Jinsi Ya Kuanzisha Blog Na Kutengeneza Kipato

Mwongozo rahisi wa jinsi ya kuanzisha Blog.

JINSI YA KUANZISHA BLOG NA KUTENGENEZA KIPATO

Kama umekuwa ukitafuta mwongozo rahisi wa jinsi ya kuanzisha blog yako mwenyewe na kuanza kutengeneza kipato (pesa), basi nikuhakikishie kuwa upo mahali sahihi. Katika mwongozo huu, utajifunza jinsi ya kuanzisha blog kwa kufuata hatua rahisi nane ambazo utatumia dakika 10 mpaka 15. Unaweza kubofya hapa kwenda moja kwa moja kwenye hatua ya kwanza.

Jinsi ya kuanzisha Blog na kutengeneza pesa: Fuata hatua hizi 8 rahisi.
1.Chagua Jina la Blog yako na mada (niche) utakayozungumizia.
2.Weka blog yako  mtandaoni kwa kuchagua mahali utakapoihifadhi  (web hosting)
3.Tengeneza blog yako kwa kuipatia muonekano (theme). Tumia theme za wordpress za bure
4.Andika Makala yako ya kwanza
5.Tangaza blog yako na uanze kutengeneza kipato (Pesa)
6.Tengeneza mpangokazi endelevu wa jinsi utakavyokuwa unaweka Makala kwenye blog yako
7.Jizatiti kuweka Makala mara kwa mara kwenye blog yako
8.Tumia picha za bure (free photos) ili kufanya Makala zako kuwa na mwonekano mzuri na kuvutia wasomaji.

Blog ni nini?

Blog ni tovuti ambayo huwa inawekewa Makala mara kwa mara kwa lengo la kuvutia wasomaji na kutengeneza kipato (pesa). Kama unasoma Makala hii kwenye blog yangu, nitakupatia mwongozo rahisi wa jinsi ya kuanzisha blog yako wewe mwenyewe.

Kabla sijaendelea mbele, hebu tuangalie maswali ambayo watu huuliza mara kwa mara.

Je mimi ninaweza kuanzisha blog?

Ndio! Kuanzisha blog ni rahisi sana na ni njia rahisi ya wewe kuwa na biashara yako mwenyewe ambayo itakuletea kipato kupitia mtandao wa internet mahali popote ulipo duniani. Huhitaji kuwa mwandishi aliyesomea uandishi au kuwa mtaalamu wa computer, wala huhitaji kuwa na degree kuanzisha blog na kujipatia kipato. Unaweza kuanzisha blog bila kujali umri, mahali ulipo au uzoefu na bado ukawa na blog yenye mafanikio na ukajipatia kipato mtandaoni.

Ninaweza kuanzisha blog bila kuwa na utaalamu wowote wa computer?

Hata kama hauna utaalamu wowote wa computer, kuanzisha blog ni rahisi sana na mwongozo huu umeandaliwa kwa namna rahisi na nitakuelezea hatua kwa hatua kiasi kwamba utaweza kuanzisha blog yako wewe mwenyewe leo.

Hivi inawezekana kutengeneza pesa kupitia blog kwa sasa?

Ndio, mamilioni ya watu duniani wanatengeneza pesa wakiwa nyumbani kupitia blog. Blog ni biashara inayolipa sana ambayo unaweza kuianzisha kwa mtaji mdogo sana. Pia unaweza kufanya kazi hii kwa muda wa ziada bila kuathiri muda wako wa kazi na bado ukajipatia kipato cha ziada. Fuatilia mwongozo huu ili ufahamu jinsi unavyoweza kuanzisha blog na ukajipatia kipato.

Inagharimu pesa kiasi gani kuanzisha blog?

Inategemea na malengo yako na aina ya blog unayotaka kuanzisha. Kuanzisha blog inagharimu kati ya $35 na $66 kukamilisha gharama zote za msingi kwa mwaka wa kwanza(gharama hizo ni kama vile webhosting na anuani ya blog (domain name).Unapoendelea kusoma mwongozo huu tutazungumzia namna ya kupunguza gharama hizo na hivyo kukuwezesha kuanzisha blog hata kama una bajeti ndogo.

Fuata hatua hizi 8 uweze kuanzisha blog na kutengeneza pesa mtandaoni leo.

1. Chagua jina la blog yako na mada utakayokuwa unaandika (niche).

Jambo la kwanza ni kuchagua jina na mada unayotaka kuandikia kwenye blog yako.

Jina la blog yako ndio kitu cha kwanza ambacho wasomaji wako wataanza kukiona. Kwa mfano: blogyako.com, kilimochetu.com,tusomeonline.com n.k. Hivyo jina la blog yako litaelezea kwa ujumla mada ambazo utakuwa unazungumzia kwenye Makala zako. Pia unaweza ukatumia jina lako kwa mfano kingikigongo.com au unaweza ukatumia jina la biashara yako kama lengo lako ni kutangaza biashara yako. Pia unaweza kutumia muunganiko wa maneno. Kwa mfano, kama blog yako inaelezea fursa za kutengeneza pesa kupitia mtandao wa internet unaweza kutumia mfumo wa kuunganisha maneno kupata jina la blog yako. Kwa mfano fursa kupitia internet (fursanet) n.k.  Pia unaweza kuipa blog yako jina lolote unaloona litakupendeza.

