Jinsi Ya Kuanzisha YouTube Channel Na Kutengeneza Kipato.

Mwongozo wa bure wa jinsi ya kuanzisha Youtube channel, kuandaa video na kutengeneza kipato.

Jinsi ya kuanzisha Youtube channel na kutengeneza kipato.

Katika mwongozo huu nitazungumzia jinsi unavyoweza kuanzisha Youtube channel na kutengeneza kipato. Sasa hebu nianze kuzungumzia kuhusu Youtube. Kila mmoja wetu inawezekana hutumia muda wake fulani kwa kuingia youtube na kuangalia video mbalimbali.

YouTube ni mtandao ambao umekuwa maarufu sana kwa kutoa maudhui yanayoburudisha katika mfumo wa video. Pia youtube imekuwa ikitumiwa na wafanyabiashara, wajasiriamali na makampuni mbalimbali kutangaza biashara zao. Kimsingi, zaidi ya nusu ya wafanyabiashara  (55%) duniani hutumia YouTube kama njia mojawapo ya kutangaza biashara zao.

Pia utafiti unaonesha kuwa, robo ya watumiaji wa mtandao wa internet hutumia masaa 10 au zaidi kuangalia video mtandaoni, na mtandao wa YouTube una wafuasi mpaka sasa wanaokadiriwa kufikia billion mbili ulimwenguni. Pia mtandao huu umetanuka sana kiasi kwamba unaweza kupatikana kwa lugha tofauti 76.

Je, bado unahitaji ushahidi zaidi?

Si hivyo tu, mtandao wa YouTube ni wa pili kwa ukubwa, hivyo kwa kutumia mtandao wa youtube kwenye biashara yako, utaweza kukuza brand yako. Mtandao wa youtube pia huwawezesha wafanyabiashara na wajasiriamali kuweza kuandaa maudhui  yanayopendwa na watu ambayo watu watajifunza na kuwashirikisha marafiki zao.

Katika mwongozo huu, nitazungumzia hatua kwa hatua jinsi ya kuanzisha youtube channel na kutengeneza kipato. Hii itajumuisha:

  1. jinsi ya kuanzisha Channel ya youtube,
  2. jinsi ya kutengeneza video,
  3. jinsi ya kufanya video zako ziweze kuonekana kwa urahisi mtandaoni (search engine optimization(SEO)),
  4. jinsi ya kutangaza Youtube channel yako ili kupata watazamaji wengi,
  5. dondoo mbalimbali za jinsi ya kutangaza youtube channel yako kwa mafanikio makubwa
  6. software ambazo zitakusaidia kuweza kutangaza channel yako kwa urahisi na kupata watazamaji wengi.
  1. Jinsi ya kuanzisha channel ya YouTube

Sasa, tayari umefanya maamuzi ya kuanzisha YouTube channel, hilo ni jambo jema sana! Ili uweze kufanikiwa, unatakiwa kufahamu mambo kadha wa kadha. Miongoni mwa mambo hayo ni:

  1. kutambua malengo hasa ya wewe kuanzisha channel,
  2. kuchagua mada utakayokuwa unafundisha kwenye channel yako,
  3. jinsi ya kutanga channel yako na
  4. njia utakazokuwa unazitumia kuingiza kipato. 

Kabla hatujaingia ndani zaidi, ni muhimu kufahamu kuwa ili kuwa na channel ya youtube yenye mafanikio, inahitajika kuwa na muda mwingi wa maandalizi na uendeshaji.

Sasa je uko tayari?

Tofauti na mitandao mingine ya kijamii, mtandao wa youtube ni mtandao unaohusika na maudhui ya video tu. Hivyo unatakiwa kuwa na muda wa kupanga, kurekodi, kuedit na kutangaza video zako ili ziweze kupata watazamaji wengi. Pia unatakiwa kufahamu malengo yako hasa ya kuanzisha channel ya youtube na kurekodi video ili kuweza kukuza brand yako mtandaoni. Kama utatumia muda na nguvu ya kutosha, utaweza kutengeneza video zinazovutia na ambazo watu watatamani kuwashirikisha marafiki zao na hivyo kuwa na kundi kubwa linalokufuatialia. Zifuatazo ni hatua unazopaswa kuzifuata.

Fungua akaundi ya Google (Gmail).

Kabla ya kuanza kurekodi video zako na kuziweka youtube, utatakiwa kuanzisha channel ya Youtube. Kwa kuwa mtandao wa youtube unamilikiwa na Google, mara tu unapokuwa umefungua akaunti ya Gmail, tayari utakuwa na uwezo wa kuingia youtube na kufungua channel.

Kutegemea na aina ya biashara yako, unaweza ukaamua kutenganisha kati ya email yako binafsi na email utakayoitumia kufungulia channel yako ili kutenganisha email zako binafsi na biashara yako.

Hatua ya 1: Tembelea Google 

Jinsi ya kuanzisha Youtube channel na kutengeneza kipato.

Hatua ya 2: Andika neno Gmail na utafute kwenye Google.

Jinsi ya kuanzisha Youtube channel na kutengeneza kipato.

Hatua ya 3: Bofya sehemu ya Sign in kama inavyooneshwa kwenye picha hapa chini ili uweze kufungua account yako ya Gmail.

Jinsi ya kuanzisha Youtube channel na kutengeneza kipato.

Hatua ya 4: Utaona maelekezo yanayokuuliza to create an account for yourself au to manage your business. Kwa kuwa youtube account yako itakuwa kwa ajili ya biashara yako, chagua To manage my business.

Jinsi ya kuanzisha Youtube channel na kutengeneza kipato.

