usichague mada ambayo utaona aibu kujitambulisha kwa watu kuwa wewe ni mtaalamu wa mada hiyo.

Swali#9. Je mada uliyoichagua itakuwa na Makala ambazo zitadumu kwa muda mrefu bila kupoteza thamani yake?

Hapa ninazungumzia Makala ambazo zikisomwa leo,kesho zinakuwa zimepitwa na wakati kwa mfano Makala zinazozungumzia matukio ya siku(News). Siku inapopita Makala uliyoiandika inakuwa haina thamani tena.Hivyo unapochagua mada kwenye blog yako usichague mada ambayo itakuwa na Makala ambazo thamani ya Makala zake zitadumu kwa muda mfupi.Chagua mada ambayo Makala zake zitakuwa na ubora uleule kwa miaka mingi ijayo (evergreen content). Hebu nitoe mfano wa mada ya Ujasiriamali: katika mada hiyo ukawa umeandika Makala ya “JINSI YA KUANZISHA BIASHARA BILA KUWA NA MTAJI WA PESA”. Makala hii hata ikipita miaka 10 itaendelea kuwa na ubora uleule japo kadri muda unavyoenda utakuwa ukiiboresha tu kulingana na mabadiliko ya jamii na teknolojia.

Faida ya kuwa na Makala zenye ubora unaodumu kwa muda mrefu(evergreen content) ni kuwa:

Badala ya kuandika makala mpya mara kwa mara kuvuta wasomaji wa Blog yako, Makala hizi zitakuwezesha kuvuta wasomaji kuja mara  kwa mara kwenye blog yako hata kama hujaweka Makala zingine mpya. Hii ni kwa sababu maudhui ya Makala zako yatabaki kuwa na ubora uleule.

Njia 4 ambazo unaweza kuzitumia kujihakikishia kuwa utafanikiwa kwenye mada uliyoichagua kabla ya kuanzisha Blog.  

Sasa tayari umeamua kuchagua mada ambayo utaitumia kwenye blog yako. Tutaenda kuangalia majaribio au njia ambazo utazitumia kujihakikishia kuwa utafanikiwa kwenye mada uliyoichagua.

Jaribio #1. Jaribu kufikiria na kuandika vichwa vya habari vya Makala angalau 50 vinavyohusiana na mada uliyoichagua.

Tenga muda wa kama saa moja hivi ukiwa peke yako sehemu tulivu. Chukua kalamu na daftari na jaribu kufikiria vichwa vya habari vya Makala zinazohusiana na mada yako.

Andika vichwa vya habari vingi kadiri unavyoweza . Lengo ni kuandika vichwa vya habari angalau 50.

Kwa mfano: Hebu tuchukulie kuwa umechagua mada ya MALEZI:

Hebu tuanze kufikiria vichwa vya habari vinavyoendana na mada yetu:

  1. Jinsi ya kulea mtoto akiwa bado tumboni
  2. Sababu 6 zinazoathiri ukuaji wa mtoto baada ya kuzaliwa
  3. Jinsi ugomvi kati ya baba na mama unavyoathiri malezi ya watoto
  4. Jinsi ya kuwafundisha watoto kusoma wakiwa nyumbani.
  5. ………….
  6. …………..
  7. ………….

Kama ukiishiwa vichwa vya habari kwenye hili zoezi kabla ya kufikia vichwa vya habari 50, basi hii ni dalili kuwa inawezekana mada uliyoichagua haitakuwa chaguo sahihi kwako. Hii ni kwa sababu ili blog yako ianze kupata umaarufu na kupata muitikio kutoka kwa wasomaji,unatakiwa uwe umeandike Makala nyingi Zaidi ya 50.

Jaribio #2. Fungua Ukurasa wa Facebook au Group la Facebook linalohusu Mada uliyoichagua.

Njia nyingine na ya moja kwa moja ya kuangalia mada uliyoichagua kama itakufaa ni kuanzisha ukurasa wa Facebook au Group.

Unaweza kuupa ukurasa wako au group lako jina ambalo utalitumia kwenye blog yako.

Anza kuandika Makala na kuziweka kwenye ukurasa wako au group lako. Kama utafurahia kuposti na kuanza kupata wafuasi ambao watakuwa wakikomenti na kulike basi hiyo ni dalili nzuri kuwa utafurahia kuendesha blog kwa mada uliyoichagua.

Jaribio #3. Jaribu kuandika Makala tano zinazoendana na mada yako.

Mwisho, jaribu kuandika Makala tano zinazoendana na mada yako.

Kama utaona kuandika Makala tano ni nyingi au kama utachoka (bored) baada tu ya kuandika Makala moja, basi unapaswa kufikiria upya uchaguzi wako wa mada inawezekana umechagua mada ambayo sio sahihi kwako.

Kwa ufupi: Jinsi gani unaweza kuchagua mada bora kwa ajili ya blog yako?

Hapa ninakupatia vitu vitatu vya kufuata (checklist):

 Fikiria mada nyingi iwezekanavyo kabla ya kuchagua mada moja. Kwa kuwa na mada nyingi ulizozifikiria unaweza kupata mada bora Zaidi kutokana na mada ulizozifikiria.

 Zifanyie mada zako majaribio kama nilivyokuelekeza katika Makala hii ili kupata mada moja ambayo itakuwa bora kuliko mada zingine.

 Kwa kutumia majaribio niliyokuelekeza katika Makala hii utaweza kuchagua mada (niche) bora sana kwa ajili ya blog yako.

Kwa leo niishie hapo. Kama una maoni yoyote kuhusiana na makala hii ya Jinsi ya kuchagua mada(niche) kwa ajili ya blog yako, usisite kudondosha maoni yako hapa chini. Pia kama unahitaji ushauri wowote, wasiliana nami kwa simu/whatsap 0752081669.

Asante na karibu katika makala zijazo.

error

Enjoy this blog? Please spread the word :)

Follow by Email
WhatsApp