Tukija kwenye mada (niche) ya blog yako, hii ni mada ya jumla ya kile unachandika kwenye blog yako. Mfano wa mada hizo ni kama vile teknolojia, uchumi, mapishi, mtindo wa maisha, kilimo, elimu n.k. Unaweza kutumia jina la mada (niche) kuwa ndio jina la blog yako. Kwa mfano: mapishibora.com, konayateknolojia.com n.k.

2.Weka Blog yako mtandaoni kwa kuchagua mahali utakapoihifadhi (Web hosting)

Hatua ya pili unapotaka kuanzisha blog ni kuiweka mtandaoni. Ili kuweka blog mtandaoni unatakiwa kuchagua kampuni itakayoihifadhi blog yako (Web hosting). Katika hatua hii utachagua kampuni inayotoa huduma ya kuhifadhi (hosting) blog ambayo itaihifadhi blog yako mtandaoni kwa ajili yako, utachagua anuani (domain name) ya blog yako na pia utachagua mfumo utakaoutumia kuendeshea blog yako. Mfumo mzuri ninaoupendekeza ni WordPress. Sasa hebu tuangalie maana za baadhi ya maneno mapya yaliyojitokeza kwenye Makala hii.

Nini maana ya web hosting?

Ili tovuti au blog yako iweze kuonekana mtandaoni, ni lazima iwe imehifadhiwa mahali ili watu waweze kusoma mafaili ya blog yako zikiwemo Makala na vyote ambavyo utakuwa umeweka. Mahali ambapo blog yako itakuwa imehifadhiwa mtandaoni panaitwa host. Host ndio inayohifadhi blog yako kwa usalama mtandaoni na kuhakikisha kuwa inapatikana watu wanapoitafuta kila wanapoandika anuani ya blog yako. Hivyo, kama blog yako ni kingikigongo.com, kila mtu atakayeandika anuani ya kingikigongo.com atapelekwa kwenye host ambayo imehifadhi Makala ya blog yako mtandaoni.

Web hosting inagharimu kiasi gani?

Gharama za hosting zinategemea na kampuni utakayoichagua kuhost blog yako. Zinaweza kuwa kati ya $ 5 na kuendelea kwa mwezi. Lakini kwa kampuni ya Namecheap, gharama ni ndogo sana kiasi cha $ 2.8 kwa mwezi. Kampuni hii inatoa huduma bora sana za hosting na kwa bei nafuu kiasi kwamba hata kama bajeti yako ni ndogo, unaweza kumudu gharama za kuhost blog yako.

Ni web hosting gani inayotoa huduma nzuri?

Kuna web hosting nyingi ambazo zinatoa huduma nzuri kuhost blog na tovuti. Kampuni ambayo kwa uzoefu wangu nimeiona inatoa huduma bora lakini kwa gharama nafuu kiasi kwamba mtu yeyote anaweza kumudu ni Namecheap.

Bofya hapa chini kuweza kuingia kwenye web hosting ya Namecheap.

—> Bofya hapa kuingia kwenye tovuti ya Namecheap

JINSI YA KUANZISHA BLOG NA KUTENGENEZA KIPATO

Chagua kifurushi (Plan)

Jambo la kwanza utatakiwa kuchagua kifurushi cha hosting.

JINSI YA KUANZISHA BLOG NA KUTENGENEZA KIPATO

Chagua anuani ya blog yako (Domain name).

Baada ya hapo utapelekwa mahali ambapo utatakiwa kuchagua anuani ya blog yako. Utakapofikia sehemu hii, andika jina unalotaka liwe la blog yako. (mfano anzishabiashara.com).

Kama domain name ya blog yako itakuwa imechukuliwa na mtu mwingine, utatakiwa kuchagua domain name nyingine.

Baada ya kupata jina la domain, itakuwa kama inavyoonekana kwenye picha hapa chini. Baada ya hapo bofya sehemu iliyoandikwa connect to hosting.

JINSI YA KUANZISHA BLOG NA KUTENGENEZA KIPATO

Baada ya hapo utapata bili ya kiasi utakachotakiwa kulipia (gharama za domain na hosting kwa mwaka)

Kisha utatakiwa kuthibitisha oda yako.

JINSI YA KUANZISHA BLOG NA KUTENGENEZA KIPATO

Baada ya kuwa umethibitisha oda yako, ili uweze kufanya malipo utatakiwa kufungua account kwa kuwa ndio mara yako ya kwanza.

JINSI YA KUANZISHA BLOG NA KUTENGENEZA KIPATO

Baada ya kuwa umefungua account, basi utalipia kwa kutumia kadi yako. Hapa unaweza kutumia M-pesa Visa Card, Airtel Mastercard n.k. Fuata hatua zote ili kuweza kulipia.

JINSI YA KUANZISHA BLOG NA KUTENGENEZA KIPATO

Hapo tayari utakuwa umefungua account yako na kulipia Domain pamoja na hosting. Waoh! Hapo tayari utakuwa umemaliza hatua kubwa sana kuelekea kuanzisha blog yako.

Baada ya kumaliza hatua hiyo, sasa hatua inayofuata ni kuanza kutengeneza blog yako. Nitakuelekeza hatua kwa hatua jinsi ya kuweka (Install) WordPress kwenye Namecheap. Kumbuka kuwa, blog yetu tutaitengeneza kwa kutumia wordpress.

Bofya hapa kuingia Namecheap ili uweze kusajiri anuani ya blog yako (Domain name) na pia kupata huduma ya kuhost blog yako (Web hosting).