Hatua ya 5: Ili uweze kufungua akaunti ya Google, weka jina lako, jina la email unalotaka kutumia na password kabla ya kubofya Next. Baada ya hapo, weka email ambayo utaitumia kurudisha email yako kama itapata tatizo au ikiwa utasahau password (recovery email) na tarehe yako ya kuzaliwa, jinsia na namba yako ya simu. 

Jinsi ya kuanzisha Youtube channel na kutengeneza kipato.

Zingatia: Google inaruhusu watumiaji wenye umri wa kuanzia miaka 13 na kuendelea. 

Hatua ya 6: Utatakiwa kuweka namba yako ya simu ili uweze kupokea code utakazoziweka ili kufungua akaunti yako.

Jinsi ya kuanzisha Youtube channel na kutengeneza kipato.

Hatua ya 7: Mwisho kabisa, kubaliana na vigezo na masharti ya Google (Google’s Privacy Policy and Terms of Service). Baada ya kuwa umekubaliana na vigezo na masharti, utatumiwa ujumbe kwenye simu yako wenye herufi na namba (code) ambazo utaziweka kwenye kibox ambacho utakuwa umeelekezwa. Baada ya kuwa umekamilisha mambo hayo yote, tayari utakuwa umefanikiwa kufungua akaunti ya Google

Kufungua akaunti ya Youtube

Sasa tayari una akaunti ya Google, na unakaribia kuanza kuweka video zako. Lakini, kabla ya kufanya hivyo, unatakiwa kufungua channel ya Youtube. Akaunti ya Youtube itakuwezesha wewe kuweza kuweka video zako na kuziboresha (editing)

Hatua ya  1: Tembelea YouTube. Ukiangalia upande wa kulia kwenye kona ya juu kabisa, kwa kuwa tayari utakuwa umefungua Google akaunti, itaonekana kama ilivyo hapo chini. Hii inaonesha kuwa tayari umeshaingia kwenye akaunti ya Youtube. Au inaweza kuonesha Sign in. Kama itaonesha sign in, utabofya mahali palipoandikwa sign in na utaweka email yako na password yako ili kuweza kuingia.

Jinsi ya kuanzisha Youtube channel na kutengeneza kipato.

Hatua ya pili 2: Baada ya kuwa umeingia, bofya kwenye account module 

Jinsi ya kuanzisha Youtube channel na kutengeneza kipato.

Hatua ya 3: kisha chagua maneno Create channel kati ya maneno yatakayokuwa yamejitokeza hapo chini baada ya kubofya.

Jinsi ya kuanzisha Youtube channel na kutengeneza kipato.

Hatua ya 4: Andika jina la Channel na kisha bofya Create Channel.

Zingatia: Unaweza  kubadilisha jina la channel yako muda wowote kwa kwenda kwenye account settings, hivyo, usiwe na wasiwasi kama utakuwa huna uhakika na jina la channel ambalo utakuwa umelichagua kwani unaweza kulibadilisha muda wowote. 

Jinsi ya kuboresha mwonekano wa channel yako.

Hatua ya 1: Bofya Customize Channel kuanza kuboresha channel yako.

Hatua ya 2: Bofya sehemu iliyoandikwa branding ili kuweka picha au logo ya channel yako (channel profile picture) pamoja na picha ya cava ya channel yako (channel art). Sehemu hizi mbili ndio zinazoonekana kwanza kabisa wakati watu wanapotembelea channel yako, Hivyo, hakikisha kuwa picha unazoziweka ziwe zinaendana na Brand yako (Maudhui au huduma unazotoa).

Hatua ya 3:  Weka picha pamoja na kava ya channel yako.

Hatua ya 4:  Bofya sehemu ya Basic info ili uweze kuweka maelezo ya msingi ya channel yako. Hii ni pamoja na maelezo ya mada unayozungumzia kwenye channel yako au huduma unayotoa kupitia video zako, email ya kampuni yako pamoja na link za tovuti yako pamoja na mitandao yako ya kijamii.

Hatua ya 5: Weka maelezo ya msingi ya channel yako. Hii ni pamoja na kubadili jina la channel yako, maelezo ya mada unayozungumzia kwenye channel yako au huduma unayotoa kupitia video zako, email ya kampuni yako pamoja na link za tovuti yako pamoja na mitandao yako ya kijamii.

Baada ya kumaliza kuweka maelezo ya channel yako, sasa ni wakati wa kuboresha mwonekano wa channel yako kwa wale waliojiunga (subscribers) na wale ambao hawajajiunga kwenye channel yako. Hapa unaweka mwonekano wa channel yako kwa wale waliojiunga uwe tofauti na mwonekano kwa wale ambao bado hawajajiunga(subscribe).

Njia nzuri ya kutumia hapa ni kuweka video ya utangulizi (trailer) ili ionekane kwa watu wote ambao hawajajiunga na channel yako ili wahamasike kujiunga.

Ili uweze kuweka video ya trailer unapaswa kufuata hatua zilezile ambazo utazitumia kuweka video ya kawaida.

Unaweza kurekodi video mbili tofauti, moja ikiwa video yako ya kawaida ambayo itaonekana kwa watu waliojiunga kwenye channel yako na nyingine ikiwa ni video fupi ya trailer ambayo itaonekana kwa watu ambao hawajajiunga kwenye channel yako.

Hatua ya 1: Anza kwa kuweka video yako ya kwanza kwa kuchagua sehemu iliyoandikwa Content inayoonekana kwenye menu upande wa kushoto kama inavyoonekana kwenye picha hapa chini. Baadaye, bofya sehemu iliyoandikwa Upload Videos.

Hatua ya 2: Bofya sehemu iliyoandikwa select kama inavyoonekana kwenye picha hapa chini.

Hatua ya 3: chagua video kutoka kwenye computer yako unayotaka kuiweka kwenye channel yako.

Hatua ya 5: Fuata hatua zote kama zilivyooneshwa kwenye picha hapo chini. 1. Weka Kichwa cha habari cha video yako, 2. Weka maelezo yanayoitambulisha video yako. Baada ya hapo weka thumbnail. Thumbnail ni picha inayoonekana juu ya video kabla haujafungua video ukiwa Youtube. Baada ya hapo bofya NEXT.

Hatua ya 6: Bainisha kama video yako inaruhusiwa kutizamwa na watu wote wakiwemo watoto. Baada ya hapo bofya NEXT.

Hatua ya 7: Sasa ni wakati wa kupublish video yako. Chagua Public ili video yako iweze kuonekana na kila mtu.

Hatua ya 8: Unaweza ukaamua kushare video yako kwenye mitandao ya kijamii ili uweze kupata watazamaji wengi.

Sasa video yako ya kwanza tayari imeshawekwa Youtube. Sasa ni wakati wa kuweka video ya trailer.

Hatua ya 1: Rudi kwenye Your channel na uchague Customize Channel.

Zingatia: Video uliyoiweka itaonekana hapa kama inavyooneshwa kwenye picha hapa chini.

Hatua ya 2: Chagua Add Channel trailer for people who haven’t subscribed.

Hatua ya 3: Chagua video utakayoifanya kuwa trailer kutoka miongoni mwa video ulizoziweka kwenye channel yako.

Jinsi unavyoweza kuanzisha Youtube channel na kutengeneza kipato.

Hatua ya 7: Bofya Publish ili video yako ya trailer iweze kuonekana kwa watu wote ambao hawajajiunga (not subscribed) kwenye channel yako.

Jinsi ya kuanzisha YouTube Channel ya pili.

Je inahitajika kuanzisha YouTube channel ya pili kwenye akaunti yako ya Google? Habari njema ni kuwa, YouTube inakuruhusu kufungua Channel nyingine kwa kutumia akaunti yako ya Gmail.

Inawezekana ukawa unahitaji kuwa na channel mbili, moja kwa ajili ya Biashara yako, na nyingine kwa ajili ya Mambo yako binafsi. Ili uweze kufanya hivyo, fuata hatua zifuatazo:

Hatua ya 1: Nenda kwenye picha ya akaunti yako (Profile Picture) na uchague Settings.

Jinsi unavyoweza kuanzisha Youtube channel na kutengeneza kipato.

Hatua ya 2: Chagua Create a Channel ili uweze kuanzisha channel mpya.

Jinsi unavyoweza kuanzisha Youtube channel na kutengeneza kipato.

Hatua ya 4: Weka Jina la Channel yako na uchague Create ili uweze kuanzisha channel.

Hatua ya 5: Boresha channel yako mpya kwa kufuata maelekezo ya mwanzo kabisa ulipokuwa unatengeneza channel ya kwanza.

Maelekezo ya jinsi ya kukuza Brand yako kwa kutumia YouTube Channel.

Channel ya YouTube inawakilisha Brand yako. Hivyo ili uweze kukuza Brand yako kwa kutumia Channel yako, ni muhimu kufuata maelekezo yafuatayo:

  • Jina la Channel: Hakikisha Jina la Channel yako linafanana au linawakilisha vyema huduma au Biashara unayofanya. Pia Jina hilo lifanane kwenye mitandao yako yote ya Kijamii pamoja na tovuti yako Kama unayo. Pia weka video zinazowiana na huduma unayotoa.
  • Weka logo ya Channel yako: Google inaruhusu kuweka logo yenye ukubwa wa 800 x 800 px ikiwa ni mraba au ya mduara. Hakikisha logo yako iwe inafanana na picha yako ya ukurasa wa Facebook (Facebook profile picture). Picha au logo uliyoiweka kwenye channel yako ndiyo itakayotumika kwenye mitandao yako yote ya kijamii.
  • Weka picha ya Channel yako (Cover image): Weka picha yenye ukubwa wa 2560 x 1440 px ambayo itaonekana vizuri kwenye aina zote za vifaa vya kielectronic vikiwemo Simu janja, Vishikwambi (tablet), Computer za mezani, kompyuta mpakato na Television.
  • Weka maelezo yanayoitambulisha channel yako: maelezo utakayoweka yaelezee channel yako inatoa huduma gani na watazamaji wategemee video zenye maudhui gani.
  • Weka video fupi inayotambulisha channel yako (Channel trailer): Video yako inatakuwa iwe fupi na inayovutia yenye urefu wa Kati ya sekunde 30 Hadi 60. Video hii itakuwa ikionekana kwa watu wote ambao hawajajiunga (subscribe) na channel yako na itakuwa ikitoa maelezo kwa ufupi kuwa channel yako inahusika na Nini na watu wategemee kupata ujumbe au maarifa gani watakapojiunga na channel yako. Mwisho wa video, usisahau kuwakumbusha watu kujiunga na channel yako.
  • Weka anuani ya channel yako inayofanana na Jina la Channel yako (channel URL):  Unapokuwa umeanzisha channel yako, anuani ya channel yako huwa inaanza na YouTube na kufuata na herufi nyingi pamoja na namba ambazo hazipo kwenye mpangilio maalumu kiasi kwamba sio rahisi kwa mtu kukumbuka anuani ya channel yako. Baada ya kuwa umefikisha Subscriber 100, na channel yako ikawa na umri wa siku 30, unaweza kubadilisha anuani iliyokuwepo na kuweka anuani ambayo watu wataikumbuka. Kwa mfano, Kama channel yako inaitwa Ujuzi academy, basi, unaweza kubadili channel yako na kusomeka hivi: YouTube/ujuziacademy.
  • Unaweza kujifunza zaidi kwa kutembelea custom YouTube URLs hapae.
  • Weka link mbalimbali: Kwenye sehemu ya “About” weka link za mitandao yako yote ya kijamii pamoja na tovuti yako ili kuwarahisishia watazamaji kuweza kuwasilisha na wewe kwa urahisi.
  • Jinsi ya kuandaa video kwa ajili ya kuziweka YouTube

Sasa channel yako iko tayari na hivyo ni wakati wa kuanza kuandaa na kuweka video kwenye Channel yako ya YouTube.