3. Tengeneza Blog yako (Kwa kutumia wordpress theme za bure)

JINSI YA KUANZISHA BLOG NA KUTENGENEZA KIPATO

Sasa tunaingia sehemu muhimu sana katika kuanzisha blog. Kutengeneza blog kwa kutumia wordpress unaweza kufikiria kuwa ni jambo gumu sana, lakini nikufahamishe tu kuwa kutengeneza blog kwa kutumia wordpress haihitaji ujuzi wowote wa lugha za computer (codes). Nimezigawa hatua hizi na kutoa maelezo ya kina na kila hatua nimetoa maelezo ya nini ufanye.

Kama unahitaji kuanzisha blog na utengeneze kipato, WordPress ndio chaguo lako la kwanza na bora Zaidi kuliko platform zingine.

Sasa hebu tuangalie baadhi ya misamiati ambayo tutaitumia kwenye mada hii.

  1. Content management system (CMS)

Nini maana ya content management system (CMS)?

Content Management System (CMS) ni mahali ambapo utakuwa unaandika na kupost Makala zako. CMS nzuri ni WordPress kwani ni rahisi kuitumia na inakuwezesha kupangilia vizuri Makala zako, kuweka video na picha na pia kuweka muonekano mzuri wa blog yako.

2.Wordpress

WordPress ni nini?

WordPress ni CMS maarufu sana duniani yenye watumiaji wengi nikiwemo na mimi. Blog hii inatumia CMS ya WordPress. Takwimu zinaonyesha kuwa Zaidi ya 60% ya blog na tovuti zote duniani zinatumia CMS ya WordPress.

Je ninatakiwa nianzishe blog kwa kutumia WordPress?

Je wordpress ni bure?

Kimsingi kuna CMS nyingi tu ambazo unaweza kuzitumia kuanzisha blog zikiwemo Blogger, Wix, Squarespace, Tumblr na Ghost, lakini ninakushauri kwa nguvu zote kutumia WordPress kama una malengo makubwa ya kutengeneza pesa kwenye blog yako na kuifanya kuwa biashara yako ya kukuingizia kipato.

Vipi kama nitaamua kutumia Wix badala ya WordPress?

Nimekuwa nikisisitiza sana kutumia CMS ya WordPress kuanzisha blog ingawa unaweza kutumia CMS zingine kama Wix.Hata hivyo changamoto kubwa ya kutumia CMS zingine kama Wix ni kuwa unakuwa hauna uhuru(flexibility) wa kubadilisha muonekano wa blog yako na pia kuweka vitu vingine ambavyo utapenda viwepo kwenye blog yako. Hivyo, kwa kuwa WordPress inakupa uhuru mkubwa wa kuweka vitu vingi kwenye blog yako, inakupa uwanja mpana wa kuwa na njia nyingi za kuingiza kipato kupitia blog yako.

Kitu cha msingi cha kuzingatia ni kuwa, WordPress ina platform mbili ambazo ni WordPress.com na WordPress.org. Zina majina yanayofanana lakini ziko zofauti kabisa. Sasa hebu tuanze kuchambua moja baada ya nyingine.

WordPress.com:

  • Ni bure kutumia lakini ina masharti mengi sana na hivyo haikupi uhuru wa kuweka mwonekano unaoutaka kwenye blog yako.
  • Haikupi uhuru wa kuweka domain unayoipenda katika mfumo wa jinalablogyako.com. Badala yake inakutaka utumie domain yenye mfumo wa jinalablogyako.wordpress.com.
  • Haikupi uhuru wa kutengeneza pesa kwa kuweka matangazo yako ya biashara (ads)
  • Haikuruhusu kuweka program tumishi (plugins) ambazo zitaongeza ubora wa blog yako.
  • Unatakiwa kulipia ili uweze kupata domain yenye mfumo wa jinalablogyako.com na pia kuondoa brand ya wordpress kwenye blog yako.

 WordPress.org:

  • Una uhuru wa kubadili muonekano wa blog yako vyovyote vile upendavyo.
  • Una uhuru wa kuchagua aina yoyote ya namna ya kujipatia kipato kwenye blog yako.
  • Kwenye blog yako unaweza kuweka duka lako la mtandaoni na watu wakanunua moja kwa moja kwenye blog yako.
  • Ada ndogo sana ambayo utailipia kwa mwezi.

Japokuwa uamuzi ni wako, lakini kama unahitaji upate manufaa makubwa kwenye blog yako na kuifanye ikue na pia kukuwezesha kutengeneza pesa mtandaoni, nakushauri utumie wordpress.org.

Jinsi ya kuweka(install) WordPress.org kwa ajili ya blog yako.

Kwa kuwa tayari utakuwa umefungua account, ingia kwenye account yako kwa kubofya sehemu ya sign in. Baada ya kuwa umeingia, bofya sehemu ya dashboard. Utafika sehemu kama inavyoonekana kwenye picha hapa chini. Baada ya hapo, bofya sehemu iliyooneshwa kwa mshale, utapata sehemu iliyoandikwa cpanel. Bofya cpanel.

JINSI YA KUANZISHA BLOG NA KUTENGENEZA KIPATO

Baada ya kuingia kwenye cpanel, bofya sehemu ya WordPress ili uweze kuinstall kama inavyoonekana hapo chini.

JINSI YA KUANZISHA BLOG NA KUTENGENEZA KIPATO

Baada ya hapo utafika mahali kama panavyoonekana kwenye picha hapa chini. Bofya install.