Katika sehemu hii nitazungumzia aina mbalimbali za video ambazo unaweza kuziandaa na kuziweka YouTube. Pia nitazungumzia jinsi ya kurekodi video hizo pamoja na kuedit.

Aina 8 za video ambazo unaweza kuziandaa na kuziweka YouTube.

Kabla ya kuanza kuandaa video, unatakiwa kuamua ni aina gani ya video unayotakiwa kuandaa ili kutimiza lengo lako. Zifuatazo ni aina za video ambazo unaweza kuandaa.

1. Shuhuda za wateja (Customer Testimonials)

Shuhuda za wateja ni video fupi ambazo huwa katika mfumo wa mahojiano(interviews) kwa wateja waliofurahishwa na bidhaa zako kama kuna bidhaa unauza. Video hizi zenye Shuhuda mbalimbali za wateja wako huifanya biashara, bidhaa au huduma unayotoa kuaminika zaidi na hivyo kuvutia wateja wengi zaidi.

2. Kuelezea ubora na jinsi ya kutumia bidhaa (Product Demonstration Videos)

Hizi ni video fupi zinazoelezea bidhaa unayouza, manufaa yake na jinsi ya kuitumia.

3. Video za mafunzo (Explainer and Tutorial Videos)

Hizi ni video ndefu zinazotoa mafunzo mbalimbali. Hivyo unaweza kuwa unaandaa video za kufundisha watu ujuzi ulionao.

4. Mahojiano na mtaalamu (Thought Leader Interviews)

Hapa unaweza kutafuta mtaalamu wa mada unayotaka kufundisha na ukachukua video ukiwa unafanya nae mahojiano kuhusiana na mada hiyo.

5. YouTube mubashara (YouTube Live)

Hapa unafundisha ujuzi wako mubashara ukiwa YouTube na watu wakakuangalia moja kwa moja. Unapokuwa unafundisha, watu wanaweza kukomenti na kuuliza maswali na ukawajibu muda huohuo.

Ili uweze kuwa live kwenye channel yako ya YouTube, bofya kitufe Cha kamera kilichopo sehemu ya juu upande wa kulia wa channel yako Kisha Chagua Go live.

Jinsi unavyoweza kuanzisha Youtube channel na kutengeneza kipato.

6. Video za makala za Blog

Hizi ni video ambazo unaweza kuzirekodi kutokana na makala zako ambazo huwa unaandika kwenye blog yako. Hivyo, Kama una blog na unaandika makala mara kwa mara, unaweza kutumia makala zako kuandaa video ambazo utaziweka YouTube. Hii itawasaidia hata wale ambao huwa ni wavivu kusoma wapate maarifa yako kupitia video.

Hatua kwa hatua jinsi ya kuandaa video

1. Tambua lengo la video yako (define your goal).

Kama ilivyo kwa aina nyingine za makala, ni lazima unapokuwa unaandaa video yako uwe na lengo unalotaka kulitimiza kupitia video yako.

Je unahitaji kutangaza brand yako ili ifahamike zaidi, kuongeza watembeleaji kwenye tovuti yako au kuongeza subscribers kwenye channel yako?

Katika Kila video unayotengeneza, hakikisha kuwa unakuwa na lengo moja unakikusudia kulikamilisha.

2. Andaa andiko la video yako (Video Script)

Hapa unaandika kila kitu unachoenda kuongea wakati unarekodi video yako. Kwa mfano: Karibu mpendwa mtazamaji katika channel yetu. Leo nitazungumzia juu ya jinsi ya kuanzisha biashara Mtandaoni. Nitaelezea hatua kwa hatua na hivyo basi, kufikia mwisho wa video hii Utaweza kuanzisha biashara yako na kutengeneza kipato.

Karibu katika somo ili tuweze kujifunza kuanzia mwanzo Hadi mwisho. Jina langu naitwa Kingi Kigongo, Karibu tujifunze………………………………………………

3. Andaa jedwali litakaloonesha jinsi video yako

itakavyokuwa(storyboard)

Baada ya kuwa umeainisha lengo la video yako, na tayari umeandika kila kitu unachoenda kuongea, sasa ni wakati wa kuandaa jinsi video yako itakavyoonekana. Utaweza kufanya hivyo kwa kuandaa jedwali litakalokuongoza hatua kwa hatua (storyboard). Jedwali hili litakuongoza maneno utakayosema na vitendo utakavyofanya kwa Kila hatua ya video yako. Ufuatao Ni mfano wa jedwali (storyboard)