JINSI YA KUANZISHA BLOG NA KUTENGENEZA KIPATO

Baada ya hapo utatakiwa kuweka maelezo ya blog yako kwa kufuata maelekezo yaliyopo kwenye screen, kisha bofya install.

JINSI YA KUANZISHA BLOG NA KUTENGENEZA KIPATO

Baada ya kuwa umemaliza kujaza maelezo yote, utaweza kuingia kwenye platform ya wordpress kama inavyoonekana hapa chini. Ukiangalia kwa makini, utaona kila kitu kinachohitajika kwenye blog yako. Kwa mfano:

Posts: Mahali ambapo utaweza kuandika Makala zako

Pages: Hapa unaweza kutengeneza kurasa mbalimbali za blog yako kwa mfano: Wasiliana nasi (Contact us), Sisi Ni Nani (About Us), Huduma zetu (Our Services), Duka n.k

Appearance: Mahali ambapo utabadilisha mwonekano (theme) wa blog yako na kadhalika.

Jinsi ya kuchagua na kuweka theme nzuri ya bure kwenye blog yako.

Unapokuwa unaanzisha blog, sikushauri kuweka theme za kulipia kwenye blog yako hadi pale blog yako itakapokuwa imeanza kupata watembeleaji wengi. WordPress huwa ina theme nyingi sana za bure ambazo unaweza kuanzia kuweka kwenye blog yako. Hivyo unapotaka kuweka mwonekano (theme) kwenye blog yako, Anza kwa kuchagua sehemu iliyoandikwa: Appearance > Themes > Add New Theme  

Hapo tayari utakuwa umeweka theme ya bure kwenye blog yako. Baadaye ukitaka kubadilisha, utarudi hapo na kufuata hatua hizo na kuchagua theme nyingine ambayo utakuwa umevutiwa nayo. Kuelewa zaidi, angalia picha hapa chini.

Jinsi ya kuweka ukurasa wa mbele (homepage).

Kwa kawaida, ninashauri kuufanya ukurasa wa mbele wa blog yako kuwa sehemu ambapo Makala zako zitaonekana. Utaweza kufanya hivyo kwa kwenda sehemu iliyoandikwa Settings>Reading halafu chagua your latest posts. Kwa kufanya hivyo, kila makala unazoandika, zitaonekana kwenye ukurasa wa mbele wa blog yako.

Pia, kama unavyoona hapo juu, una uwezo wa kuchagua static page ambapo utaweza kuonyesha bidhaa unazouza, unaweza kuweka fomu ambayo watu watajisajiri na mambo mengine mengi. Lakini kwa sasa weka Makala zako zionekane ukurasa wa mbele wa blog yako hadi pale blog yako itakapokuwa na Makala nyingi na kuanza kupata umaarufu.

Jinsi ya kuweka menu kwenye blog yako.

Kwa sasa huhitaji kuwa na menu, mpaka pale utakapokuwa umetengeneza kurasa muhimu kwenye blog yako (Sisi ni Nani, Wasiliana Nasi, Duka n. k). Utakapokuwa tayari umetengeneza kurasa hizi, sasa unaweza kuweka menu ili iwe rahisi kwa watembeleaji wa blog yako kuweza kuona kurasa zako. Ili uweze kutengeneza menu, fuata hatua zifuatazo:  Appearance > Menus.

Hapo utaweza kuweka kurasa zako zote kwenye menu.

Tengeneza kurasa muhimu za Blog yako (Sisi Ni Nani, Wasiliana Nasi, Huduma Tunazotoa n.k)

Kila blog ni lazima ionyeshe taarifa za muhimu kwa wasomaji ili waweze kuelewa ni kitu gani watakipata kwenye blog hiyo, wanawezaje kuuliza maswali kama watakuwa na changamoto na wanawezaje kupata huduma zinazotolewa kwenye blog hiyo. Ili kukidhi matakwa ya wasomaji, ni lazima kila blog kuwa na kurasa mbalimbali ambazo zitawawezesha wasomaji kupata taarifa za muhimu. Mfano wa kursa za msingi kabisa kwenye blog ni: Sisi Ni Nani (About us), Wasiliana Nasi (Contact us), Kozi zetu(courses), Tembelea Duka letu (Shop) n.k. Ili uweze kutengeneza kurasa mbalimbali, bofya sehemu ya pages na uchague new kutengeneza ukurasa.

4. Andika Makala yako ya kwanza.

Sasa tunakuja kwenye msingi wa kuanzisha blog. Nao ni kuandika makala. Nataka nikuambie kuwa, watu hawatembelei blog ili waone jinsi ilivyopambwa vizuri, bali watu wanasoma blog kwa sababu kuna makala muhimu kwao ambazo zitawaelimisha na kuwawezesha kutatua matatizo au changamoto zao. Hivyo kuandika makala bora ni jambo la muhimu sana kwa ukuaji wa blog yako na ndizo zitakazoifanya blog yako iwe maarufu na kukuwezesha kutengeneza pesa.

Ili uweze kuandika Makala bora, zenye mvuto kwa wasomaji na zenye kuleta thamani kwenye maisha yao, ni lazima ujiulize maswali yafuatayo kabla ya kuandika Makala yako yoyote:

  • Kwa nini umeamua kuandika mada hiyo kwenye blog yako?
  • Kwa nini watu watapenda kusoma kile ulichoandika (ni tatizo gani au changamoto gani unayoitatua kwenye Makala yako)?

Ili uweze kujibu maswali hayo hapo juu kwenye kila Makala unayoandika, ni lazima uwe na mada maalumu uliyoichagua na kundi la watu unalolenga. Kwa kiingereza inaitwa “niche”. Kwa mfano, katika blog yangu, mada (Niche) yangu ni:

Jinsi ya kujiajiri na kutengeneza kipato (Pesa) kupitia mtandao wa internet bila kuathiri muda wa kazi.

Tatizo ninalotatua katika jamii:

Ukosefu wa ajira, na kipato kidogo kwa wale wenye ajira na waliojiajiri:

“Tunawasaidia Wajasiriamali, wafanyakazi walioajiriwa, wahitimu wa vyuo, wanafunzi wa vyuo na wote wenye ujuzi wowote kujiajiri na kutengeneza kipato kupitia mtandao wa internet bila kuathiri muda wao wa ziada.”

Kundi la watu ninalolenga:

Wajasiriamali, wafanyakazi walioajiriwa, wahitimu wa vyuo, wanafunzi wa vyuo na wote wenye ujuzi wowote.

Hivyo, kila makala unayoandika inatakiwa iwe inaelezea mada uliyoichagua kwenye blog yako.

Sasa hebu tuangalie kwa undani neno Niche

Niche ni nini?

Niche ni mada unayoielezea kwenye blog yako. Lakini pia neno hili linaenda mbali zaidi kwani linaelezea pia kundi la watu ambao unahitaji mada yako iwafikie, namna ambavyo utakuwa ukifikisha ujumbe wako na jinsi ambavyo utajipambanua wewe kama mtaalamu wa hiyo mada unayofundisha.

Sasa, baada ya kuwa umeamua ni mada gani utakuwa ukiandikia makala zako, kazi inayofuata ni kuanza kuandika makala. Kumbuka kuwa, makala zako zote zinatakiwa zilenge kwenye mada (Niche). Kwa mfano; Kama blog yako inahusu kilimo, usichanganye makala kwa kuweka makala za siasa. Ni lazima makala zako ziwe zinazohusu mada (Niche) uliyoichagua yaani, kilimo.

Jinsi ya kuandika Makala kwenye Blog yako.

Baada ya kuwa umeandaa Makala yako, sasa ni wakati wa kuiweka kwenye blog yako. Fuata utaratibu huu: Nenda sehemu iliyoandikwa

Posts

Baada ya hapo, bofya sehemu iliyoandikwa Add New.

Baada ya hapo, utapelekwa sehemu wazi ambayo ndiyo mahali ambapo utaandika Makala yako.

Kanuni 4 za kufanya Makala zako kuwa zenye mwonekano mzuri.

Sasa hebu tuangalie ni kwa namna gani unaweza kuandika Makala zenye mvuto kwa wasomaji wako.

1. Hakikisha Makala zako zinasomeka kwa urahisi.

Hakikisha unatumia maandishi makubwa kwenye Makala zako ili iwe rahisi kwa wasomaji wako kusoma bila kuumia macho. Pia tumia rangi ambazo haziumizi macho na zinazosomeka kwa urahisi.

2. Weka picha kwenye Makala zako.

Binadamu anakumbuka anaposoma na anapoona. Hivyo kama utaweka picha kwenye makala zako, wasomaji wako wataweza kukumbuka kwa urahisi makala zako. Hivyo, hakikisha katika kila makala yako, unaweka picha inayoendana na kile unachoelezea.

3. Gawanya Makala yako katika vichwa vya habari vidogovidogo.

Watu huwa wanachoka haraka wanaposoma Makala ndefu. Ili kuwafanya wasomaji wako kufurahia makala zako hata kama zikiwa ndefu, gawanya Makala zako kwa kuweka vichwa vya habari vidogovidogo ndani ya kila Makala yako. Pia unaweza kuweka picha kwenye kila kichwa kidogo cha habari ndani ya makala zako.

4. Kazia pointi za msingi kwa kubadilisha aina ya mwandiko (unaweza kubold au kuweka maandishi ya italic)

Hakikisha unabadili aina ya mwandiko unapokuwa unakazia point kwenye makala zako. Hii itawafanya wasomaji wako kuelewa kwa urahisi point za msingi kwenye makala zako.

Jinsi ya kuweka Makala yako kwenye blog.

Baada ya kuwa umemaliza kuandika makala yako, sasa ni wakati wa kuiweka kwenye blog ili iweze kusomwa na watu (publish). Utaweza kufanya hivyo kwa kubofya publish.

Baada ya kupublish makala yako, sasa ni wakati wa kuitangaza blog yako ili kupata wasomaji.

5. Tangaza blog yako na uanze kutengeneza kipato(Pesa)

Katika sehemu hii tutaangalia njia ambazo utazitumia kutangaza Makala za blog yako:

i.Tumia mitandao ya kijamii kutangaza blog yako.

Kimsingi mitandao ya kijamii ni sehemu ambazo watu huwa wanatumia muda wao mwingi kuchati na marafiki zao, kuangalia na kusoma habari mbalimbali. Mitandao hiyo ni facebook, Twitter, Youtube, LinkedIn, Instagram n.k. Mitandao hii ni mizuri sana kutangaza makala zako. Hivyo kila makala unayoichapisha kwenye blog yako, jitahidi kuishare kwenye mitandao ya kijamii.

Jinsi ya kuchagua mitandao ya kijamii kutangaza blog yako.