HATUAMANENO UTAKAYOZUNGUMZAVITENDO
1.Karibu mpendwa mtazamaji katika channel yetu. Leo nitazungumzia juu ya jinsi ya kuanzisha biashara Mtandaoni. Nitaelezea hatua kwa hatua na hivyo basi, kufikia mwisho wa video hii Utaweza kuanzisha biashara yako na kutengeneza kipato. Karibu katika somo ili tuweze kujifunza kuanzia mwanzo Hadi mwisho. Jina langu naitwa Kingi Kigongo, Karibu tujifunze.Nitakuwa nimekaa nikiongea huku nimeangalia moja kwa moja Kwenye kamera au Simu ninayotumia kurekodia.
  2.Sasa hebu tuangalie njia ambazo unaweza kuzitumia kuanzisha na kumiliki biashara yako mtandaoni. Njia ya kwanza ni kuanzisha na kumiliki Youtube channel. Ili uweze kuanzisha Youtube channel fuata maelekezo yafuatayo.Nitakuwa nimesimama nikiandika kwenye ubao hatua za kufuata kuanzisha youtube channel.
3.……………………………….
4.………………………………..
5.…………………………………

Kila hatua ya storyboard ni kipande cha video (slide). Baada ya kuwa umemaliza kurekodi, utakuwa umerekodi vipande(slides) vingi vya video ambavyo utaviunganisha kwa kutumia video editor na kutengeneza video ndefu nzuri na yenye vitendo vya aina mbalimbali ambavyo vitavuta usikivu kwa watazamaji wako.

3. Baada ya kuwa umerekodi video yako, unaweza kuongezea viambata vingine kwenye video yako.

Hapa unaweza kuweka slide yenye kichwa cha habari cha video yako, pia unaweza kuongeza kitu kingine chochote ambacho unahisi kitaifanya video yako iwe yenye kuvutia.

4. Amua urefu wa video yako.

Unapokuwa unaandaa script na storyboard yako, pia unatakiwa kuzingatia urefu wa video yako. Lazima uamue unataka kuandaa video yenye urefu gani kulingana na maudhui unayotaka kuyafikisha kupitia video yako.

5. Edit video yako.

Kuna software nyingi ambazo unaweza kuzitumia kuedit video yako. Zingine ni za bure na zingine ni za kulipia. Mfano wa software za bure ni kama vile openshot, iMovie, Windows Movie Maker na kadhalika. Pia kuna software zingine ambazo ni za kulipia. Mfano wa software hizo ni Final Cut Pro X, Adobe Premiere CC, na kadhalika. Pia unaweza kutumia software za mtandaoni kuedit video yako. Miongoni wa platform ambazo unaweza kuzitumia kuedit video yako ukiwa mtandaoni ni kama vile Canva, clipchamp na kadhalika.

Weka Thumbnails kwenye video zako.

Thumbnail ni picha inayoonekana juu unapokuwa umeweka video youtube. Kabla ya kuweka video yako youtube, hakikisha umetengeneza thumbnail nzuri. Thumbnail itavutia watazamaji kuweza kufungua na kuangalia video yako.

  • Jinsi ya kufanya video zako ziweze kuonekana kwa urahisi watu wanapotafuta Mtandaoni (YouTube Videos Search Engine Optimization (SEO))

Sasa, tayari channel yako iko mtandaoni. Hebu nizungumzie jinsi ya kuzifanya video zako ziweze kuonekana kwa urahisi watu wanapotafuta mtandaoni.

Kama nilivyoelezea mwanzo kuwa mtandao wa YouTube ni wa pili kwa ukubwa Baada ya Google. Japokuwa kuandaa video zenye ubora ni jambo muhimu sana, hata hivyo kwa hilo tu sio kigezo cha kuwa na mafanikio kwenye channel yako. Ili channel yako iweze kuwa na mafanikio, inatakiwa kutembelewa na watu wengi. Hivyo ni jambo la muhimu kuhakikisha kuwa video zako zinaonekana kwa urahisi mtandaoni.

Hatua ya Kwanza kabisa ni kuweka maelezo yanayofafanua video yako. Maelezo hayo yanajumuisha kichwa cha habari cha video yako (video tittle), ufafanuzi (video description), video yako inahusiana na nini (tags), vichwa vya habari vidogo (subtitles) na picha ya video yako (thumbnail).

Unapokuwa umeweka taarifa sahihi kuhusiana na video yako, kutaifanya video yako ionekane kwa urahisi mara tu watu wanapokuwa wanatafuta mtandaoni taarifa zinazowiana na video yako.

Kichwa Cha Habari

Ni vizuri kuhakikisha video zako zinaonekana vizuri na kwa urahisi kwa kuweka vichwa vya habari vinavyowiana na maudhui ya video yako (optimize your video’s title and description).Kichwa Cha Habari Cha video yako ndio kitu Cha Kwanza kabisa ambacho watu watakiona kabla ya kuamua kuangalia video yako au la. Hivyo hakikisha Kichwa Cha Habari kinalenga kutatua matatizo ya watazamaji wako.

Fanya utafiti ili uweze kufahamu ni mambo gani watu huwa wanatafuta suluhisho mtandaoni yanayoendana na maudhui ya video zako (keyword research) ili uweze kuweka Kichwa Cha Habari kinachoendana na Mambo ambayo watu hutafuta mtandaoni.  Jambo la mwisho, hakikisha unapokuwa unaandika kichwa Cha habari kiwe na herufi zisizozidi 60 ili kufanya Kichwa chako cha habari kionekane chote mtandaoni bila kukata maandishi.

Maelezo ya Video.

YouTube huwa inaonesha maelezo yenye herufi zisizozidi 100 ambazo Ni mistari ya Kwanza miwili mpaka mitatu. Ukizidisha maneno, YouTube huwa inakata maneno na kuandika “Show more” hivyo ili mtazamaji aweze kusoma maelezo yote, atalazimika kubofya maneno hayo.

Weka Tags.