 Kila mtandao wa kijamii una aina ya wasomaji na hivyo unapaswa kuwa makini na aina za makala zinazopendwa na watu ndani ya mtandao husika. Kwa mfano:

  • Facebook: Video, Picha na Makala za maandishi.
  • Instagram: Picha zenye ubora na kuvutia, Nukuu (quotes), na habari fupifupi.
  • Twitter: Habari, Makala na Nukuu.
  • YouTube: Video  
  • LinkedIn: Makala za kitaalamu.

Jinsi ya kutumia mtandao wa Youtube kutangaza blog yako.

YouTube ni mtandao wa pili kwa umaarufu baada ya Google. Hii inamaanisha kuwa ukiutumia mtandao wa Youtube vizuri unaweza kupata wasomaji wengi sana kwenye blog yako.

Mara tu baada ya kuanzisha blog unaweza pia kuanzisha channel ya Youtube ambako utakuwa unaweka video mbalimbali zinazowiana na makala zako. Lengo la kuanzisha channel ni kupata wafuasi (Subscribers) ambao pia ndio watakuwa wasomaji wa blog yako. Katika kila video unayoiweka Youtube, Chini ya video yako, weka maelezo ya video hiyo na uweke link ili kila anayeangalia video yako, akitaka maelezo zaidi abofye hiyo link kwenda kwenye blog yako ambako atasoma makala zako.

ii.Jiunge na Majukwaa mbalimbali pamoja na magroup ya facebook.

Pia unaweza kujiunga na majukwaa mbalimbali kwa mfano Jamii forum pamoja na magroup mbalimbali ya facebook. Unapokuwa umeandika makala yako, unaweza pia kuiweka kwenye majukwaa mbalimbali. Hii itakufanya uwe maarufu na watu kukuamini kuwa wewe ni mtaalamu na umebobea kwenye eneo hilo.

Pia jiunge na magroup mbalimbali facebook yanayoendana na kile unachokiandikia kwenye blog yako. Share makala zako kwenye magroup hayo ili kupata wasomaji kwenye blog yako.

iii.Tumia email kukuza blog yako (email newsletter)

Email ni njia nzuri sana ya kuongeza wasomaji kwenye blog yako. Hii ni njia ambayo unaitumia kukusanya email za wasomaji wako ili uweze kuwa unawatumia makala au ofa mbalimbali ambazo utakuwa unazitoa kwenye blog yako. Njia hii ni rahisi. Weka fomu ya kujisajiri kwenye blog yako, halafu weka zawadi yoyote kama vile kitabu pepe. Kila mtu atakayetaka kupakua kitabu hicho itabidi ajisajiri kwa kuweka Jina lake na email yake ndio aweze kukipakua. Kwa kufanya hivyo utaweza kukusanya email za wasomaji wako.Email hizo utazitumia kuwatumia taarifa kila unapoweka makala mpya kwenye blog yako. Pia utazitumia kuwapa taarifa za ofa na bidhaa mbalimbali ambazo utaamua kuziuza kwa wasomaji wako.

Kuna software nyingi za kulipia ambazo unaweza kuzitumia kukusanya email za wasomaji wako, mfano ConvertKit na Aweber. Hizi software ni za kulipia. Lakini kuna software ya bure kabisa kutumia ambayo ni Mailchimp ambayo inakusanya email za wasomaji wako 2000 bure kwa mwezi. Idadi ambayo ni kubwa mno kwa wewe ambaye ndio unaanza kukuza blog yako. Hivyo kama ndio unaanza kukuza blog yako, nakushauri utumie Mailchimp.

Njia 5 za kutengeneza kipato (Pesa) kupitia blog.

Kuna sababu kwa nini nimeweka hizi njia za kujipatia kipato kupitia blog karibia mwishoni mwa mwongozo huu. Hii ni kwa sababu ili uweze kutengeneza kipato kupitia blog, kwanza unatakiwa uwe umepata wasomaji wa kutosha na pia uwe umejenga mahusiano ya kutosha na wasomaji wako. Mahusiano hayo yatajengwa pale ambapo utakuwa unaandika Makala bora ambazo zitawasaidia wasomaji wako kutatua matatizo yao. Hapo wasomaji wako watakupenda kupitia kile unachokiandika na utaweza kuwa na ushawishi wa kuwauzia huduma au bidhaa uliyonayo.

Sasa hebu tuangalie njia 8 za kutengeneza kipato kupitia blog yako.

1. Uza huduma kutokana na ujuzi ulionao.

Kwa sababu utakuwa umeandika makala ambazo zitakuwa zinagusa changamoto za wasomaji wako, unaweza kuwauzia huduma mbalimbali kutokana na ujuzi unaoutoa kwenye blog yako. Watu watapenda kujifunza kwa undani zaidi kile unachokiandika kwenye blog yako au kuhitaji ushauri. Hivyo unaweza kutoza pesa kidogo ili uweze kutoa ujuzi zaidi kwa kile unachofundisha. Pia unaweza kutoza pesa watu wanapohitaji ushauri wa kina kutokana na changamoto ulizozitatua kupitia makala zako.

2. Tangaza bidhaa za makampuni mengine (Affiliate Programs)

Pia blog yako ikiwa maarufu unaweza kuwasiliana na makampuni yanayotoa huduma au kuuza bidhaa zinazoendana na maudhui ya blog yako na ukakubaliana nao kutangaza bidhaa zao na kupata gawio (commissions).