Baadaye, Weka maneno ya muhimu yanayobeba ujumbe wa video yako (tags).

Ainisha kundi (category) la video yako.

Baada ya kuwa umeweka video yako kwenye mtandao wa YouTube, unatakiwa kuainisha aina ya video uliyoweka. Utaweza kufanya hivyo kwa kwenda sehemu iliyoandikwa Manage Videos.

Jinsi unavyoweza kuanzisha Youtube channel na kutengeneza kipato.

Ili kuchagua kundi unalotaka kuweka video yako, chagua sehemu iliyoandikwa Manage videos.

Kisha bofya sehemu liyoandikwa edit kama inavyoonekana hapa chini:

Kwenye maneno yaliyotokea, Chagua category

Jinsi unavyoweza kuanzisha Youtube channel na kutengeneza kipato.

YouTube inakuwezesha kuweka video yako kwenye miongoni mwa makundi yafuatayo: Muvi (Film & Animation), Vyombo vya moto (Autos & Vehicles), Muziki(Music), Wanyama (Pets & Animals), Michezo(Sports), Safari (Travel & Events), Magemu(Gaming), watu na blog (People & Blogs), Vichekesho(Comedy), Burudani na Siasa (Entertainment & Politics), Video za mafunzo (How-to & Style, Educations), Sayansi na teknolojia (Science & Technology) na Misaada (Nonprofits & Activism).

Weka picha kwenye kava ya video yako (Thumbnail)

Thumbnail ndio picha ambayo huwa inaonekana kabla mtu hajafungua video yako. Hapa unatakiwa kuweka picha nzuri lakini inayoendana na maudhui ya video yako ili kuvutia watu kubofya na kuangalia. YouTube pia huwa inatengeneza picha ambayo itaonekana juu ya video yako bila wewe kuhangaika kufanya chochote, lakini ninakushauri wewe mwenyewe utengeneze picha yako nzuri ambayo unahisi itawavutia watembeleaji wa YouTube na hivyo kupata watazamaji wengi.

Kwa mujibu wa Ripoti za YouTube, inakadiriwa kuwa  “90% ya video zote zinazofanya vizuri kwa kupata watembeleaji wengi zinatumia thumbnail zilizotengenezwa na kuboreshwa (custom thumbnails)”. Hivyo, Unapokuwa umeweka video yako YouTube, Hakikisha unaweka picha nzuriambayo itavutia watazamaji. YouTube inapendekeza picha yako iwe na vipimo vya 1280 x 720 px ili iweze kuonekana vyema kwenye aina zote za vifaa vya kielectronic.

Muhimu: Ili uweze kuweka picha ya thumbnail uliyotengeneza mwenyewe, unatakiwa kwanza uihakikishie YouTube kuwa channel unayoweka video ni ya kwako (verify your YouTube account). Unaweza kufanya hivyo kwa kutembelea youtube.com/verify baadaye utatumiwa ujumbe wenye herufi na namba  (verification code ) kwenye Simu yako. Kisha utafuata maelekezo kukamilisha zoezi Hilo.

Jinsi ya kuweka video kwenye makundi kulingana na maudhui(Playlists)

Je unaandaa video zenye maudhui yanayofanana? Kuweka video zako kwenye Playlists ni jambo la muhimu sana kwako. Playlist inakuwezesha kuweka video zinazofanana kimaudhui kwenye kundi moja ambapo mtazamaji anaweza kuangalia video kuanzia ya Kwanza mpaka ya mwisho.

Ili uweze kutengeneza Playlist, Nenda kwenye video unayotaka kuiweka kwenye playlist na ubofye kwenye dot tatu zinazoonekana mbele ya video. Hapo yatatokea maneno kama yanavyoonekana kwenye picha hapa chini, halafu chagua save to playlist. Kwa sababu utakuwa hauna playlist yoyote chagua create a playslist.

Jinsi unavyoweza kuanzisha Youtube channel na kutengeneza kipato.
Jinsi unavyoweza kuanzisha Youtube channel na kutengeneza kipato.
  • Jinsi ya kutangaza channel yako ya YouTube.

Sasa tayari umeshaandaa video yako na kuiweka youtube. Hatua inayofuata ni kuitangaza channel yako ili uweze kupata watazamaji wengi. Hivyo ili uweze kupata watazamaji wengi, ni lazima utangaze channel yako. Zifuatazo ni njia mbalimbali ambazo unaweza kuzitumia kutangaza channel yako na ukapata watazamaji.

Tangaza channel yako kupitia mitandao ya kijamii.

Kutumia mitandao ya kijamii kutangaza video zako ni njia nzuri na rahisi ya kupata watazamaji wengi kwenye video zako. Ili uweze kushare video yako kwenye mitandao ya kijamii, bofya sehemu iliyoandikwa share iliyopo chini ya video yako. Baada ya hapo utachagua ni mtandao gani wa kijamii unaotaka kushare video yako. Pia unaweza kukopi link ya video yako na kwenda kuiweka mahali popote unapotaka video yako iweze kuonekana.

Unapokuwa unashare video zako kwenye mitandao ya kijamii, usiweke link kavu isiyokuwa na maelezo. Njia nzuri na yenye mafanikio ni ile ya kuelezea kwanza mada inayotatua tatizo linaloendana na maudhui ya video yako kisha unawaelekeza watu kwenye link uliyoiweka ili wakajifunze zaidi maarifa unayofundisha.

Anzisha Blog au Tovuti.