3. Toza pesa watu wanapotaka kutangaza huduma zao kwenye blog yako (Sponsored Content)

Kama utakuwa na idadi kubwa ya wasomaji kwenye blog yako, wajasiriamali au makampuni watahitaji kuweka makala zinazotangaza bidhaa zao kwenye blog yako ili ziweze kuwafikia watu wengi zaidi. Hivyo unaweza kutoza kiasi fulani cha pesa kwa huduma hiyo.

4. Andaa kozi na uuze mtandaoni (Online Courses)

Kwa kuwa utakuwa na makala nyingi ambazo utakuwa umeziandika na pia una ujuzi wa kutosha kwa kile unachofundisha, unaweza kuandaa kozi kutokana na makala zako na ukaziuza kwa wasomaji wako.

5. Anzisha duka mtandaoni (eCommerce) na uuze bidhaa zako mwenyewe kwenye blog yako.

Naipenda sana wordpress kwani unaweza kuanzisha duka kwenye blog yako na watu wakanunua bidhaa zako moja kwa moja kwenye blog yako. Hivyo unaweza kuanzisha duka kwenye blog yako na ukauza bidhaa zinazoendana na blog yako na watu wakanunua.Jambo la kufurahisha ni kuwa unaweza kuunganisha pia mfumo wa malipo kwenye duka lako na watu wakanunua bidhaa zako kwa kulipia moja kwa moja kwa kutumia simu zao au kadi za benki.

6. Tengeneza mpangokazi endelevu wa jinsi utakavyokuwa unaweka makala kwenye blog yako

Ili uweze kufanikiwa kukuza blog yako, unapaswa kuandika makala bora. Hivyo, ili uweze kufanikiwa kuandika makala zenye mvuto na watu wakaipenda blog yako, unapaswa kuweka mpangokazi wa namna ambavyo utakuwa unaweka makala kwenye blog yako. Mpango kazi huo uonyeshe ratiba ya kuweka makala na aina ya makala ambazo utakuwa unaandika.

7. Jizatiti kuweka Makala mara kwa mara kwenye blog yako

Kama unataka watu watembelee mara kwa mara blog yako, unatakiwa kuwapa sababu ya wao kutembelea blog yako.

Hivyo unatakiwa uwe na ratiba maalum ya kuweka makala kwenye blog yako. Kuna sababu nyingi za wewe kuwa na ratiba maalum ya kuweka makala kwenye blog yako. Miongoni mwa sababu hizo ni hizi zifuatazo:

Kuwapa wasomaji wako mategemeo ya kuwa watapata makala na maarifa mapya kila wanapotembelea blog yako: Kwa sababu wasomaji wako watakuwa wanajua ratiba yako ya kuweka makala mpya (kila siku, kila wiki au kila mwezi), basi kila wanapotembelea blog yako watakuta makala mpya na hivyo watapenda kufuatilia blog yako. Kujiwekea malengo wewe mwenyewe ya kukuza blog yako: Unapokuwa na ratiba maalum ya kuweka Makala kwenye blog yako na ukaifuata ipasavyo, utakuwa unajijengea nidhamu kwenye kazi yako na hivyo utakuwa unajua ni muda gani uweke makala mpya. Pia unapokuwa unaweka makala mpya mara kwa mara na kwa ratiba maalum utaweza kujua ni makala zipi au maarifa yapi yamependwa zaidi na wasomaji wako na hivyo kukupatia mwanga uwekeze nguvu zaidi kwenye maarifa gani.

Hivyo, hata kama blog yako haitakuwa na wasomaji wengi mwanzoni, jinsi unavyoandika makala nyingi kutaifanya blog yako kupata wasomaji wengi.

Kama ulikuwa umeweka malengo ya kuandika makala yenye maneno 1000 kila juma na ukashindwa kufikia malengo hayo, ni bora uweke hata kama ni makala yenye maneno 500 kuliko kuacha kabisa. Ni bora kuweka makala na ukafuata ratiba yako hata kama makala ni fupi kuliko kuacha kabisa ukisubiri mpaka uwe umekamilika. Kumbuka kuwa Kuna msemo wa Kingereza unaosema “done is better than perfect”. Kwa tafsiri isiyo rasmi ni kuwa “Ni bora kutenda jambo kuliko kusubiri mpaka uone kuwa umekamilika kulitenda kwa ukamilifu ndio utende”. Hivyo ukisubiri mpaka uwe umekamilika utaua blog yako.

8. Tumia picha za bure (free photos) ili kufanya Makala zako kuwa na mwonekano mzuri na kuvutia wasomaji.

Kabla hujaweka Makala mpya kwenye blog yako, kuna jambo moja la msingi unalopaswa kulifanya nalo ni kuweka picha.

Utafiti unaonyesha kuwa makala zenye picha hupata wasomaji wengi, 94% zaidi ya makala ambazo hazina picha. Pia tunapokuja kwenye mitandao ya kijamii, makala zenye picha hupata shares nyingi kama ifuatavyo: tweets zenye picha hupata 150% ya retweets kuliko ambazo hazina.  Wakati kwenye Facebook makala zenye picha hupata shares na likes mara 2.3 kuliko ambazo hazina.

Hivyo weka picha kwenye makala zako ili kuzifanya ziwe na mwonekano mzuri wenye kuvutia na hivyo kuongeza wasomaji kwenye blog yako.

Tovuti unazoweza kupata picha za bure zisizokuwa na hatimiliki ambazo utazitumia kuweka kwenye Makala yako.