Njia nyingine ni kutangaza video zako kupitia blog au tovuti. Katika njia hii, unatakiwa kuanzisha blog yako ambayo utakuwa ukiandika Makala mbalimbali zinazoelimisha jamii zinazoendana na maudhui ya video zako. Kila unapoandika Makala utakuwa unaweka na video inayoendana na Makala yako na hivyo kwa kutumia njia hiyo utaweza kuongeza watazamaji wa video zako. Kitendo cha kuweka video kwenye Makala zako siyo tu zitaongeza watazamaji kwenye video zako bali pia zitaongeza watembeleaji wa blog yako. Unaweza kufanya hivyo kwa kukopi link iliyoko kwenye video yako ya youtube na kuipaste kwenye Makala yako. Kitendo hiki kinaitwa kwa kingereza embedding.

Unaweza kuangalia pia hatua kwa hatua jinsi ya kuembed video ya youtube kwenye blog yako. 

Kutumia njia ya barua pepe (email)

Kama una blog na tayari una watu ambao wamejiunga (subscribe) kupata makala mbalimbali kwenye blog yako, unaweza kuwa unawatumia kwenye email zao taarifa kila mara unapokuwa umeweka video mpya kwenye channel yako.

Kujibu maoni na maswali ya watazamaji wako.

Jambo la mwisho lakini la muhimu, hakikisha unajibu maoni na maswali ya watazamaji wako. Pia wahamasishe watazamaji wako kutoa maoni yako kuhusiana na mada uliyofundisha kwenye kila video yako. Kumbuka kuwa, kuanzisha YouTube Channel ni njia nzuri ya kukuunganisha na watu, hivyo unapokuwa unajibu maoni yao unakuza mahusiano.

Njia 8 za kukuza channel yako ya Youtube.

Sehemu iliyopita tumeangalia jinsi ya kutangaza video zako na kupata watazamaji wengi. Katika sehemu hii, tutaangalia mambo manane ya kuzingatia ili kukuza channel yako ya YouTube.

  1. Hakikisha jina (brand) la channel yako linafanana kwenye mitandao yako yote ya kijamii.
  2. Hakikisha video zako zinapatikana kwa urahisi mtandaoni watu wanapokuwa wanazitafuta (search engine optimization (SEO)) kwa kufuata hatua nilizoelezea hapo juu kwenye Makala hii.
  3. Jirekodi au tumia watu halisi au vikaragosi (animated faces) kwenye video zako badala ya kurekodi maandishi pekee.
  4. Chagua picha(thumbnail) nzuri inayoendana na maudhui ya video yako.
  5. Toa wito (calls-to-action (CTAs)) ili watu wachukue hatua baada ya kuangalia video zako. Unaweza kuwahamasisha wasubscribe kwenye channel yako, watembelee blog yako au wanunue bidhaa au wajiunge na huduma unayotoa.
  6. Wahamasishe watazamaji wako kuwashirikisha (share) marafiki zao video zako.
  7. Weka mwendelezo wa video (playlists) kwa video zinazoelezea ujuzi au maarifa yanayoshabihiana.
  8. Kuwa na ratiba ya kuweka video kwenye channel yako na ujizatiti kuifuata.
Jinsi unavyoweza kuanzisha Youtube channel na kutengeneza kipato.

Jinsi ya kupima na kutathmini maendeleo ya Channel yako (YouTube Analytics)

Tayari umetumia muda na nguvu nyingi kuanzisha channel ya YouTube na kuanza kuweka video, sasa ni wakati wa kupima na kufanya tathmini ya maendeleo ya channel yako. Ili uweze kufahamu maendeleo ya channel yako kama vile kuona unaweza kufungua kwenye YouTube Analytics. Hapo utaona idadi ya watu walioangalia video zako (views), muda waliotumia kuangalia video zako (watch hours), ni kwa kiwango gani watu wanaangalia video zako kuanzia mwanzo mpaka mwisho (retention rate), maeneo wanayotoka watazamaji wako (Traffic Sources), umri wa watazamaji wa video zako (demographics) na kadhalika.

Sasa, ili uweze kupima vizuri maendeleo ya channel yako, unatakiwa kufuata hatua zifuatazo:

1. Tambua lengo au dhumuni la wewe kuanzisha Channel.

Jambo la Kwanza kabisa unatakiwa utambue lengo lako la kuanzisha Channel ya YouTube. Huwezi kupima mafanikio bila kuwa na malengo. Malengo ndiyo yatakayokuonesha Kama channel yako inakua au la. Kuna malengo ya Aina nyingi, inawezekana ukawa na malengo ya kuongeza mauzo kwenye biashara yako kwa kuitangaza kupitia YouTube, kuongeza subscribers, kutengeneza kipato kupitia matangazo ya Google Adsence, na kadhalika. Hata Kama una malengo mengi kwenye Channel yako, hakikisha kuwa kila unapoandaa video yako moja, iwe na lengo moja. Usiweke malengo mengi kwenye video moja.

2. Pima ukuaji wa channel yako kwa kuangalia viashiria vya ukuaji.

Baada ya kuwa umetambua lengo la video au channel yako, sasa unaweza kutumia viashiria mbalimbali kupima maendeleo na ukuaji wa channel yako. Ili uweze kupima maendeleo ya channel yako, nenda sehemu ya  youtube.com/analytics. Baada ya kuwa umeingia mahali hapo, sasa unaweza kuangalia vitu vifuatavyo ambavyo ni viashiria vya ukuaji wa channel yako.

Watch time:  watch time ni jumla ya muda wote ambao watu wametumia kuangalia video zako zote za channel nzima na pia unaweza kuangalia muda waliotumia kuagalia kwa kila video yako.

retention rate:  retention rate ni asilimia ya watu ambao wameangalia video yako kuanzia mwanzo mpaka mwisho.