Njia moja rahisi ya kufanya makala zako kuwa zenya mvuto ni kuweka picha. Sasa zifuatazo ni tovuti ambazo unaweza kuzitumia kuweza kupata picha za bure kwa ajili ya blog yako. Kumbuka kuwa blog ni biashara hivyo unapochukuachukua picha sehemu yoyote mtandaoni unajiweka katika hatari ya kuchukua picha ambazo zinalindwa na hakimiliki. Hivyo ili kuepuka hilo, nimekuwekea tovuti ambazo utazitumia kupata picha hizo bila kuwa na wasiwasi.

1. Unsplash

Unsplash ni tovuti nzuri sana yenye picha nyingi ambayo unaweza kuitumia kupata picha kwa ajili ya blog yako. Picha zote zilizopo kwenye tovuti hii zina ubora wa hali ya juu sana na una uhuru wa kuzipakua (download) bila masharti yoyote.

2. Death to Stock

Hii ni tovuti nyingine yenye picha nzuri na zenye ubora. Lakini kwenye tovuti hii wanatoza kiasi cha $12 kwa mwezi. Hivyo, kama una bajeti na unahitaji kupata picha bora Zaidi, basi unaweza kuingia kwenye tovuti hii na ukalipia. Lakini kwa ushauri wangu unaweza tu kutumia picha za bure kutoka kwenye tovuti niliyoielezea hapo juu.

3. Pixabay

Hii ni ni tovuti nyingine ambayo unaweza kupata picha za bure kabisa. Hivyo unaweza kuitembelea ili uweze kupata picha kwa ajili ya blog yako.

Tovuti bora za bure kwa ajili ya kufanyia ubunifu(design) picha na Makala zako.

Pia pamoja kuweka picha kwenye makala zako, unaweza pia kuamua kuweka ubunifu kwenye picha zako na makala zako kwa ujumla. Hapa nimekuwekea tovuti ambazo unaweza kuzitumia kufanya ubunifu (design) wako wowote bure.

1. Canva 

Canva ni tovuti ya bure ambayo unaweza kuitumia kufanya ubunifu kwenye picha zako. Tovuti hii imekuwepo toka mwaka 2012.Tovuti hii ni nzuri sana kwani unaweza hata kuitumia kufanya ubunifu kwenye machapisho yako unayoyaweka kwenye mitandao ya kijamii, pia unaweza hata kutengeneza logo mwenyewe.

2. Visme 

Pia kama ilivyo Canva, Visme ni tovuti ambayo unaweza kuitumia kuweka ubunifu kwenye Makala zako.

3. Noun Project 

Kama unahitaji pia kutengeneza alama (icons) ambazo unaweza kuzitumia kwenye logo au sehemu yoyote unaweza kutumia tovuti hii bure.

Kwa ufupi: Jinsi ya kuanzisha Blog na kutengeneza pesa kupitia mtandao wa Internet

Sasa hebu nimalizie Makala hii kwa kuweka ufupisho wa jinsi ya kuanzisha blog na kutengeneza pesa kupitia mtandao wa internet.

Unapotaka kuanzisha blog na kutengeneza pesa kupitia internet unatakiwa kufuata hatua hizi:

  • Chagua mada (niche) pamoja na jina la blog yako.
  • Chagua anuani ya blog yako mtandaoni(domain name)
  • Weka blog yako mtandaoni (Web hosting)
  • Chagua WordPress kwa ajili ya kuendeshea blog yako.
  • Weka mwonekano wa blog yako (theme) kwa kutumia theme za bure za WordPress.
  • Anza kuandika makala yako ya kwanza na kuendelea.
  • Tangaza blog yako yako ili iweze kuwa maarufu na uanze kujipatia kipato kwa njia mbalimbali ambazo utakuwa umezichagua.
  • Jizatiti kuweka makala mara kwa mara kwenye blog yako.
  • Tumia tovuti za bure kupata picha na kufanya ubunifu kwenye Makala zako ili ziweze kuwa na mvuto.

Je una maoni Zaidi jinsi ya kuanzisha blog na kutengeneza pesa kupitia mtandao wa internet?

Usisite kuweka maoni yako hapa chini. Kama utahitaji nikutengenezee tovuti au blog usisite kuwasiliana nami. Pia wasiliana nami kwa simu na. 0752081669 kwa ushauri zaidi. Asante na karibu kwenye makala zangu zinazofuata.

Kingi Kigongo
Ungana nae
Latest posts by Kingi Kigongo (see all)

10 Replies to “Jinsi Ya Kuanzisha Blog Na Kutengeneza Kipato”

  1. nashukuru sana nimejifunza kitu kutokana na makala yako hii nzuri. naomba kuuliza mfano brog ikiwa na watembeleaji wengi tofauti na njia ulizozipndekeza kupata pesa. watu wakitembelea sana unaweza kuwa unalipwa kwa dollar. inakuhitaji uwe na watembleaji wangapi ili uweze kulipwa?

    1. Asante sana kwa Swali zuri.
      Njia nyingine ambayo unaweza kuitumia kutengeneza kipato ni kwa kuweka matangazo ya Google. Program hii inajulikana Kama ‘Google Adsense’. Ili uweze kukidhi vigezo, ni lazima blog yako iwe ya Kingereza au lugha zingine za kimataifa.

  2. Asante sana, nimehitaji kwa muda mrefu kuwa na blog kwa ajili ya makala zangu, leo nimepata elimu na nimejua pa kuanzia na mtu wa kuniongoza, Mungu akubariki ndugu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error

Enjoy this blog? Please spread the word :)

Follow by Email
WhatsApp