Traffic Sources: Traffic sources ni maeneo ambayo watazamaji wa video zako wametokea. Hapa inawezekana watazamaji wako wakawa wametokea youtube, kwenye mitandao ya kijamii kama vile facebook, twitter na kadhalika baada ya kuwa umeshea video zako au wengine wanaweza kutokea Google na kadhalika.

Demographics: Demographics ni ripoti inayoonesha umri na jinsia za watazamaji wa video zako. Ripoti hii inasaidia kuangalia ni watu wa aina gani wanapenda kuangalia video zako na hivyo kuweza kuboresha Zaidi na pia kuamua ni bidhaa au huduma gani unaweza kutoa kulenga makundi hayo ya watu.

Software zinarahisisha kutangaza na kukuza channel yako ya YouTube.

Ili uweze kukuza channel yako kwa urahisi na haraka, kuna software ambazo zinaweza kukusaidia kukuza channel yako kwa haraka. Software hizi ni VidIQ na Tubebuddy. Nitaelezea Tubebbudy kwa kuwa nina uzoefu nayo.

1. Tubebbudy

 Jinsi unavyoweza kuanzisha Youtube channel na kutengeneza kipato.

Tubebuddy ni software inayokusaidia kufahamu watu wanatafuta hasa nini mtandaoni (Keyword Inspector Tool).

na hivyo kukuwezesha kuandaa video zinazoendana na vile vitu watu wanavyovitafuta na hivyo kukuwezesha kupata watazamaji wengi. Kwa kutumia software hii utawezesha video zako kupata watazamaji wengi na kwa muda mfupi na hivyo kukuza channel yako kwa haraka.

Mambo ya kuzingatia ili uweze kukuza channel yako.

1. Weka ratiba maalumu ya kuweka Makala na uiheshimu. Kumbuka kuwa, watu waliosubscribe channel yako, wanategemea kupata maarifa mapya mara kwa mara kupitia channel yako. Hivyo unapokuwa umeweka ratiba inayoeleweka ya kuweka video zako, watu watakuwa wakitembelea channel yako ili kupata video mpya kulingana na ratiba yako uliyoiweka. Moja ya makosa makubwa ambayo wamiliki wa channel za YouTube hufanya wanapoanzisha channel zao ni kutokuwa na ratiba maalumu ya kuweka video. Ni afadhali ukawa na ratiba ya kuweka video moja kwa juma kuliko kuweka video kila siku kwa majuma mawili halafu baadaye ukaacha ghafla.

2. Uwe na kamera ya kuchukulia video kabla ya kuanzisha channel ya YouTube.

Hapa inategemea na uwezo wako wa kifedha. Unaweza kununua kamera au ukatumia smartphone yako kuchukulia video zako. Hajalishi utaamua kutumia kamera au Smartphone, jambo la kuzingatia ni kuwa, kabla haujaamua kuanzisha YouTube channel yako unapaswa kuwa tayari una kifaa kitakachokusaidia kuchukulia video zako.

3. Weka malengo ya jinsi utakavyotengeneza kipato kupitia Channel yako.

Hapa lazima ufahamu jinsi utakavyotengeneza kipato kupitia channel yako. Inawezekana ukawa na bidhaa au huduma unayotaka kuwauzia watazamaji wako au kutengeneza kipato kupitia matangazo ya Google AdSense. Kama unataka kutengeneza kipato kupitia matangazo ya Google AdSense, ni lazima ufahamu mfumo unavyotumika. Kwa kawaida Wamiliki wa YouTube hupata 68% ya mapato ya matangazo ya AdSense yanayoonekana kwenye channel zao kutoka Google.  Ili uweze kukidhi vigezo vya kutengeneza pesa kupitia matangazo ya youtube (Google adsence), channel yako inatakiwa ifikishe subscribers kuanzia 1000 na masaa ya watu kuangalia video (watch hours) zako yafikie 4000 ndani ya mwaka mmoja.

Sasa ni wakati wa kuchukua hatua.

Ikiwa na  watembeleaji  billion 2.1, YouTube sio tu sehemu ambayo unaweza kuingia na kuangalia video kwa ajili ya kujiburudisha, bali ni sehemu ambayo unaweza kuitumia kuanzisha biashara, ukajiajiri na kutengeneza kipato. Hivyo, tumia fursa hii uanzishe biashara yako bila kuwa na mtaji mkubwa wa pesa na bila kuathiri muda wako wa majukumu mengine ya kazi.

Ni matumaini yangu kuwa umepata maarifa ya kutosha kupitia mwongozo huu ambao utakuwezesha kuanzisha YouTube Channel. Usisite kuwashirikisha ndugu, jamaa na marafiki maarifa haya kwa kushare kwenye mitandao ya kijamii. Kama una maoni yoyote usisite kundika maoni yako hapa chini. Pia kama unahitaji nikutengenezee channel ya YouTube au unahitaji ushauri, usisite kuwasiliana nami moja kwa moja kupitia namba 0752 081669.

Asante sana na karibu kwenye Makala zangu zinazokuja.

Kingi Kigongo
Ungana nae
Latest posts by Kingi Kigongo (see all)

26 Replies to “Jinsi Ya Kuanzisha YouTube Channel Na Kutengeneza Kipato.”

    1. Asante sana kwa kufuatilia makala hii. Ili uweze kukidhi vigezo vya kuanza kulipwa nimeielezea kwenye makala hii kuwa ni lazima channel yako ifikishe subscribers kuanzia 1000 na masaa ya watu kuangalia video (watch hours) zako yafikie 4000 ndani ya mwaka mmoja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error

Enjoy this blog? Please spread the word :)

Follow by Email
WhatsApp